G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,596
- 36,018
Mimi na baadhi ya wana jukwaa na kwa heshima kubwa niwataje baadhi yao kama The Boss Salary Slip VUTA-NKUVUTE na wengine wengi (Pasco haeleweki bado) tumekuwa hatumuungi mkono rais Magufuli na kwa dhati kabisa tunalisimamia hilo kutokana na mambo tusiyokubaliana nayo katika utendaji wake ambayo dhahiri yanaonekana kwa macho!
Kwanza watendaji wa Magufuli takribani wote wamekuwa ni watu wa mkondo mmoja (mkondo wa msimamo mkali) mkondo wa 'zero tolerance' kwenye mambo mengi. Mkondo huu hauwezi kwenda sambamba na dhana ya utawala bora.
Leo hii ili mtendaji wa rais Magufuli ili ajione kuwa kafanya kazi basi ndani ya wiki ni lazima afukuze, ashtukize, atoe matamko makali, atoe onyo kali! Jamani, kwani ni shinikizo?
Mtendaji wa rais Magufuli asipofanya moja kati ya hayo basi anajiona si salama ndani ya serikali! Na kwa dhati kabisa hali hii imehasisiwa na viongozi wakuu wetu!
Kuna wakati nilileta thread humu nikitaadharisha kuwa mwenendo wa rais Magufuli unaweza kuwaathiri sana watendaji wake nikafika mbali na kusema kuwa wataweza kufanya kazi mithili ya 'pressure cooker'
Rai yetu ambao huwa ni kawaida yetu kutoa ushauri; ni budi mambo yatulizwe na watu wafanye kazi na kuleta ubunifu! Watendaji wasioneshe wazi kuwa wapo chini ya shinikizo la kisera! la hasha! Wafanye kazi kwa kutumia akili, juhudi, maarifa na uwezo ili kuleta ubunifu wenye tija!
Juzi baada ya rais kusisitiza mapato tukashuhudia waziri ambaye baadaye alihamishwa wizara aliyekuwa na jukumu la kuleta maji safi na salama kwa umma akigeukia swala la mapato na kuisihi DAWASCO kutumia mita zenye mfumo wa LUKU ili wakusanye mapato! Kweli?
Niipongeze mahakama kuu kitengo cha ardhi kwa kufuata kanuni za utawala bora pia nimuombe mwanasheria mkuu wa NEMC aliangalie swala la bomoa bomoa kwa mapana na mazito!!