Kwanini CCM Wanakataa "Katiba" - Wanaogopa Yanayotokea Kenya

niweze

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
1,008
116
Wanaofuatilia Uongozi Afrika na Duniani Kote Watakuwa Wamesoma Hawa Mawaziri Watatu wa Kenya Walioshitakiwa Kusabibisha Vifo na Uchochezi Inchini Kenya. Tangu Katiba ya Kenya Ifanyiwe Mabadiliko, Tumeona Viongozi Wengi wa Kenya Kushitakiwa na Tuhuma za Rushwa. Kwa Swala la Rushwa, Hili Linawagusa Sana CCM na Katiba Mpya Definitely Itatoa Madaraka kwa Wanasiasa na Kurudisha kwa Mahakama ya Ukweli Sio kwa Chama Chochote Inchini. Wengi Tunaona Kutopatikana Kwa Haki na Adhabu ya Kutoa Mafundisho Inasababisha Kupanuka kwa Mabavu ya Mafisadi. Haya Ndio CCM Wanayoogopa na Yatawakuta Hata Wakiajaribu Kukwepa Katiba Hivi Sasa. Kitu Kingine ni Katiba ya Kenya Imeleta ni Kuipa Nguvu Sana Justice System ya Inchi na Kurudisha Madaraka kwa Wakenya. Tatizo la Tanzania Mpaka Sasa Sio Mkoloni au Wageni Inchini ila ni Hiki Kikundi Kidogo cha CCM. Hawataki Kuondoka Madarakani na Hawataki Hii Katiba Izungumziwe. Hata CCM Wafanye Wanavyotaka, Wananchi Watanzania Watashinda Tu...Ukweli na Haki Siku Zote Vinashinda Hata Ukitumia Vyombo vya Usalama au Viboko, Watanzania Tukitaka Haya Mabadiliko Yatakuja Tu...

"Katiba Mpya Italeta Transparency na Kikubwa Maendeleo Tanzania. Mpaka Leo Duniani Hakuna Inchi Ilioweza Kuendelea Bila Katiba Yenye Nguvu"
 
Back
Top Bottom