Kwani hakuna fursa nje ya Tanzania?

Kwani hakuna fursa nje ya Tanzania?

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2018
Posts
1,403
Reaction score
2,550
Vijana wasomi mnakwama wapi?

Kwani hakuna fursa zingine nje ya nchi hii mpaka muanze kuendesha bodaboda?

Inakuaje mnasoma kwa miaka zaidi ya 16 halafu mnaishia kufanya kazi za waliomaliza darasa la saba?

Naomba Wizara ya Kazi na Ajira itangaze fursa zilizopo nje ya nchi ili vijana waweze kujiachia ngambo kutafuta fursa maana wanavyozidi kukaa nyumbani bila kazi za maana kulingana na taaluma zao ni kuloteza ujuzi bure.

Jana nimekutana na mhitimu wa UDSM mwenye GPA YA 4.4 ambaye ni bodaboda. Imeniumiza sana maana kulingana na elimu yake na ufaulu wake ilipaswa awe sehemu akirithisha elimu yake kwa wengine.

Mwenye fursa za kazi za kitaaluma nje ya nchi tafadhali asaidie hawa vijana sio vyema kila swala tuiachie serikali. Kama serikali imeshindwa kuwaajiri watanzania iliyowasomesha kwa gharama zake, najua kuna nchi zina uhaba na wafanyakazi tuwapeni fursa hawa vijana wahitimu.
 
Ingependeza kama ungeanza wewe kwa kuwaonyesha baadhi ya hizo fursa kama mfano, between, nyuzi ni nyingi humu zinazozungumzia fursa za nje huko, kabla hujakimbilia kupost ungefanya marejeo humu humu, jf ni zaidi ya uijuavyo!
 
Mkuu mosi bodaboda pia ni ajira.
Pili suala sio kuwa na elimu tu ila quality ya elimu yako ni muhimu sana.

Huwa siamini sana kwenye maG.P.A makubwa kuwa ndio sababu ya wewe kufanikiwa.

Hebu watafute classmates wake wenye G.P.A za 3 tuone wapo wapi na wanafanya nini.

The true revolution comes from inside yourself....!
 
Ni kwa uzalendo uliotukuka tumeamua kubakia nchini, huko nje mababu zetu walipelekwa utumwani kwa mabavu... sio suala la kujivunia.
 
Miye nataka nizamie hapo Kenya kuchoma mishikaki japo nina kadiploma kangu ka ualimu
 
Ni afadhali hiyo bodaboda,kuna wengine wakata fesi za miba
 
Back
Top Bottom