Kwanini CHADEMA wanafukuzana wenyewe

Kwanini CHADEMA wanafukuzana wenyewe

Zee la kitaa

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2017
Posts
403
Reaction score
211
Nimekuwa nafuatilia mienendo ya vyama mbalimbali nchini nikagundua kufukuzana sio jambo jipya katika vyama hivi.

Kilichonishangaza zaidi ni idadi ya wanachama waliofukuzwa chama cha demokrasia na maendeleo kuwa wengi ikilinganishwa na chama kingine chochote nchini.

Sasa sijajua chanzo ni usaliti ama kukosa weredi katika kuongoza chama husika.

Kila chama kina kanuni za kushughulikia wanachama wanaokiuka maadili na mienendo ya chama na kumfukuza mwanachama inakuwa ni suala la mwisho kabisa baada ya mambo mengi kufanyika ikiwemo kupewa onyo ama la.

Ushauri mdogo tu vyama vya siasa viimarishe demokrasia ndani ndipo vijitokeze kudai demokrasia na uhuru wa kutoa maoni katika taifa.

Kama haitakuwa hivyo tutakuwa hatuna uhalali wa kudai kitu ambacho katika vyama vyetu hatufanyi.

Naomba kuwasilisha
 
kwa kuwa malaika ndio chanzo cha idadi kubwa ya wanachama kufukuzwa. Kwa hiyo hataki kukusolewa ama kuambiwa lolote?
Samahani mkuu hili ni swali?,ukitoa hio alama ya kuuliza utapata jibu lako kwa usahihi kabisa.
 
Hiyo ndio formula ya vyama vya siasa vya upinzani Tanzania na wao Mda wao ndio umefika wa kufanya hayo

NCCR ilivyofika ktk pick walifukuzana
CUF ilivyofika katika pick walifukuzana

Sasa ni zamu ya CHADEMA maana wao ndio wapo katika pick

Mbunge wa CHADEMA usipo jiweka carantine unafukuzwa uanachama
 
Kwn ccm wao huwa hawafukuzani?? kwahiyo mtu akienda kinyume na katiba ya chama aachwe tu??? Kwn maisha hayaendi bila kuitaja au kuiandika chadema???
 
Ishu sio wao kufukuzana, kuna nguvu kubwa wanapambana nayo kutoka nje.

Pesa
Kuahidiwa madaraka
Kufunguliwa kesi na kupewa msukosuko
Vitisho vya kuuwawa
Kufungwa jela

Sio CHADEMA tu hata wewe unaweza kumsaliti mkeo ikiwa hujajitoa kupambana na hayo ya juu.
 
Kwani Membe alifukuzwa na Chadema?
 
Kwn ccm wao huwa hawafukuzani?? kwahiyo mtu akienda kinyume na katiba ya chama aachwe tu??? Kwn maisha hayaendi bila kuitaja au kuiandika chadema???
Ka hiyo kutokukaa quarantine ni kinyume cha katiba ya chadomo?
 
mtaandika wee lkn mwaka huu mtashangaa na roho zenu za kishetwani
 
Hiyo idadi ya hao wanachama wengi waliofukuzwa huko Chadema una hesabu yake kamili ukilinganisha na vyama vingine vya siasa?
 
Kwn ccm wao huwa hawafukuzani?? kwahiyo mtu akienda kinyume na katiba ya chama aachwe tu??? Kwn maisha hayaendi bila kuitaja au kuiandika chadema???
Chadema hamna mtu aliyefukuzwa. Mlifanya maigizo ya kuwafukuza baada ya kujua wameshaondoka. Nani akae katika mazingira ya kisiasa kama yale?
 
Back
Top Bottom