Usemalo ndo ukweli wa wabongo na tatizo limekwenda mbali zaidi hadi kwa kizazi cha sasa.Kama ambavyo watanzania wengi tunasoma kwa ajili ya kupata vyeti na kupata kazi, ndivyo walivyo Maprof na wale waliopata PhDs! Wengi wamefikia level hiyo wakiwinda promotion na kujulikana kwamba wana elimu kubwa na si mahitaji ya ufanisi katika shughuli walizokuwa wakizifanya. Utashangaa mtu kapata digrii yake ya kwanza leo, kesho anasoma digrii ya pili mara ana phd. Kazi hajawahi kufanya hata siku moja, changamoto za kazi hazijui, sasa atabuni kitu gani cha kusaidia jamii wakati hajui mazingira ya kazi yakoje? Atakachofanya ni kuangalia jamii inafanya shughuli gani na yeye ataiboresha kidogo kwa uprof wake na huo ndio ubunifu wake! Angalia baa nzuri au mgahawa mzuri, utaambiwa wa prof fulani au dr fulani! Huo ndio mchango wao na hilo ndilo tatizo la kusoma bila malengo ya kimahitaji!
Tatizo si maprofessor au Ph.Ds. Tatizo ni jamii ambayo haijajipanga vizuri kuwahamasisha watu wake kuwa wabunifu, wagunduzi na kuthamini taaluma. Katika nchi zilizoendelea vyuo vikuu siyo taasisi za kufundisha peke yake bali ni mahali pa kutafiti na kugundua maarifa au teknolojia mpya. Inventions nyingi ambazo baadae zinakuja kuwa na matumizi ya kila siku (innovations) nyingi zinaanzia kwenye tafiti katika vyuo vikuu. Hapa kwetu sivyo ilivyo. Vyuo vikuu ni shule tu. Hata pale ambapo utafiti/ugunduzi unafanyika (kwa mfano pale CoET ya UDSM) matokeo yake huyaoni yakiwekwa katika matumizi ya kupunguza shida/changamoto zinazoikabili jamii. Watafiti wanapata Ph.D zao au wanapata promotion na kuwa maProf. yanabaki hapo kwenye makaratasi. Hata kuitangazia jamii ili iweze kujua nini wanafanya ili wajasiriamali watumie hayo maarifa mapya haifanyiki. Kwa nini? Labda ni kwa sababu biashara za baa, n.k. zina returns nzuri na mapema zaidi kuliko hizo za kitaaluma na kitafiti. Kama kuna maprofesa na wasomi wengine hapa JF watupe upande wao wa sarafu.Hao maprofs na phd holders wanaona kama wamemaliza kila kitu so uwajibikaji unakua wa kujisikia but si ujanja watumie elimu yao kuvumbua mipangilio kimaisha.akina Newton,Socrates au Bill Gates c maprofs ona michango yao
Wengi kama c wote ni wabangaizaji wa life shida yao sana2 wana-aspire kumiliki nyumba, gari totoz na uhakika wa ulabu. Nenda mitaa ya Survey, Kambarage kwa SUA na Changarawe utathibitisha ninayosema.