Kwani nchi hii haina watu wenye akili?

Kwani nchi hii haina watu wenye akili?

Mkuu! Umeongea vema! Watu unaowataka wenye akili, busara, maarifa na maono juu ya jamii tuliyomo na hatari inayotukabili huko mbeleni kama tutaendelea hivi, tupo! Mmojawapo ni mimi! Ila mfumo umetutema! Utaanzia wapi?
[emoji23][emoji23]
JamiiForums-121456483.jpg
 
Ukiona vyaelea vimeundwa. Ukikuta kuna walakini kwa watu angalia uongozi mzima uko vipi.
Yangu miye haya hapa:

Muda wa mapinduzi vyamani ni sasa

Tunahitaji viongozi bora wa kuwaongoza si bora viongozi.
"Kiongozi mlamba asali, mwoga, mwizi, fisadi au mnafiki amkomboe nani vipi.

Ninakazia "asilaumiwe dobi kaniki ni rangi yake." Bila kusahau "mtoto umleavyo ndivyo alivyo."
Wanatakiwa watu aina ya von Bismarck, frank Roosevelt, Adolf Hitler, Putin, Kim kiduku, wazaliwe Kwa 100,000 ivi Tz....Kwa sasa maoni yangu ni hayo
 
Mkuu sasa tufanyeje kama taifa ?
Tuendelee tu kulalamika huku tukiwa tumejificha kwenye mitandao. Maana hakuna namna. Ukijitokeza tu hadharani, unashughulikiwa faster.

Kiasi cha kuwafanya wasomi wengi waogope kujitoa mhanga. Mtu akiangalia ana watoto wadogo, ana familia inamtegemea! Aisee inatia huruma sana.
 
Tuendelee tu kulalamika huku tukiwa tumejificha kwenye mitandao. Maana hakuna namna. Ukijitokeza tu hadharani, unashughulikiwa faster.

Kiasi cha kuwafanya wasomi wengi waogope kujitoa mhanga. Mtu akiangalia ana watoto wadogo, ana familia inamtegemea! Aisee inatia huruma sana.

Mkuu ninachokisoma hapa kwako ni woga, kusaka na kulinda fursa (opportunism).

Yalitokea JKNIA au hata Kiluvya. Kwani nini kimebadilika hadi woga huu stiff kuwafika waja hawa hawa na kwa kiasi hicho?

Ninakazia:

Upinzani - walio waoga (cowards) si Wafuasi
 
Mkuu ninachokisoma hapa kwako ni woga na kulinda fursa (opportunism).

Yalitokea JKNIA au hata Kiluvya. Kwani nini kimebadilika hadi woga huu stiff kuwafika waja hawa hawa na kwa kiasi hicho?

Ninakazia:

Upinzani - walio waoga (cowards) si Wafuasi
Kiukweli Watanzania wengi hatuna ujasiri wa kuingia barabarani na kukinukisha. Sijui huu uoga ni wa kurithi!! Maana unaambukizwa kizazi na kizazi.

Tuko wengi sana tu! Na huu uoga ndiyo unaowapa jeuri ccm ya kufanya chochote kwa msaada wa karibu kabisa kutoka kwenye lile jeshi lao pendwa. Mimi nimesema tu ukweli.
 
Kiukweli Watanzania wengi hatuna ujasiri wa kuingia barabarani na kukinukisha. Sijui huu uoga ni wa kurithi!! Maana unaambukizwa kizazi na kizazi.

Tuko wengi sana tu! Na huu uoga ndiyo unaowapa jeuri ccm ya kufanya chochote kwa msaada wa karibu kabisa kutoka kwenye lile jeshi lao pendwa. Mimi nimesema tu ukweli.

Sidhani kama uko sahihi sana.

Waliokwenda kumpokea Lissu walikuwa watanzania.

Waliokomaa na Lissu Kiluvya walikuwa watanzania.

Unaweza kutathmini kuna nini cha kufanana au kutofautiana na zama hizo?

Una maana hata kina Erythrocyte nao leo wana mikakati mipya isiyojulikana?
 
Hata akitoa mwenye akili watamzima haraka sanaa maana ataonekana anaharibu ulaji wa watu
Akizimwa ujue wazimaji wamemzidi akili na maarifa.

JFK few hours before his assassination, alitua somewhere in Texas, akakuta full ujumbe umesambazwa na mwingine umebandikwa kila mahali.

Funny enough, ulikuwa umetaja sababu ambazo zingemfanya auawe, he simply brushed them aside like normal rumors until the truth actually caught up with him.

Intelligent? I doubt! At least angebadili hata protoko ya kutumia limousine yake.
 
Watu wenye akili wapo, ila wale wenye akili timamu ndiyo wachache sana...
 
Wakati mkiendelea na zoezi la sensa nawaomba watanzania mje na mjibu swali hili ambalo nimedhani litatuongezea upeo wa kutafakari.

Uchumi umekua kama jinamizi ambalo linaondoa usingizi wa wananchi wengi wakubwa na wadogo. Wakiteswa na njaa, magonjwa, ukosefu wa huduma za jamii za msingi ikiwemo makazi duni na kazi zisizo na staha.

Elimu duni inayopelekea wahitimu kupoteza muda shuleni na gharama kubwa licha ya wakihitimu kumaliza elimu zao pasina kuwa na maarifa na ujuzi wenye manufaa unoweza kutatua changamoto za maisha. Hili pia ni zigo ambalo kama taifa hatuna jawabu.

Mmomonyoko mkubwa wa maadili unaolitafuna taifa. Sio vijana wala wazee wote hakuna wa kumfunga kengele mwenzie. Kiwango kikubwa cha utumiaji wa vilevi na madawa, ndoa kuvunjika, uzinzi na uchangudoa, utoaji mimba na mengine kama hayo yanazidi kuliteketeza taifa.

Uongozi mbovu na ufisadi bado vinazamisha meli yetu ya maendeleo na kama taifa simuoni mwenye akili wakutusaidia kushinda changamoto hizi. Hajui ni sifa zipi kiongozi anapaswa kuwa nazo, viongozi kutamani kutumikiwa na sio kutumika, rushwa Ili kuwa kiongozi na ubadhilifu wa Mali za umma ni matatizo ambayo jamii yetu bado inatapatapa pasina majawabu

Je, hatuna wenye akili katika jamii zetu wakutupa solution za changamoto hizi?

Historia inaweka kumbukumbu ya philosopher waliowahi kuishi na kwa matumizi mazuri ya akili zao walizisaidia jamii zao. Je sisi hatuna watu kama hawa wenye ufahamu na akili nzuri ya kuleta majawabu? Je jamii yetu inawatambua watu wa namna hii, je kuna mifumo ya kuwabaini na kuwawezesha kufanya kazi hii ya kufikiri na kuja na majibu ya kimikakati?

Wako wapi philosopher hawa ambao wataanzisha community schools Ili wawaendeleze follower wao. Usinishawishi kuwa hawa philosopher ni akina Mtume Mwamposa, Mtalemwa, Jo Davie, Mzee wa Upako au askofu Mwingila?

Nauliza tena je jamii zetu hazina watu wenye akili?

Karibuni.
Watapatikana wapi wakati wengi Wao wamefanywa hivi?
20211219_102505.jpg
 
Back
Top Bottom