Unaposema kwamba Lowassa alitubu ujumbe unaotoa ni kwamba kweli Lowassa alifanya makosa anayotuhumiwa kwa namna moja au nyingine. Unapotaka kuingiza suala la ubinadami na kudai eti Lowassa nae ni mwanadamu kama mwanadamu mwingine unatakiwa kwanza kufahamu ikiwa makosa anayotuhumiwa nayo ni makosa yanayotokana na upungufu wa kibinadamu au vinginevyo. Ikiwa kweli Lowassa alitubu kutokana na makosa ya ufisadi ambayo amekuwa akituhumiwa; ufisadi si moja ya makosa yanayotokana na mapungufu ya kibinadamu. Wewe huwezi kuwa muuaji halafu ukataka usamehewe kwa kuwa nawe ni mwanadamu kama mwanadamu mwingine wakati uuaji hautokani na mapungufu ya kibinadamu hususani kama uuaji wako haukusababishwa na mapungufu ya kibinadamu kama vile hasira ulipomkuta dume juu ya kifua cha mke wako na ukashindwa kuji-control na kufanya mauaji! Hasira ni makosa ya kibinadamu kwa maana hata kwenye elimu ya viumbe, tunaambiwa mwanadamu ana hormone zinazoitwa adrenaline hormones na hizi hormones zinapokuwa secreted/produces, automatically mwanadamu atajikuta anapandwa hasira! So, the more your body produces these hormones the more you become less control na hasira! You've no control on your hormones na ndio maana kosa litakalotokea hapo litahesabiwa ni la kibinadamu though it's not an excuse either!Hivi baadhi ya watanzania ni kwamba wanamchukia tu Mh. Lowasa kwa sababu zao au wanaogopa utendandaji kazi wake?
Mh Lowasa ni mtanzania na binaadamu kama mtu mwingine yeyote yule ambaye ni mtanzania na binaadamu, watanzania wamekuwa wakimuhukumu huyu mzee na kujisahahu kama wao pia ni binaadamu na wanakosea, na kwakufanya hivyo watanzania hao, wamechukua nafasi ya Mungu, na kujiona wao ndio wanaweza kuhukumu na sio Mungu, kama nikikumbuka vizuri Lowasa alishatubu tena na akaenda mbele zaidi kwa kuchukua maamuzi magumu na kuamua kujiuzuru wadhifa wake wa uwaziri mkuu.
Na Mungu alishatuambia hata kama dhambi zenu zilikuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa nyeupe kama sufi, kwa maana hiyo Yeye ndiye anaye samehe na Yeye ndiye anaye hukumu, na msamaha wa Mungu unatatokana na pale tu, mtu anapotubu, na tukishatubu huwa tunaamini ya kwamba tumesamehewa, kwahiyo Mh Lowasa alishatubu na akaamini ya kwamba amesamehewa, sasa ni kwanini baadhi ya watanzania wanahukumu kitu ambacho kilishafanyiwa toba?
Watanzania wengi huwa hawajiamini, na kutokujiamini huwa inaleta woga, na woga ukikoma huleta chuki na wivu, tusipokuwa makini chuki na wivu ambao upo kwenye jamii leo hii, zitatuingiza kwenye migogoro isiyofaa, watanzania tubadilike, tuombee nchi yetu na tuombee viongozi wote pasipo kubagua, na mengine tumwachie Mungu.
Mawazo yako saafi, kama ni kutokuwa na sifa za uongozi tuanze na yule mkulima toka kigoma maana hajawahi kuwa kiongozi.Wanaomtuhumu Lowasa kisa kachukua form ni vilaza tu na hata wachangiaji wengi wa JF wanaosapoti hilo ni vilaza tu coz kuna watia nia 40 ndani ya ccm na kati yao atapitishwa mmoja na wenye mamlaka ya kupitisha wagombea 5 ni cc yenye wajumbe 28 tu hivyo ni ujinga kuanza kumshambulia mtu mmoja as if ni yy tu asiefaa kati ya wagombea wote 40 kitu ambacho sio kweli.
Suala la kugawa pesa ni la kawaida kbs kwa uchaguzi hasa ndani ya ccm miaka yote ndio maana hata wabunge wa ccm ni wale wenye pesa tu ndo wanashindaga kwenye kura za maoni hivyhivyo kwa rais pia hilo loko wazi.
Kwa hiyo sioni busara kumshambulia Lowasa kisa alishawishi serikali iingie mkataba na richmond ambayo haikuwa na usajiri nchini marekani. Hilo ni kosa la kiuongozi ambalo linafanywa na viongozi kibao wa serikalini na wengine wapo bado serikalini na wengine wanatangaza nia lkn hakuna anaewaongolea kila mtu ni lowasa acheni cc ifanye kazi yake kelele za watu wa IQ ndogo km watangaza nia wanaoacha kuuza sera zao na kuanza kushambulia mtu haziwezi kubadili chochote kwenye cc ya ccm