4 7mbatizaji
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 11,496
- 13,326
Propaganda zao mfu zilishakwama, hawana jipya, CCM sio level ya Chadema tena ,wanalazimisha yaende lakini wapi,Pamoja na kuwa ukweli ni mchungu ni lazima usemwe.
Ukweli huogofya na ndiyo maana wale wanaosubiri matunda bila ya kutaka kuwa sehemu ya kuyatafuta, hao ruksa kuingia mitini na hata kutoa povu kabisa.
Ukweli ni mchungu ndiyo maana walio waoga na wasio tayari kuzilipa gharama chungu za ukombozi, ni sahihi kuwahimiza kwa bidii kabisa, kukaa pembeni kwani kwa hakika hata mawazo yao hayahitajiki.
Ni heri kuwa na watu wachache waliodhamiria, kuliko kuwa na watu wengi mizigo.
Tafakari za kina za tulikotoka, tulipo na tunakokwenda haziwezi kuepukwa katika kufikia malengo ya wazi yaliyopo.
Kuna hili la kuitwa SACCOS. Hili si la kufumbia macho. Kuona kukosolewa kwake kwa marefu na mapana yake kunaweza kutuvusha.
Chama kinachopigania katiba ya wananchi kama agenda yake kuu ya sasa, hakiwezi kuwa baridi namna hii tangia Mbowe kushikiliwa.
Chama kinachopigania haki, uhuru na usawa hakiwezi kuwa baina ya vyama ambavyo havijatoa kauli yoyote hadharani ya mshikamano na askofu Mwingira.
Chama kinachopigania haki, uhuru, usawa na demokrasia hakiwezi kuwa hakijatoa kauli yoyote rasmi na hadharani ya mshikamano na mzee wa upako, askofu Shoo na hata Polepole.
Mbowe akiwa kizuizini na Lissu akiwa nje ya nchi ni wazi sasa kuwa kwa mustakabala wa harakati kuendelea, chama kinabidi kujitathmini kwa kina.
Siasa za ukombozi zina tija zaidi "on the ground" kuliko mitandaoni.
Wako wapi kina Heche, Kigaila, na kina Lwaitama?
Wako wapi kina Mdude?
Ziko wapi busara za kina Bagonza, Ulimwengu, Niwemugizi, Ponda, Mwamakula na wenzao?
Ifahamike, ukombozi hauwezi kuwa wito kwa kila mtu. Yaani hata J4?
__________
Uanaharakati ndiyo njia pekee ya kuipata katiba ya wananchi
Watanzania tu wasahaulifu sana. Tumeshasahau yaliyotokea kwenye rasimu ya Warioba? Nani ataipitisha hiyo katiba mpya? Unadhani wanao faidika na katiba ya sasa ambao ndiyo watoa maamuzi watakubali kupitisha katiba itakayo wanyang'anya keki mdomoni? Thubutuuu! La sivyo, walete rasimu ya Warioba, yenye matakwa ya watanzania kama ilivyokuwa, bila kuchakachuliwa, tuipigie kura mahali pa wazi na kura zihesabiwe papo kwa papo mbele ya wapiga kura. Kinyume chake itakuwa usanii mtu.
Tunaongelea Mbowe kwa sababu mada inahudu chadema.
Na hao wengine wakija na mada zao tutawaambia hivyohivyo.
Demokrasia inatakiwa ianzie nyumbani.
Ndiyo maana tunasema hiyo ni saccoss na kwa style hiyo Kukamata nchi mtaendelea kukusikilizia kwenye bomba.Mbowe katangaza kung'atuka 2023 hata hivo CDM wakiamua kwa ridhaa yao kumpa mi5 mingine hilo ni jambo la ndani lisilomhusu mtu yeyote baki.
Au nasema uongo ndugu yangu?
Hapo sasa mnataka kuingilia mambo ya ndani ya chama kingine.Ndiyo maana tunasema hiyo ni saccoss na kwa style hiyo Kukamata nchi mtaendelea kukusikilizia kwenye bomba.
Wacha CCM waendelee kukamata nchi.
Tunaheshimu ila wananchi hatupo tayari kukombolewa na chama cha kidikteta kisicho na demokrasiaHapo sasa mnataka kuingilia mambo ya ndani ya chama kingine.
Kwani uliwahi kuwasikia CDM wakipiga kelele mlipokuwa mkisema atake au asitake mtamwongezea muda zaidi kukamilisha miradi aliy okuwa akiijenga kwa pesa za ndani?
Ustaarabu ni kuheshimu mambo ya ndani ya wengine.
Tunaheshimu ila wananchi hatupo tayari kukombolewa na chama cha kidikteta kisicho na demokrasia
Tunakiona kwa mtu mmoja kushikilia uenyekiti miaka nenda miaka rudiChama kisicho kuwa na demokrasia unakiona vipi kutokea nje?
Si walisema pilipili usizozila zikuwashe namna gani?
Tunakiona kwa mtu mmoja kushikilia uenyekiti miaka nenda miaka rudi
Ziniwashe kwanini!?
Natoa maoni yangu na kuwaambia ukweli kwamba kwa mfumo wenu tu mlionao sahauni kupata nchi.
Na haiwezi kupatikana kama hamko organized.Ngoja tudai katiba mpya kwanza. Bila shaka hata wewe unahitaji katiba bora kwako na hata kwa watoto wa wajukuu zako.
Hata sioni kama umejibu hoja yangu, naona umezua jambo ambalo halina uhusiano wowote na nilichoandika.Kwahiyo mazingira ya siasa ndiyo yaliyosababisha huko CDM kuwe na mwenyekiti mmoja miaka nenda miaka rudi?
4. Kuuza kadi za chama wakati huu chama hakina ruzuku hilo wazo nakubaliana nalo, ni sehemu ya kuongeza kipato kwa chama.1- Mtei kumrithisha Mbowe, mkwewe uenyekiti mpaka leo.
2- Kila mbunge kulazimishwa kuchangia chama lakini hana haki ya kujua matumizi ya Ruzuku.
3- Mbowe kuendelea kujichotea pesa za Ruzuku kila siku, kwa kisingizio kuwa alikopesha chama wakati wa kampeni. Ila hilo deni halijawahi kuisha.
4- Sasa hivi wametengeneza na kuuza kadi za chama kwa mfumo wa HISA kama SACCOS.
5- Linapokuja suala la pesa Mbowe humwambii kitu, ndio maana chama hakuna msimamo wowote isipokuwa ule ulio sambamba na masilahi ya madaraja na kimapato.
We mwanamke unaakili sana ndio maana napendekeza ukagombee cheo cha Malafyale uwe Rais wa Liverpool halisi ππAkina mdude ni wanachadema,wajumbe au mashabiki?
Binafsi huwa nakiona chama cha hovyo na cha kihuni kutokana na watu waliopo humo.
SawasawaHata sioni kama umejibu hoja yangu, naona umezua jambo ambalo halina uhusiano wowote na nilichoandika.
Mbowe yupo kama m/kiti wa CDM kwa kuchaguliwa na wanachama kihalali, kama wewe hutaki ukidhani ndio ujanja sikushangai ndio uelewa wako ulipoishia.
πππWe mwanamke unaakili sana ndio maana napendekeza ukagombee cheo cha Malafyale uwe Rais wa Liverpool halisi ππ
Nimepata taarifa alipitiwa na kimbuga jobo
Hapana sina nia hiyo nimependa vile unapenyeza busara zako kwa vijana wa ufipa maana hawa vichwa zao zimejaa matusi.πππ
Mkuu usiharibu uzi na mambo yetu ya Liverpool tafadhali.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hapana sina nia hiyo nimependa vile unapenyeza busara zako kwa vijana wa ufipa maana hawa vichwa zao zimejaa matusi.
Jitahidi usitumie lugha ya Merseyside maana kops hamchelewi kubadili gia angani