Kwanini Bima ya Afya hawatibu Wanachama Siku za Mapumziko?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Ndugu zangu wana JF Mimi ni Mwanachama wa Bima ya Afya nakerwa sana na kutopata matibabu siku za mapumziko kama Jumamosi,Jumapili na siku za Sikukuu.Siku hizo tunaugua kama kawaida na ajali pia hutupata kwani hatuombia bali hutokea bila sisi kutaka,sasa kwanini Bima ya Afya haiweki utaratibu wa matibabu siku hizo?Vituo vingi vya Afya kwa siku hizo hudai watu wa Bima ya Afya hawapo hivyo hulazimika kujilipia matibabu hapohapo au sehemu nyingine.Hii ni Haki?Naomba mchango kwa yeyote.
 
Ni vema Bima ya Afya wafanye utaratibu wa kutoa matibabu kwa siku zote za wiki ili wanachama wapate huduma ipasavyo.
 
Jamani Bima ya Afya mfike hata Vijijini kwani wanachama wenu tukisafiri tunapata shida ya matibabu.Pia suala la udanganyifu katika Bima ya Afya linatokana na mlolongo wa taratibu uliowekwa hati mwanachama atibiwe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom