Kwanini Boko Haram na makundi mengine hayakamatiki?

Kwanini Boko Haram na makundi mengine hayakamatiki?

Paul S.S

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2009
Posts
6,408
Reaction score
3,269
Wakuu najiuliza sana hivi inawezekana vipi kikundi kama Boko Haram hakiwezekaniki kuthibitiwa na kipo ndani ya Nigeria?
Kama tuliweza kumfyagia Idi amini mwanzo mwisho kwanini wanaigeria wasiingize jeshi kipande ile hatua kwa hatua hadi mpakani?
Hebu nifafanulieni ugumu wake ni nini haswa?
 
Ni swali zuri sana sana umeuliza. Hata mimi nilikuwa nafikiria nchi kama Nigeria yenye jeshi kubwa inakuwaje inasumbuliwa na kikundi ''kidogo'' kama hiki. Mimi nadhani hili kundi lina support kubwa ya wananchi, viongozi na vyombo vya ulinzi ambavyo kwa namna moja hawapendi utawala wa rais wa Nigeria
 
Ni kama Ansar Beit al Maqdis au Hezbollah
 
Wakuu najiuliza sana hivi inawezekana vipi kikundi kama Boko Haram hakiwezekaniki kuthibitiwa na kipo ndani ya Nigeria?
Kama tuliweza kumfyagia Idi amini mwanzo mwisho kwanini wanaigeria wasiingize jeshi kipande ile hatua kwa hatua hadi mpakani?
Hebu nifafanulieni ugumu wake ni nini haswa?

Unashangaa serikali ya nigeria kuwashindwa CIA?
 
Wakuu najiuliza sana hivi inawezekana vipi kikundi kama Boko Haram hakiwezekaniki kuthibitiwa na kipo ndani ya Nigeria?
Kama tuliweza kumfyagia Idi amini mwanzo mwisho kwanini wanaigeria wasiingize jeshi kipande ile hatua kwa hatua hadi mpakani?
Hebu nifafanulieni ugumu wake ni nini haswa?

Kuna habari kwamba Boko Haram inadhibitika ila ni a "manufactured crisis" kwa sababu za kisiasa na wakubwa wa Nigeria wenyewe wanahusika.
 
Government is the real gangster, grow up bwana mdogo. Uliwahi kuisikia AL QAEDA kabla ya 9/11? hujaona ISIS ilivyukuwa kama uyoga fumba na kufumbua
 
Ikishakuwa kundi la kidini ni ngumu sana kulimaliza kama nchi imegawanyika katika dini kuu
 
Ila pia Magaidi wana technique kali sana, pesa,elimu ya shule , support, na wanaishi kwa makundi makundi sana...
 
Ila pia Magaidi wana technique kali sana, pesa,elimu ya shule , support, na wanaishi kwa makundi makundi sana...

Mbona wanasema Waislam hawapendi shule, hawataki kabisa kusoma na hata hao Boko haram hawataki watoto wakasome shule...

Au huwa wanadanganya
 
Government is the real gangster, grow up bwana mdogo. Uliwahi kuisikia AL QAEDA kabla ya 9/11? hujaona ISIS ilivyukuwa kama uyoga fumba na kufumbua

Haujamsaidia kitu zaidi ya kufumba zaidi, mweleze ata kwa kifupi ni kwanini hawakamatika.
We umemuongezea makundi mengine IS an AL QAEDA.
 
Mbona wanasema Waislam hawapendi shule, hawataki kabisa kusoma na hata hao Boko haram hawataki watoto wakasome shule...

Au huwa wanadanganya

Halafu wanatumia elimu hiyo hiyo kutishia watu, kuua, na pengine kuendesha maisha yao kiujumla. Hapa kweli tunapigwa changa la macho.
 
wameshapenya hata kwenye system. usalama, jeshi nk, hivyo wakipang mkakati, majamaa yanawatonya
 
hao noma kaka NAWAPENDA SANA haswa jina lao BOKO HARAM eti THE WESTERN EDUCATION IS SINFUL-ELIMU YA MAGHARIBI NI HARAMU/DHAMBI.much respect BOKO HARAMU THE WINNERS.
 
Ugaidi ni "ideology" na ideology yoyote inaweza kuzimwa/kupigwa vita kwa kutumia another stronger ideology. Sasa wao wanapambana na ugaidi kwa mitutu na makombora HAWATOWEZA KAMWE maana ukimuuwa gaidi m1 unawapa morale vijana wengne 100 kuwa magaidi, nani asiyependa kwenda kupasua bikra 72 per day?. So long as watu wataendelea kuamini kuwa gaidi ni kumtumikia Mungu ugaidi hautokwisha hata muwafanyie vitimbi gani.
 
Swali zuri sana uloliuliza,nami ningependa kuchangia machache tu ya kwanini BOKO HARAMU (walolaaniwa) hawadhibitiwi na serikali ya Nigeria.
KWANZA KABISA inatubidi tujiulize,kwa kuwa silaha siyo biasha ya mahindi au nguo ambayo unaweza kuitoa sehemu moja au taifa moja na kwenda kuuza katika taifa lingine,je silaha wanazotumia zinatoka wapi na kama kuna anaewadhamini hawa jamaa,je wauzaji (mataifa makubwa) kwanini yaridhie silaha zao kutumika kiholela kama sio wao wanaodhamini ugaidi ili soko lao likue ?
Nafikiri jibu kamili lipo kwa kinara wa upambanaji wa ugaidi wa ugaidi ambae tayari aliahidi na kuitangazia dunia kuwa atawapa mafunzo waasi wa ******* ambapo muda mfupi baadae tukasikia "I S" wameibuka na leo kuwa tatizo kwa wanadamu lakini kwa kuwa ni mpango wa shetani kuitawala dunia,basi wasona macho yashatekwa akili.
Siyo ajabu boko haramu kuendelea kuisumbua Nigeria kwa sababu mawakala wao wanafaidika na wanazidi kuinyonya Nigeri halafu wanapandikizwa mbegu ya dini ili wasijue kinachoendelea.
HUO NI UKOLONI WA KISASA.
Boko haramu hawafanyi kazi kwa kutokujua na ndio maana hata viongozi wa Nigeria wanashindwa kuwaangamiza maana masilahi yapo,hivi ni kweli waweza kumdhibiti anaekupa misaada ?
Niliwahi kuandika kuhusu unyama unaofanywa na hawa jamaa na makala yangu ilikuwa na kichwa cha habari "UKAFIRI WA BOKO HARAMU KATIKA VAZI LA UISLAMU" lakini ajabu uzi huo hauonekani na umefungwa,labda ni sheri pale unapouweka ukweli halisi mambo yanafungwa kama hivyo,lakini yule yule mmoja aloona ujumbe huo atakuwa ameelewa na kama anataka dunia yake kuwa sawa basi atauchambua uwongo unaofanywa na hawa mashetani (Boko Haram).
Turudi nyuma kidogo na kumkumbuka yule kibaraka,mkandarasi wa barabara na majengo ambae baba alikuwa rafiki mkubwa wa taifa lenye raisi mweusi mwenye roho ya kizungu ambae hata ajali asili ya baba yake.
Mkandarasi huyo aliweza kuisumbua dunia na maelfu ya watu kuangamizwa rasilimali kuibiwa na mataifa kupinduliwa,hapo lengo lilianza kutimia.
Lakini mwisho wa siku ndipo walipozaliwa boko haramu kwa ajili ya kuendeleza kazi hiyooo,wizi wa rasilimali.
Siku tukijahamka,tutakuta tumewekea panga shingoni na hapo ndo mwisho wa Afrika.
 
Ukabila na Udini nigeria ndo imeileta Boko Haram
 
Back
Top Bottom