Kwanini asemwe yeye tu kati ya wengi wengine?

Kwanini asemwe yeye tu kati ya wengi wengine?

Achanakia

Member
Joined
Jan 28, 2021
Posts
69
Reaction score
81
Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wafuasi wa Shujaa wetu juu ya kitendo cha baadhi ya Watanzania wenzetu kumsema shujaa wetu kwa mabaya.

Malalamiko haya si mitaani na kwenye mitandao ya kijamii tu bali mpaka kwa baadhi ya viongozi wa serikali na bungeni.

Walalamikaji wanadai wanaoneza ubaya wa shujaa wanasujumwa zaidi na husda,wivu na fitina kutokana na maendeleo makubwa aliyoyafanya shujaa kwenye nchi yetu, hivyo wanaoeneza ubaya wanajaribu tu kuharibu image na legacy ya shujaa.

Wanadai kama wakosoaji wa utawala washujaa wangekuwa na hoja basi wangeanza kwanza kuanika maovu ya akina Mkapa na Nyerere maana nao walikuwa marais. Lakini kama shida ni kwamba akina mkapa tangu wamefariki ni muda kidogo umepita, Maalim Seifu amefariki mwezi mmoja kabla ya Shujaa wetu, naye alikuwa ni kiongozi vile vile Makamu wa kwanza wa rais lakini yeye mbona mabaya yake hayasemwi?

Wafuasi wamekuja na hitimisho kwamba Shujaa hakuwa mti wa mwarobaini alikuwa mti wa matunda ndiyo maana anapigwa sana mawe.

Lakini wakosoaji nao wanasema kumfananisha shujaa na Maalim ni makosa maana Maalim hakufanya mambo yoyote mabaya ya kuumiza jamii.

Wanahitimisha kwa kusema mtu hatumii nguvu kubwa kumuondoa jongoo akiingia ndani anachukua kijiti na kumrusha jongoo nje hajihangaishi kumuua maana madhara kivile tofauti na Nyoka ambaye hupondwa kichwa.

Kwa maneno mengine wana maana Maalimu alikuwa kama jongoo kwa jamii maana yake hakuwa na madhara ndiyo maana hasemwi vibaya.
Lakini shujaa ni kama alikuwa cobra.

Je nini maoni yako Mwanajukwaa?
 
Wewe acha tu.

Hata ndugu zake Akwilina wanatakiwa waimbe mazuri ya shujaa.

Familia ya azory gwanda nao wasimlilie ndugu yao, bali wamlilie shujaa mkombozi.
 
Hawa jamaa walikuwa wanamsifia muda wote, baada ya yaliyotokea plus "acquired stupidity" wamejikuta hawana la kuongea, WANAONA BORA wahakikishe kuwa koti halichunguzwi vizuri kama WATU watakavyo.
 
Bora pangekuwepo na upigaji ambao upo wazi i.e hata wananchi wakajua kuwa wanapigwa kuliko kiongozi kuwaaminisha wananchi kuwa unapigana kila siku vita dhidi ya mabeberu kwa manufaa ya wananchi wakati katika uhalisia kiongozi ndio beberu halisi. hakuna cha vita na mabeberu wala nn. Hapo lazima ujadiliwe hata uende dunia ya wap
 
Tunataka mikataba ifuatayo;
1. Mkataba wa manunuzi ya ndege zote

2. Mkataba wa ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere.

3. Mkataba wa ujenzi wa Chato Airport

4. Mkataba wa ujenzi wa reli ya SGR

5. Mkataba wa ujenzi wa Ikulu ya Dodoma.

6. Mkataba wa ujenzi wa Daraja la Busisi

7. Maelezo kuhusu procurement process ya miradi yote hapo juu.

Hii ni baadhi ya miradi ambayo wananchi wanapaswa kufahamu mchakato mzima kuanzia hitaji ni nini? Procurement process mpaka alipopatikana huyo mkandarasi, mkataba na malipo yake yamefikia wapi mpaka sasa.

Huyu mtu alikuwa anaamua tu kama anaenda kununua muwa.
 
Back
Top Bottom