Kigorohe
Senior Member
- May 21, 2019
- 160
- 255
Habari zenu wana JF! Jamani leo tena kuja kwenu ili kubadirishana mawazo juu ya swala zima la mahusiano. Ni miaka kadhaa sasa nipo kwenye mahusino. Ila kinacho nishangaza ni kuwa sijawahi kudumu na mwanamke au binti zaidi ya miezi 7! Huwa napenda sana nidumu na binti ila ikitokea tukafanya tendo huwa naanza kumpotezea kabisa. Binti wa mwisho nilimpata mwaka jana mwezi 12 nikampenda sana na nikafikilia kumuoa kabisa lakini sijui kilitokea nini nikajikuta namwambia wazi kabisa "kuanzia leo naomba tuachane". Jamani wanaume mliodumu adi kuoana naombeni ushauri. Nikiisha mwacha huwa naumia sana kwa siku zingine ila najikuta tu nimeacha. Karibuni sana