Kwanini CDM haiendi ICC ?.

Kwanini CDM haiendi ICC ?.

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
21,504
Reaction score
38,367
Kwanini CDM mpaka sasa haijawalisha ushahidi wa tukio la utupaji wa bomu uwanja wa Soweto Arusha katika mahakama ya ICC.

Tuliambiwa hapa jamvini kwamba CDM inao mkanda wa tukio la urushwaji wa bomu katika mkutano wake wa kuhitimisha kampeni za udiwani katika uwanja wa Soweto Jijini Arusha.Mpaka sasa umeshapita muda mrefu CDM imeshindwa kuwasilisha mkanda / ushahidi mahakamani.

Naweza kukubalina na CDM kwamba mahakama zetu,ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka na jeshi la polisi kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikiendesha upelelezi,mashtaka na hata hukumu katika namna inayotia shaka kubwa.Kwakuwa jeshi la polisi ni watuhumiwa na kwakuwa serekali kupitia Rais wa JMT amekataa kuunda tume ya kimahakama kuchunguza suala zima la urushaji wa bomu katika mkutano wa kisiasa nilitegemea CDM kupitia wanasheria wake mahiri wangefikiria kupeleka mashtaka katika mahakama ya kimataifa kwasababu ya kukosa imani na vyombo vya dola.

Nilitegemea CDM wangeijuza jumuiya ya kimataifa kupitia balozi mbali mbali na ofisi ya UN na mashirika yote juu ya uovu unaofanywa na vyombo vya dola (POLISI) lakini mpaka sasa sioni hilo likifanyika badala yake muda unazidi kwenda huku malumbano yasiyo na tija yakichukua nafasi.

Niwazi CDM inapoteza tena nafasi nyingine adimu ambayo kama ingetumika vizuri pengine ingekomesha mauaji ya raia pasipo sababu za msingi.
 
Nadhani cdm inachambua ni namna gani ya kuwasilisha ushahidi,uliodaiwa kuwa upo. Maskio ya watanzania yanataka kujua.
 
Mkuu Apolonary unajua unapochelewesha jambo muhimi kama hili kwa kutumia visingizio dhaifu unakaribisha shaka shaka juu ya madai yao hata kama yana ukweli ndani yake.
 
Last edited by a moderator:
Wachambuzi wa masuala ya siasa wana sema uchaguzi wa Kenya uliomwingiza madarakani Uhuru Kenyatta ungekuwa na umwagaji mkubwa wa damu kama si kitisho cha ICC.CDM ingeanza kufikiria kupeleka mashtaka ICC mapema sio kusubiri mauaji wa watu wengi wangeanza sasa.
 
Mkuu Apolonary unajua unapochelewesha jambo muhimi kama hili kwa kutumia visingizio dhaifu unakaribisha shaka shaka juu ya madai yao hata kama yana ukweli ndani yake.
ICC hiwezi kuchukua kesi kama hii.
ICC prosecutions zake zina base kwenye gravity of the crime .... yaani kundi kubwa la binadamu likfanyiwa unyama uliokithiri na kundi lingine, baada ya kuhamasishwa na watu fulani.
 
CDM ikienda ICC -basi ccm they deserve jahanam

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mkuu Kobello kwahiyo mpake watu 100 wauwawe.Mimi nilikuwa nafikiri kama kuna ushahidi wa usio na shaka na ubabaishaji wa ofisi za mwendesha mashtaka unadhihirisha kuficha jambo fulani ICC ipewe nafasi.

ICC hiwezi kuchukua kesi kama hii.
ICC prosecutions zake zina base kwenye gravity of the case .... yaani kundi kubwa la binadamu likfanyiwa unyama uliokithiri na kundi lingine, baada ya kuhamasishwa na watu fulani.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kobello kwahiyo mpake watu 100 wauwawe.Mimi nilikuwa nafikiri kama kuna ushahidi wa usio na shaka na ubabaishaji wa ofisi za mwendesha mashtaka unadhihirisha kuficha jambo fulani ICC ipewe nafasi.
Nadhani wanaanza na maelfu.
Kuhusu kuwa na ushahidi ambao unaminywa na prosecutors, hiyo inakuwa haiwahusu.
Naona watu wengi humu, hata wanasheria wa bongo wanaongelea ICC bila kujua admissibility yake ina base kwenye nini.
 
Back
Top Bottom