Kwanini chadema ninawakubali kwa%100? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini chadema ninawakubali kwa%100?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ebaeban, Mar 17, 2012.

 1. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,834
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Tafiti ni shughuli (activity) ambazo hufanywa na wasomi wa inchi husika, na mala nyingi matokeo ya tafiti hizo ni hupelekea mabadiliko chanya katika jamii husika , mabadiliko hayo yanaweza kuwa ya kiuchumi, kisiasa ,kiutamaduni na hata kijeshi aidha tafiti huweza kulisaidia taifa kubuni sera au kutunga sheria zenye kulenga kuwaletea wanachi wake maendeleo ya haraka. Mfano tafiti za mbegu bora ili mkulima apate mazao mengi aongezee kipato na hatimae awe na maisha bora, utafiti wabreeds za ng`ombe wanaotoa maziwa mengi, tafiti za chanjo za kuzuia magonjwa ili mwanainchi atumie kipato chake kujiletea maendeleo na wala si kujitibia magonjwa n,k,. Sasa CCM imejenga mazingira ambayo wasomi wengi wameona kuwa kwenye maeneo yao hakuna tija mahala pazuri penye kujiletea maendeleo ya haraka ni kwenye siasa,hivyo basi wanaviacha vitengo vyao wanakimbilia siasa ili kupata malisho ya kijani kwa kisingizio eti wanaenda kutumia elimu zao kuwaletea wanainchi wao maendeleo wakati dhana hiyo ni kinyume kabisa, Kimsingi pale walipokimbia ndiao hasa wanawatumikia wanainchi na kuwawezesha kupata maendeleo ya haraka. SERIKALI YA CCM IMEFANYA SIASA MAHALI PA KUPATIA MASLAHI MAZURI KABISA YANAYOMFANYA MWANASIASA AISHI KAMA PEPONI WAKIONA KIPATO HAKITOSHI BAADA YA MSHAHARA WOTE KUKATWA BAADA YA KUKOPA SHANGINGI WANAAMUA KUONGEZA POSHO. Siasa inameza watafiti sasa utafiti utafanywa na nani? Matokeo yake


  1. Wasomi wanakimbilia siasa watu kama Pro. Salungi, Mwakyusa Mwandosya, Msolla na wengine hawa huku kwenye siasa wameingia choo cha kike kiutumishi kwa manufaa ya wanainchi wenge ilifaa wabaki kulekule kwenye vitengo vyao,
  2. Wafanya biashara ambao ndio walipa kodi wakubwa nao wakajitoma kwenye siasa kupitia CCM eti wanaipenda (uwongo ) matokeo yake kwa sababu za kiufundi hawailipi serikali kodi vizuri kwa privilege ya lobbing, kodi ambayo ingeisaidia serikali kuwaletea wananchi maendeleo inapotea kwa sababu ya walipa kodi wakubwa kuwa eti wabunge, hapa nalenga watu kama Ahmed Shabib, Murji, Abood, Mohamed Dewji na wengine wataje. Mswada wa kutenganisha biashara na siasa mpaka sasa uko wapi?
  3. Matapeli na majizi nao wakajikita kwenye siasa kwa kupitia CCM eti wanaipenda nia wakifanya utapeli wao wawe na ka immunity Fulani hapa nalenga waliotoka FAT na kwenda kuwarubuni wanyamwezi maskini ya mungu.

  Sasa CHADEMA inataka kufanya kinyume chake, ina nia ya kufanya siasa kiwe kitengo ambacho kitakuwa na maslahi ya kawaida kabisa na yasiyo na faida ili watu watakao taka kuwa wanasiasa wawe na wito na kazi hiyo. Mfano wameipiga vita posho (sitting allowance) kwa nguvu zote matokeo yake kila mwenye macho ameona, na sasa juzi kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo Arumeru walitembeza bakuli ili kukiwezesha chama kufanya kampeni , kwa wenye akili nyingi kama sisi jamvini hiyo ni geresha tu nia hapa ni kuanza kuvuta kasi hatimae kuanza kuzipiga vita ruzuku za vyama ili vyama vijitegemee visingoje kodi ya wanaichi mwisho wa siku hela za ruzuku ya vyama iende moja kwa moja kuwaletea maendeleo wanainchi wao kwani ushaidi mkubwa wa kimazingira ruzuku kubwa wanayopata CCM inaishia kwa akina Mwigulu Nchemba kuhonga wanawake za watu tu.


  Tuwaunge mkono CHADEMA wanaona mbali.

  Great thinker unasemeje, saidia basi ARUMERU wafanye uamuzi sahihi,
   
 2. t

  tumpale JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 201
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana kimsingi, wataalamu sio kwamba wanapenda kukimbilia siasa kama inavyotafsiriwa bali wasomi wanapuuzwa na kudharauliwana wanasiasa, mfano madaktari wanasumbuliwa na akina mizengo, mponda, jakaya, makinda na wengine. hiyo inawalazimu kwenda kwenye siasa hukohuko ili wakapambane, wakiamini kuwa wana uwezo mkubwa sana ukilinganisha na wanasiasa uchwara waliopo. ushauri wangu, ili wasomi wasikimbilie kwenye siasa kuwekwe mkakati kuhakikisha maslahi na heshima ya wasomi isimamiwe na wasomi wenyewe na si wanasiasa.
   
 3. c

  collezione JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  This is what am always saying. Asante sana kufikisha huu ujumbe
   
 4. c

  collezione JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  CCM inafanya hii nchi tuabudu siasa. Kila kitu leo hii ni siasa.

  Umeme umekuwa siasa, barabara zimekuwa siasa. Madini, Huduma za afya (madaktari) nako kuna siasa.

  Na huko kwenye siasa (uongo) ndo kula hela. Kisiasa ndo tunaletewa hawa RICHMOND, EPA. Ila kwa kwasababu waTanzania ni wapole, tunanyamaza

  Hii nchi kuna siku damu zitanwagika pindi watu watapochoka siasa
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  unawakubali kwa sababu wanapora wake za watu na kuvunja ndoa kwa sababu ya umaarufu na pesa zao
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  ivi CLUB BILICANASi inaharibu vijana wangapi wanaojiingiza kwenye umalaya na matumizi ya madawa ya kulevya kwa mwaka.
   
 7. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 160
  Chama kizuri na kinapendwa kweli na kinatoa changamoto nzuri na muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa letu

  Agwe bulayi mnya mpwapwa..........ukutiachiii!!!!!!!????????

  1. Dr Slaa sio msomi jamani????
  2. Brother Zitto na dada Mdee, T.A. Lissu hawa sio wasomi hawa????
  3. Mkuu Mbowe sio mfanyabiashara jamani???
  4. Mzee Ndessa naye niaje blayi????

  1. Yaweza sababisha matusi mengi hii majibu yangu but come what may........Blayi wa Mpwapwa; premises ulizoanza nazo haziwezi kukufikisha kwenye conclusion tarajiwa.......tabia hii ya kuwa na weak arguments kwenye mada nzito inatufelisha sana baadhi ya Watanzania na inafanya sometimes tuonekane kama hatujui tunalolitaka ila tunaendeshwa na mihemko ya mwili na hisia (Mapenzi zaid kuliko fikra pevu)

  2. So utafiti wako ndo umekufikisha kwenye kuleta mada kama hii hapa?????? Yaani unaamini A na a ni tofauti by essence????? Kweli bora kile chuo kijengwe na makada (mka-)wakasome huko maana kama hii ndo thinking capacity kazi bado ni kubwa sana.

  Agwe bulayi na wana wako mkuhulika?????
  Wose wahano kulikukaya kwako (CDM) sikuwaonaaaa?????  Walamsaje kukaya................mkonongo wa chilume nilibaha
   
 8. JOHN MADIBA

  JOHN MADIBA JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ccm imepitwa na waatiiii kimejeukakuwa chama cha mauaji kolimba, sokoine, nyerere bado dr makyembe hawajammalizia
   
 9. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,834
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Inaelekea wewe bado uko gizani, tena giza nene kabisa, giza totolo, wewe ni wa huku kabisa ambae CCM wakiweka fisi na CHADEMA waweke mtu utachagua fisi. Mimi nataka niwaamushe wewe sasa tena unataka kuwarudisha gizani, ndekaje leche nkomaza.
  Wewe unafurahiya uozo wa hao? Amka usilale kama na wewe unalala basi hao magamba wataendelea kulima juu mgongo wako.
   
 10. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 160

  Eeeeeenh haya.......authenticating...........caliber mismatch.............disconnecting
   
 11. O

  Olele kibaoni Member

  #11
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 17, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We c wakukameruni au unazan a2jui.
   
Loading...