Wana weweseka tu, si unajua hata taifa stars ikifungwa na Timu ya taifa ya BRAZIL, utawasikia wanatoa sababu za kufungwa as if walidhani kuwa wangeshinda. CCM haina uwezo wa kupambana na CHADEMA tukiondoa polisi na usalama wa taifa, ndiyo maana kila kitu kinachofanyika wanahisi kuwa CHADEMA wako nyuma yake kwa sababu ndiyo chama pekee ambacho kinaweza kuwahamasisha watu wakahamasika kutekeleza maazimio ya chama. Ni halali kwa ccm kufikiri kuitupia lawama CHADEMA, hawana namna nyingine, upeo wao umeishia hapo, wao wameicha kufikiri kuwa matatizo ya watz yamepelekea watz kuichukia nchi yao, wao wanaona adui yao mkubwa na mchonganishi wao na watz ni CHADEMA. Hizo zote ni dalili za dola inayoanguka.