Habari yenu ndugu zangu.
Nimekuja kwenu nione kama kidogo naweza kushusha mzigo toka moyoni kwa yale ninayopitia. Sababu ya kunifanya nijiisi napotea ni Pombe,nimekua mtumiaji mzuri sana wa pombe kiasi naona kabisa inakoelekea ni kunipoteza.
Kiukweli kama ni mtumiaji wa kilevi nikikuelezea pombe ninayokunywa utajua kabisa mim sio mnywaji ni mlevi. Sio bia tu ata pombe kali mim kote nipo,ilifika kipindi naweza kunywa Kvant kubwa na safari kubwa sita peke yangu na hapo nakua sijakata moto.
Imefika kipindi naona sasa sitaki tena sababu inakoelekea ni kuniondolea sio tu reputation yangu bali vitu vyote nilivyotafuta kwa jasho.
Sijui nifanyeje nitokane na ili janga naisi pia ushauri kutoka kwa watu walioacha na mipombe utanisaidia namna walivyopamba na huyu ambae kabisa kwangu amekua adui.
Asante