Kwani kakumbuka nn?....

mahirtwahir

JF-Expert Member
Jan 12, 2013
595
500
1. Anazitaka zirudi, ayyamu walayali
Zilizo vunja miadi, na kututenga wawili
Zikatuweka baidi, tukaishi mbali mbali
Vipi leo zitarudi, ziwe tena za awali

2. Nilimpa moyo wangu, ukawa ni nyumba yake
Akaijua mivungu, milango na njia zake
Sina pembe ilo yangu, zote mikononi mwake
Asione ghali langu, pendo liloishi kwake

3. Kachezea ihsasi, zangu huku akijua
Akajifanya hahisi, na roho kunisugua
Akasahau asasi, asili alivyokua
Nilipompa nafasi, ulimwengu kumjua

4. Leo kwikwi na machozi, na miguu kunishika
Analilia mapenzi, raha anazikumbuka
Aloshindwa kuzienzi, machoni zikamtoka
Zikampata mjuzi, hab'bub wakuziweka
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom