Kwani CCM mafisadi ni Rostam, Chenge na Lowassa tu?

JOMBAAA

Member
Jun 2, 2011
25
2
Mafisadi ndani ya CCM ni wengi sana kuwapa barua hao wachache ni kama kuwafanya wananchi hawajui kitu. Kwa taarifa yenu mnajidanganya tena ndo mnazidi kuua chama.wapinzani watazidi kupeta na kuongezeka kila siku. UKWELI NDO HUO!
 
Hao ndio vinara wa wizi ! Uking'oa mizizi matawi yatakufa.
Hao ni waizi wa mali ya umma wakongwe.
 
Hao ndio vinara wa wizi ! Uking'oa mizizi matawi yatakufa.
Hao ni waizi wa mali ya umma wakongwe.

Mkuu, nitajie hawa uliowataja wameiba nini, mimi nakutajia:JK ameiba kwenye meremeta na ndiye beneficially wa IPTL ndo maana pamoja na kuwa IPTL ina zalisha umeme kwa gahrama kubwa kuliko hata Dowans bado gvt imengangania IPTL izalishe umeme lakini Dowans NO.
 
Nimesoma Raia Mwema kuhusu utetezi wa Lowasa kwenye vikao vya ccm, hivi hata ukiwa wewe ndo lowasa utakubali kufukuzwa? CCm kuna mafisadi nafikiri asilimia 90, na 10 iliyobaki ndo wanaweza angalau kuwa safi. I am not lowasa fan but it makes sense. Wapo wengi ambao hata sina sababu ya kuwataja hapa, ccm inabidi iwafukuze wote wanaotuhumiwa na kashfa za rushwa na ndio lowasa ataridhika or else inabidi wamuangalie kwa ukaribu sana ama sivyo ataisambaratisha ccm. The guy doesnt want to loose, jamaa ni mgumu aiseee. Na sie tunasubiri hilo litokee ili tujitwalie nchi kirahisi! ccm hakuna msafi they are all rotten.
 
na wewe pia ni ROTTEN kama ni hivo....!!!

unaona raha kuwaambia wenzako rotten....!!


basi na wewe ni rotten namba moja, tena uliyekubuhiu....!
 
na wewe pia ni ROTTEN kama ni hivo....!!!

unaona raha kuwaambia wenzako rotten....!!


basi na wewe ni rotten namba moja, tena uliyekubuhiu....!
Kumbe wewe ndio CCM na CCM ni wewe aibuuuu hiloooooooooooooooo!!
 
ufisadi ni mwingi ndani ya ccm,ufisadi wa mapacha watatu ulikuwa wazi na ulizidi kipimo.ufisadi wao umepelekea chama chao kuchafuka.kujiuzulu nafasi zao za kiserikali na kichama kumeonyesha wamekubaliana na shutuma zinazowakabili.sioni mantiki ya wao kupinga kuvuliwa gamba kwa sasa,kwa nafasi walizokuwa nazo serikalini walitakiwa kukemea matendo ya kifisadi badala yake walikaa kimya,usaliti wa namna hii haufai na wanastahili kunyongwa!Jk niazime uchair nikunyooshee watu.
 
KIGUGUMIZI CHA CCM KUJIVUA GAMBA DODOMA INA UJUMBE KWAMBA HIYO SARATANI IMESAMBAA MNO MWILINI HADI IKULU KIASI KWAMBA HATA PA KUWEZA KUKATA ILI MGONJWA AENDELEE KUISHI JAPO KWA MATUMAINI HMNA

Wingi wa mafisadi ndani ya CCM kama ambavyo wengine wanavyodai hapa hata siku moja haiwezi fisadi aliyekamatwa tayari na wananchi dhambi zake zikayeyuka tu eti kwa sababu ni kosa lililotendwa na wana CCM wengi sana, hapana!!

Hata kama zaidi ya theluthi tatu ya wana CCM wangetuhumiwa kuwa ni mafisadi, na kiukweli ndivyo hali halisi inavyoonyesha siku zote katikaa vitabu vyeusi mikononi mwetu wananchi juu yao, lakini HILO PEKEE kamwe haliondoi ukweli kwamba zoezi la kuvua gamba ndani ya chama hicho lazima ianzie mahala na kila faili kupitiwa kwa wakati wake.

Kwa msingi huo, kama ambavyo CCM lenyewe tu lilivyojitokeza na kukiri kuchukizwa na gamba kati kati yake na kuanza kujikana kujisafish na tatizo hilo sugu ili KIWEZE KUPENDEKA TENA nchini, hadi hivi sasa macho yote ni kusubiri kitu gani kinachotokea kwa kufunuliwa kwa faili zao akina
Mafisadi waliokubuhu - Chenge na Edward Lowassa huko Dodoma.

Lakini kwa bahati mbaya sana CCM ikifanyia mzaha swala la Ufisadi na mafisadi huko kwenye kikao cha huko basi sote tuhesabu tu kwamba hilo ndilo litakalokua sanda na jeneza la kisiasa nchini.

Hili la Lowassa kulialia eti kwa nini asulubiwe WAKATI YEYE ALITUKWAPULIA WANANCHI SI KWA FAIDA YA FAMILIA YAKE BALI NI KULE KULITUNISHA DHANA ILE ILE YA 'MASLAHI YA CHAMA' ndio kwanza limeongezea kuchafua mambo zaidi kwa CCMmpaka dakika hii na CHADEMA sasa kuonekana kuwa ni wakweli kupindukia juu ya tuhuma zote juu hawa magamba.

Ndio, nasema mpaka hapo tu ni kwamba amefanya kesi yake iwe mbaya zaidi na wala sidhani kama hiyo CCM anayodai kuifaidisha na wizi huo kweli wWATAMWACHI JAPO KA-KIPENYO kwenda kusema nje kile anachokiita yeye UKWELI WOTE JUU YA UFISADI WA RICHMOND alias DOWANS au kwa jina lingine SI-MBIONI.

Nimesoma Raia Mwema kuhusu utetezi wa Lowasa kwenye vikao vya ccm, hivi hata ukiwa wewe ndo lowasa utakubali kufukuzwa?

CCm kuna mafisadi nafikiri asilimia 90, na 10 iliyobaki ndo wanaweza angalau kuwa safi. I am not lowasa fan but it makes sense. Wapo wengi ambao hata sina sababu ya kuwataja hapa, ccm inabidi iwafukuze wote wanaotuhumiwa na kashfa za rushwa na ndio lowasa ataridhika or else inabidi wamuangalie kwa ukaribu sana ama sivyo ataisambaratisha ccm.

The guy doesnt want to loose, jamaa ni mgumu aiseee. Na sie tunasubiri hilo litokee ili tujitwalie nchi kirahisi! ccm hakuna msafi they are all rotten.
 
Siyo kweli kwamba Lowassa na Chenge pekee ndo mafisadi kwenye ccm. Ccm yote imeoza, wote ni mafisadi na hata hao 10% uliosema ni wazuri labda wanaweza kuwa afadhali tu, lakini hakuna msafi hata mmoja. Hata mwenyekiti wao ni fisadi nyangumi, ndo maana anakosa legitimacy ya kuwawajibisha mafisadi wenzie.
Huwezi ukawa msafi na kuwa kiongozi ndani ya ccm maana uongozi ndani ya ccm unapatikana kwa ufisadi.
 
Wasubiri kuhukumiwa na enzi,kifo chao kitakua cha aibu kulikoni Gaddafi na wale waliokuwa wamemzunguka,wakati unakuja ambao watajutia sana maamuzi haya mabovu ya kulindana,jamani,labda Kama nchi hii iko ktk sayari nyingine,lakini Kama ni hii hii dunia tuliyomo ndio nchi hii ipo,basi waangalie,Kenya,Zambia,Malawi,Tunisia Libya Misri na nk.AMA kweli sikio la kufa halisikii dawa.....nuku....

Habari za huko mliko lala...Chaka chetu kikubwa sana....hahahaha.....

Wameisha.
 
Sio,tatizo Lao ni Uchu WA madaraka,ubinafsi,kisasi,ubaguzi na ukabila.....hay a ndio yanayowaumiza watu hawa wawili.
 
Hilo ndilo suala la kujiuliza. Leo wanaweza kuwafukuza hao lakini kwenye ile list ya mwembeyanga watakuwa wamebaki wanane! Watarudi tena kuwafukuza hao wanane waliobaki na itakuwa ni kufukuzana na kusahau kutekeleza ilani ya Uchaguzi.
 
kwani lowasa akifukuzwa ndo mswada wa katiba utarudishwa kwa wananchi?kama ndo hivyo poa na afukuzwe lkn kama sio hivyo, kufukuzwa kwake sithani kama kutafanya ufisadi unaoendelea kwenye wizara za maliasili,nishati na matumizi mengine mabaya ya fedha za umma utakosa,hii ni technic ya wala rushwa kugeuza attention ya watz kwa lowassa huku wakiendelea kuiba hela,na watz walivyo mazezeta na yenyewe yamegeza shingo hukohuko kwa lowasa huku pesa ikizidi kuibiwa kila kukicha!
 
Back
Top Bottom