Kwangu, Zitto Mbunge wa kipekee mwaka 2012

Kwangu, Zitto Mbunge wa kipekee mwaka 2012

nice 2

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2011
Posts
747
Reaction score
520
  • Kila mkutano alianzisha na kusimamia ajenda
  • Wengi walidandia kwa kuunga mkono au kupinga


KUNA namna nyingi za kuelezea taswira ya Bunge na wabunge katika mikutano yake minne ndani ya mwaka 2012, uliokwisha. Unaweza kulielezea Bunge na wabunge kwa kutazama aina ya hoja zilivyoendeshwa ndani ya chombo hicho nyeti nchini.

Lakini pia Bunge linaweza, kwa kadiri ya fursa za mijadala, kupambanua uwezo binafsi wa kila mbunge. Kwa mfano, nani mbunge hodari ‘kudandia' hoja na hata kuiteka na kuiboresha. Nani mbunge hodari wa kuvuruga hoja zenye maslahi kwa taifa, na zaidi, nani mbunge hodari kutohudhuria vikao vya Bunge.

Nani mbunge mahiri katika kushauri pale ushauri wa kibunge unapohitajika katika masuala nyeti na tata nchini. Lakini mbali na hapo, nani mbunge wa kufoka zaidi, yaani nguvu nyingi hoja za msingi chache katika dakika za kujieleza kwake ndani ya Bunge.
Safari ya Bunge na wabunge katika mwaka 2012 imekwisha na sasa ni safari mpya ya 2013. Wabunge wamejipanga vipi, tutarajie nini hasa kwa manufaa ya taifa kutoka kwao? Ili angalau kutabiri ya mwaka 2013 ni vizuri kupitia ya muhimu katika 2012.

Itakumbukwa kwamba mkutano wa 12 wa Bunge ulihitimishwa Novemba 2012, kwa aina yake. Siku mbili za mwisho za mkutano huo zilichangamsha vikao vya Bunge kutokana na aina ya hoja zilizowasilishwa na kujadiliwa. Zilikuwa hoja zinazogusa moja kwa moja maslahi ya wananchi na nchi kwa ujumla.

Hoja ya Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee, kuhusu masuala ya ardhi sambamba na hoja ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) Zitto Kabwe, kuhusu Watanzania waliotorosha mabilioni ya fedha na kuzificha huko ughaibuni na hasa nchini Uswiss, ndizo zilizochangamsha mno uhitimishaji wa mkutano wa Bunge kwa mwaka 2012.

Hizo bado hoja viporo, serikali imeahidi Bunge kwenda kuzifanyia kazi na bila shaka, namna zitakavyotua kwa mara nyingine bungeni mwaka huu wa 2013 itategemea na utekelezaji wa serikali.

Licha ya kwamba Zitto na January Makamba (kabla Makamba hajateuliwa naibu waziri Mei 2012) walipata kung'ara bungeni katika sakata la kupinga wabunge kuongezewa posho za vikao, lakini Zitto kwa ujumla wake, Zitto anang'ara zaidi kwenye masuala mbalimbali aliyoyaibua bungeni, akiwa na rekodi ya kuanzisha hoja zinazoungwa mkono kwa sehemu kubwa ya Bunge na hata kwa wananchi mitaani.

Kwa mfano, katika mkutano wa kwanza wa Bunge mwaka 2012 (mkutano wa sita), Zitto akiwa ametoka kwenye matibabu nchini India, aliwasilisha bungeni hoja ya zao la mkonge.

Katika hoja hiyo alitaka serikali kuwekeza vya kutosha kupitia wakulima wadogo wadogo ili kuongeza uzalishaji wa mkonge nchini. Alitaka Tanzania irejee kuwa taifa la kwanza duniani kwa kuzalisha mkonge mwingi zaidi kuliko mataifa yote duniani.

Itakumbukwa kwamba hoja hii ilipingwa na wabunge kupitia Mbunge wa Korogwe Mjini, Yusuph Nassir. Hata hivyo, Zitto aliamua kufanya ziara ya kisiasa mkoani Tanga kuipeleka hoja yake kwa wananchi na hatimaye katika vikao vya Mkoa wa Tanga (RCC), uamuzi wa kutekeleza hoja hiyo ulifikiwa rasmi.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga alitangaza kauli mbiu ya "Tanga ni Mkonge na Mkonge ni Tanga" na kuanza mara moja kulipa stahili za wafanyakazi wa zamani wa Mamlaka ya Mkonge Tanzania na hatimaye kuanza kuangalia upya ardhi iliyotengwa kwa mashamba makubwa ya mkonge na kuigawa kwa wananchi, wakulima wadogo wadogo.

Mkutano wa saba wa Bunge ulikuwa mkutano wa kihistoria kwani kwa mara ya kwanza, kusudio la hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu wa Tanzania liliibuka.

Katika historia ya Uhuru wa Tanganyika na Muungano wa Tanzania, haijapata kutokea mbunge kutoa hoja ya kutaka kumng'oa Waziri Mkuu kwa kutokuwa na imani naye.

Zitto alisimamia hoja hii, akiunganisha makundi ya wabunge ili kupata sahihi 75 zilizounga mkono hoja yake. Chama chake (CHADEMA) kina wabunge 48 tu na kama Zitto angekuwa hana kipaji cha ushawishi basi ingekuwa vigumu kupata angalau sahihi za wabunge 70 zilizotakiwa ili hoja iweze kuwa hoja.

Hoja hii ilikuwa na mafanikio makubwa sana na kati ya matokeo yake ni Rais Jakaya Kikwete kufanya mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri katika kile kilichoweza kutafsiriwa kuwa ni kumwokoa Waziri Mkuu lakini pia kuimarisha utendaji kazi wa serikalini bungeni na nchini kwa ujumla.

Mawaziri wanane waliondolewa na Rais Kikwete kupata fursa ya kuteua mawaziri wapya na hivyo kupata timu ya wachapa kazi ambao ni pamoja na Waziri Dk. Harrison Mwakyembe, Balozi Khamis Kagasheki na Prof. Sospeter Muhongo.
Kulikuwa na maneno kwamba Zitto alitumwa na Rais Kikwete kutoa hoja hii, jambo ambalo Zitto binafsi alilipinga vikali. Maneno haya yanatokana na ukaribu unaodaiwa kuwapo kati ya Zitto na Kikwete, jambo ambalo licha ya kuleta wasiwasi wa kisiasa lakini wakati mwingine ukaribu huu ulisaidia sana kukamilisha suala la Katiba.

Gazeti hili la Raia Mwema liliwahi kuandika namna ambavyo Zitto alitumia uhusiano wake mzuri na wazee wastaafu kama Jaji Joseph Warioba na Dk. Salim Ahmed Salim kwa upande mmoja na ukaribu wake na Rais Kikwete kwa upande mwingine, kuhakikisha CHADEMA wanaingia kwenye mchakato wa kuandika Katiba, baada ya kususia kujadili Muswada wa Sheria Mabadiliko ya Katiba bungeni.

Lakini mkutano wa nane wa Bunge pia ulikuwa mkutano uliotishia heshima ya Zitto kimaadili. Zitto alihusishwa na kundi la wabunge walioonekana kumtetea aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, William Mhando.

Mhando alisimamishwa kazi TANESCO na baadaye kuachishwa rasmi kazi hiyo baada ya Bodi ya TANESCO kujiridhisha kuwa alijihusika katika ukiukwaji wa maadili kwa kutoa biashara kwa kampuni ya mkewe.

Ingawa Spika alitoa uamuzi wake kwamba wabunge hawakujihusisha na rushwa, lakini Zitto anapaswa kuwa makini sana siku za usoni kutojihusisha na watendaji ambao maadili yao ni ya shaka.

Licha ya suala hili, Zitto pia alifanikisha kuandikwa kwa sheria ya fedha 2012, akiwa amefanikiwa kuandika na kupitisha mapendekezo yake ya sheria ya kulinda viwanda vya ndani vya nguo na maziwa.

Vile vile sheria ya nyongeza ya mitaji (capital gains) kwa kampuni zinazouziana rasilimali za nchi na pia sheria ya kulinda haki za wasanii ambapo kwa sasa, kazi zao zitalindwa kwa mujibu wa wigo wa taratibu za kodi.

Mkutano wa tisa ambao ndio mkutano wa mwisho kwa mwaka 2012, ulimalizika kwa kishindo kwa Zitto kuibuka shujaa wa kupambana na mafisadi watoroshaji wa fedha za kigeni za nchi.

Zitto alifanikiwa kuunganisha wabunge bila kujali itikadi zao za vyama kupitisha hoja binafsi iliyotaka serikali kuchukua hatua dhidi ya mabilioni ya fedha yaliyofichwa Uswiss.

Licha ya juhudi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Frederick Werema, kutaka kuilainisha hoja hii, hoja ilipita kwa kishindo na kuweka historia ya moja ya mabunge katika Afrika yaliyoamua kuchukua hatua dhidi ya utoroshaji wa fedha na kufichwa ughaibuni.

Nilizungumza na Zitto mwenyewe wakati fulani mwaka jana kuhusu mafanikio ya kazi zake za kibunge katika mwaka 2012 naye alinijibu na nadhani ni vizuri nikanukuu kwamba- "Kwanza ifahamike kuwa hoja ya mabilioni ya Uswiss ni hoja ya kwanza binafsi iliyowasilishwa na kupitishwa na Bunge tangu nimekuwa Mbunge.

"Nimefurahi kufanikisha juhudi hizi za kupambana na ufisadi. Watu waone kuwa hawana pa kujificha wakiiba mali ya umma. Pili, ili mbunge afanikiwe katika kazi za ubunge lazima ajisomee.

"Tatizo la wabunge wengi, hasa wabunge vijana wanaendekeza sana starehe na kusahau majukumu yao ya kibunge. Mimi tangu nimekuwa mbunge sijawahi kufika Mnadani (eneo la nyama choma-Dodoma), lakini kuna wabunge bila kujali uzito wa kazi, kila Jumamosi wapo Mnadani.

"Wanashinda kwenye baa kunywa na kutafuta wanawake. Huwezi kuwa mbunge bora kama Dodoma kwako ni nyakati za starehe badala ya kazi. Tatu, kutokukata tamaa. Mwanasiasa mahiri anakomazwa na misukosuko. Nashukuru sana wabunge wenzangu kuniunga mkono.

"Hata hivyo, suala la hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwangu inabakia hoja ya kihistoria kuliko nyingine yoyote katika maisha yangu ya kisiasa.

Natumai wachambuzi wa mambo ya siasa wataweza kuiandika historia hiyo."


Source: Raia Mwema - Kwangu, Zitto mbunge wa kipekee mwaka 2012

My Take: Naungana mkono na muandishi wa makala hii, na kumuombea kwa Mungu bw. Zitto aendelee kufanya vizuri kwa maendeleo ya taifa letu mwaka 2013
 
ni mbunge mahiri nakubali lakini mbona kama ameruhusu unafiki umzunguke?
 
Kinachomsumbua Zitto ni unafiki na kutumika, akili anazo...
 
nice 2!

Amekulipa shilingi ngapi ili 'umfagilie' humu jamvin?
 
Zitto Namkubali ni mahiri wa kujenga hoja na kuzitetea! Zitto ooyeeeeeeeee!
 
hiyo ya kutokuwa na imani na w/mkuu aliumwa sikio

Lissu was the best
 
this is extremely the cheapest analysis, unastahili kupuuzwa, hata hivyo Lissu was the best n the possible next president of URTZ
 
Hata SHETANI alikuwa Malaika tamaa ikamponza so ZKK wa sasa sio yule aliye aminiwa na wtu wa rika zote miaka iliyopita, nawambieni huyu ZZK wa sasa ni janga kwa maskini na wazalendo wanaotafuta ukombozi wa pili wa nchi yetu, Ukichunguza mambo yote aliyofanya shetani wakati akiasi na ZZK ndiyo anayoyafanya sasa hivi ni tangu lini kwa mtu msomi na kijana wa karne hii ya high tech akatishia kuloga hadi panya wasio na hatia????
 
Ndugu zangu hebu tumuache huyu mtu apumue!! Kila siku tunamuandama.


Sent from my Nokia 8310 using Tapatalk
 
Usituchanganye kuna vigezo vya kumpata mbunge bora wa mwaka, mojawapo ni kiasi cha michango bungeni , maswali just to mention few qualities.He/she who qualifies must have attained the minimum requirements zitto is behind Mnyika there is no way one could talk anti-fact
 
"Nimefurahi kufanikisha juhudi hizi za kupambana na ufisadi. Watu waone kuwa hawana pa kujificha wakiiba mali ya umma. Pili, ili mbunge afanikiwe katika kazi za ubunge lazima ajisomee.

"Tatizo la wabunge wengi, hasa wabunge vijana wanaendekeza sana starehe na kusahau majukumu yao ya kibunge. Mimi tangu nimekuwa mbunge sijawahi kufika Mnadani (eneo la nyama choma-Dodoma), lakini kuna wabunge bila kujali uzito wa kazi, kila Jumamosi wapo Mnadani.

"Wanashinda kwenye baa kunywa na kutafuta wanawake. Huwezi kuwa mbunge bora kama Dodoma kwako ni nyakati za starehe badala ya kazi. Tatu, kutokukata tamaa. Mwanasiasa mahiri anakomazwa na misukosuko. Nashukuru sana wabunge wenzangu kuniunga mkono.

"Hata hivyo, suala la hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwangu inabakia hoja ya kihistoria kuliko nyingine yoyote katika maisha yangu ya kisiasa.

Natumai wachambuzi wa mambo ya siasa wataweza kuiandika historia hiyo."
Siasa za Tanzania zinachekesha sana. Zinahitaji usanii wa kucheza na akili za watanzania ambao wengi hawaoni correlation kati ya siasa na maendeleo yao ya kila siku. Kwa mfano huyu jamaa anajifanya eti ''mafisadi waone hakuna mahali pa kujificha'' wakati mafisadi wa Tanzania wala hawana sababu ya kujificha kwani hakuna wanacho ogopa.
 
Watatupa ban kwa name calling ,ukweli unabaki this is the same person trying hard to clean his name shame mods
 
Huu ni mtazamo wake hatujui ameangalia nini akaona Zitto ni mbunge bora 2012 kwangu mimi Zitto ni sawa na Makinda,Mwigulu au Lukuvi hayupo sawa na Mnyika wala Lissu,hana uwezo sio tu wa kuvaa viatu vyao bali hata kushika kidamu ya viatu vyao(viatu vya Lissu na Mnyika)
 
Huyu Matunguli anafaa kuwa mbunge mchawi kuliko wote!si amejitangaza mwenyewe?acha kuzunguka mr Matunguli tumeshang'amua ni ww unajaribu kupima kina cha maji hapa.Hakuna jembe 2012 bungeni kama Lissu.Mihimili yote ya dola ameitikisa barabara,hana chembe ya unafiki.Matunguli bingwa wa kupayuka na kutishia haja ndogo wakati anahara!taja na uthibitishe hao wenye fedha Uswis kama Dr Slaa enzi yake tujue we kidume,au ndo unawatisha ili wakupoze?
 
yako wap makali ya zito? mbon ka2lia?
kwa upande wa wana ccm lazima mumpode Zito maana sio sera zenu kuwasaidia wananchi sera zenu ni kuwakandamiza wananchi na ufisadi, lakini mwisho wenu utafika tu,
 
Huyu Matunguli anafaa kuwa mbunge mchawi kuliko wote!si amejitangaza mwenyewe?acha kuzunguka mr Matunguli tumeshang'amua ni ww unajaribu kupima kina cha maji hapa.Hakuna jembe 2012 bungeni kama Lissu.Mihimili yote ya dola ameitikisa barabara,hana chembe ya unafiki.Matunguli bingwa wa kupayuka na kutishia haja ndogo wakati anahara!taja na uthibitishe hao wenye fedha Uswis kama Dr Slaa enzi yake tujue we kidume,au ndo unawatisha ili wakupoze?
tunachosema chadema nyinyi ccm tumeshawangundua hizo ndizo kauli zenu sisi wanachadema kauli hiyo ingekuwa imetoka kinywani kwa mboe au Silaa, tungeiamini lakini kwa maneno yako unajisumbua.
 
Huu ni mtazamo wake hatujui ameangalia nini akaona Zitto ni mbunge bora 2012 kwangu mimi Zitto ni sawa na Makinda,Mwigulu au Lukuvi hayupo sawa na Mnyika wala Lissu,hana uwezo sio tu wa kuvaa viatu vyao bali hata kushika kidamu ya viatu vyao(viatu vya Lissu na Mnyika)
kwa maneno yako hayo wewe sio mwana chadema, sisi sasa hivi akisifiwa kiongozi yoyote wa chadema tunaunga mkono,ccm hawana ujanja wa kujifanya ni chadema alafu wanalaumu mipango yetu,mambo hayo yalikuwa zamani
 
Huwezi kuwa mbunge mahili kama unaendekeza ulevi, Zitti ni mbunge anayejituma, na anauwezo mkubwa wa kupambanua mambo. Ni mbunge pekee mwaka 2012.
 
Back
Top Bottom