Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Makamanda wa CHADEMA hawana raha kabisa. Wamejikunyata kama kifaranga aliyenyeshewa mvua. Hii ni baada ya tamko la Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka kutangaza tarehe ya Rais Magufuli kukabidhiwa chama kuwa ni tarehe 23 Julai.
Makamanda wamejawa na huzuni kuu kwani wanajua dhahiri kuwa sasa Magufuli atavaa kofia mbili. Yaani Mwenyekiti wa chama tawala na Rais wa nchi. Hili ni pigo kubwa kwao. Kama mnavyokumbuka, mgombea wa CHADEMA, Edward Lowasa akiwa CCM alitoa masharti kwamba ikiwa ataukosa Urais, basi apewe uenyekiti wa chama. Hakuna aliyemsikiliza na hatimaye akahama chama. Baada ya kuondoka kwake, vibaraka wake waliomo ndani ya CCM wakaendelea kupaza sauti na sasa wanaumgwa mkono na Makamanda wa CHADEMA kuwa Magufuli asikabidhiwe chama.
Jitihada zinaonekana za dhahiri hasa kutokana na matamko mfululizo wanayotoa wakisaidiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa wataenda Dodoma kuzuia mkutano wa CCM. Swali la kujiuliza, ni kwa nini hawa Makamanda wanamuogopa sana JPM? Wao si makamanda? Yaani wametishika tu na push up za Magufuli na sasa wanahaha ili asivae kofia mbili?
Wamevurugwa. CCM ndicho chama dola. Tunafanya tutakavyo na hakuna wa kutuzuia. Wengine wote lazima mfuate taratibu zetu