Kwanini CCM hawataki mfumo wa serikali 3?

Kwanini CCM hawataki mfumo wa serikali 3?

Magembejr

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2014
Posts
618
Reaction score
76
wana jamvi naomba hoja za msingi na zenye takwimu na si za kishabiki kwanini ccm wao hawataki mfumo wa serikali 3? maana nasikia maneno maneno yasiyo ya kitafiti juu ya uwepo wa serikali 2 wanazo taka ccm,so mwenye ufafanuzi huo aweke humu tupate kujua ukweli wao
 
Maccm hawana majibu ya kisayansi zaidi ya porojo tu watakazokuja nazo ili kuendelea kujinufaisha wao na watoto wao!!
 
Mimi nafkiri sababu ni za kisiasa zaidi, kuliko uhalisia wenyewe. Tatizo ni kwamba CCM hawataki tu kuwa wa kweli kuna kitu wanakiogopa iwapo serikali tatu itapita. Hoja alizotoa Jaji Warioba kiukweli ni za msingi zaidi kuliko za CCM. Na sio mara ya kwanza kutolewa pendekezo la serikali tatu. Tume kama mbili au tatu zilizowahi kuundwa tangu kipindi cha Mwinyi na hata Mkapa nazo zilipendekeza serikali tatu lakini majibu yake yaliwekwa kapuni. Ninachokiona wanafanya tu porojo na kudanganya watu. Na kitu ambacho binafsi nimekiona kama kutakuwa na serikali tatu kutakuwa na ugumu sana wa wao kushinda pande zote tatu Muungano, Tanganyika na Zanzibar kutokana na ukweli kuwa kwa sasa upinzani unazidi kuimalika zaidi. Kama Zanzibar kule CUF ina nguvu sana na huwa inawatesa. Kwa hyo, kwa maoni yangu serikali 2 zinawanufaisha zaidi CCM kuliko serikali tatu. Si hilo tu, ni mambo mengi tu mazuri Tume ilishayapendekeza wao wanayakataa mfano, maswala ya tunu za taifa na miiko na maadili ya uongozi. Wao wanadai yatungiwe tu sheria.

Mwisho, lazima Watanzania wajue kuwa CCM kimsingi hawakutaka na bado hawahitaji katiba mpya kwani katiba ilyopo sasa inawanufaisha zaidi kisiasa kuliko hiyo rasmu mpya iliyopendekezwa na Tume. Na mtaona tu watakavyopinga!
 
Kwa sababu wanataka tu kuvuruga mchakato wa katiba. Wanataka uchaguzi mkuu ujao katiba hii mbovu iendelee kutumika...
 
Hawana jipya magamba na mwaka huu wata lia maana wanalazimisha kura ya bunge la katiba iwe ya mmoja mmoja kuhojiwa au kuhoji bunge zima ili kuwa bana wabunge wake wanao taka kupigia serikali 3 kura ya siri
 
Ttzo kubwa hawataki tu kuiona zanzibr ina mamlaka kamili,hofu yao kubwa kanisa halitoweza tena kutawala zanzibr,si mumemsikia pengo alivyosema?
 
Mimi nadhani ni hofu ya kisiasa kuwa ccm ndiyo itakuwa mwisho. Mathalani hata sasa ukifuatilia vizuri ccm inawaendesha wananchi waliyoko mwambao wa bahari ya hindi na zanzibar kiujumla. Hivyo ni dhahiri zanziba wakijitenga kule hali kadharika Tanganyika,hili litawaletea ccm wakati mgumu.

Lakini zaidi ya yote Zanzibar ni mzigo kwa Tanganyika kama ilivyo mizigo mawaziri na rais wa JMT,maana hakuna Tanganyika inachonufaika toka Zanzibar ila Zanzibar ndiyo KUPE kwa Tanganyika.
 
Ttzo kubwa hawataki tu kuiona zanzibr ina mamlaka kamili,hofu yao kubwa kanisa halitoweza tena kutawala zanzibr,si mumemsikia pengo alivyosema?
Exactly Mkuu umegusa point ya muhimu. Kikubwa ni kuwa Pengo amekataa serikali3 na ccm hawawezi kwenda kinyume, wakienda kinyume inamaana wakose kura 2015 pia kushinda serikali3 ni ngumu hivyo wanakomaa ili waendelee kuwepo madarakani. Lakini hoja kubwa ya kukomalia muungano ni kanisa kudhibiti Uislam na wala hakuna ingine.
 
MSALANI, naamini unajipambanua kama mwana CCM; je wewe binafsi unapendelea mfumo wa serikali mbili? Kwa sababu zipi?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kwa nini wewe hujatuambia kwa nini idadi ya serikali unazokomaa nazo unazitaka za nini na ili iweje.
 
kwa sababu mafanikio yao yanapatikana kwa kuibeba zanzibar, ukitaka kujua angalia bunge la muungano lina watu wangapi toka zanjibari, wakati ratio ya population tuwape 2m:45m, uchumi 4%:96% lakini wabunge 30%:70%
 
wana jamvi naomba hoja za msingi na zenye takwimu na si za kishabiki kwanini ccm wao hawataki mfumo wa serikali 3? maana nasikia maneno maneno yasiyo ya kitafiti juu ya uwepo wa serikali 2 wanazo taka ccm,so mwenye ufafanuzi huo aweke humu tupate kujua ukweli wao

Ccm hawataki serikali 3 kwa vile wanaogopa kuwa kukirudishwa serikali ya Tanganyika chama chao kitapasuka, kwani kuna uwezekano mkubwa Zbr wakarejesha chama chao cha ASP kwa mfumo wa katiba yao mpya ambayo haina uhusiano na muungano unaolazimishwa na wahafidhina wa ccm. Serikali 2 haiwezi ku work out unless katiba ya Zbr inakuwa rescinded kitu ambacho Wazanzibari hawawezi kuridhia!!
 
Mimi nadhani ni hofu ya kisiasa kuwa ccm ndiyo itakuwa mwisho. Mathalani hata sasa ukifuatilia vizuri ccm inawaendesha wananchi waliyoko mwambao wa bahari ya hindi na zanzibar kiujumla. Hivyo ni dhahiri zanziba wakijitenga kule hali kadharika Tanganyika,hili litawaletea ccm wakati mgumu.

Lakini zaidi ya yote Zanzibar ni mzigo kwa Tanganyika kama ilivyo mizigo mawaziri na rais wa JMT,maana hakuna Tanganyika inachonufaika toka Zanzibar ila Zanzibar ndiyo KUPE kwa Tanganyika.
hapo ckupingi bro maan ZANZIBAR hawana madini wale rasimali yoyote ya msingi wao labda wana urojo 2
 
Back
Top Bottom