Kwanini CCM inafanya haya?

Kwanini CCM inafanya haya?

This is...

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Posts
5,185
Reaction score
5,431
Rejea ya hiki ninachotaka kuweka hapa Ni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Rombo.

Baada ya mikutano ya vyama vya siasa kuruhusiwa tena, CCM na washirika wake wanafanya Mambo ambayo kimsingi hayakubaliki.

Nikiwa Rombo kuna kitu kinaitwa maagizo ya Waziri Mkuu kwenda kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya, na wakuu wa Wilaya kuwaagiza Walimu wakuu wa shule za Msingi na Sekondari kwamba Ni LAZIMA wanafunzi wanapokuwa paredi asubuhi kabla ya kuingia madarasani Mwalimu anasema. ''KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI'' na wanafunzi wanatakiwa kujibu ''KIDUMU CHAMA TAWALA CCM''

Hii Ni amri si ombi! Mkuu wa Wilaya ya Rombo amekuwa akitembelea shule au kuwapigia Walimu Wakuu simu kuhakikisha Hilo linafanyika.

Na juzi Jumapili tarehe 15.1.2023 kulikuwa na kikao Cha Walimu wakuu wote wa shule za mkoa wa Kilimanjaro pamoja na Waratibu elimu Kata wote, pamoja na viongozi wa CCM , kikao kilichoitishwa na mkuu wa mkoa kuweka MIKAKATI ya kuzidi kufanikisha hilo.

NILICHOBAINI:CCM wanajua kizazi hiki siyo kizazi cha ndio Mzee. Na takwimu zinaonyesha kundi la watu wa umri wa miaka 55 Hadi 70+ kundi ambalo kimsingi Ni wapiga kura wa CCM linaisha. Wamepunguza Sana.

Kundi kubwa Sasa hivi , zaidi ya asilimia 60+ Ni vijana wa umri Kati ya miaka 18 Hadi 45 ambao Ni kundi hatari kwa uhai wa CCM. Hiki Ni kizazi cha kuhoji!

CCM imeona waingize sumu kuanzia kwa watoto wadogo wa shule za msingi ili kujiimarisha huko mbeleni.

Mimi binafsi sijaelewa km Hili linafanyika nchi nzima.

Nini maoni yako!
 
Back
Top Bottom