Wewe ndio huna akili ndugu, hii mipaka ni ya kufikirika, iondoe kabisa kichwani mwako utatoboa mbaya mbovu, kwani kunawahindi wangapi ni matajiri kuliko wazungu kibao? Dangote kwa mfano, ni muafrika na kaburuza mamilioni ya wazungu kwa ukwasi na wengine wengi wapo dizaini yake…
Usihangaike na mchezo wa wazungu wa kutujumlisha, pambania hali yako na jipime wewe kama wewe, ukianza kutaka kujumlisha na walevi wanaoshinda baa asubuhi mpaka jioni, malaya wahongaji waliokubuhu na wapuuzi wengine kwamba wote mtoke kimasomaso utachelewa sana, wapo wabongo wenzako wanaishi zaidi ya ulaya, na wapo wazungu ulaya safari ya kuja Tanzania tu mfano wanajipanga miaka mitano na zaidi… unadhani kila mzungu anaweza kuwa na lifestyle ya Mengi, Mo, Rostam, Rugemalila, Mbowe, Shirima, Samatta, AY, FA, Kinje, na wengine wengi tu wasio maarufu, tena hiyo ni bongo tu, vp Kenya, Rwanda, Nigeria, Morocco, Egypt, SA aiseeee!!!!.
Hatuko vibaya sana, tunajikongoja, safari bado mbichi hii, time will tell….