Kwako Waziri wa Nishati na Madini

Kwako Waziri wa Nishati na Madini

Vijisenti

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2011
Posts
544
Reaction score
330
Sisi wananchi wa Newala tunafikisha malalamiko yetu kwako kutokana na vitendo vinavyofanywa na shirika la umeme TANESCO, wengi wetu tunajiamini kuwa tumelipa bili na hatudaiwi, jambo la kushangaza mwaka huu TANESCO wameibuka ghafla na kuanza kuwapachikia watu madeni makubwa makubwa zoezi ambalo linaenda sambamba na ukataji wa umeme. Ukipeleka risiti zao wanakurudisha miaka ya nyuma 2010,2011,2012 na 2013 na wanafanya hivi kwa kujua wengi wamepoteza karatasi za bili, mfano kwenye deni langu inaonesha mwaka 2012 sijalipa kwa miezi 6 wakati si kweli kwani Tanesco kama hujalipa mwezi 1 tu unakatiwa umeme.

Huu ni uonevu mkubwa sana kama kuna muhasibu au meneja alikuwa hawasilishimalipo yetu isiwe sababu ya kulipa deni hilo kwa kuwakata wananchi maskini, nimeshuhudia jamaa mmoja ambaye alikuwa na deni la milioni mbili akiwa na rundo la karatasi za bili na hadi mwisho wa uhakiki deni lake likabaki 68,000 tena baada ya baadhi ya risiti kutoonekana, Tafadhali muheshimiwa Waziri tunakuomba msaada juu ya hili.
ALIYEIBA AKAMATWE ISITUMIKE MBINU YA KUSAWAZISHA DENI KUPITIA MIFUKO YA WANANCHI MASKINI.
 
usiwe na wasi wasi kijana hapo newala kuna tatizo lilitokea kwenye ofisi yetu,tuliibiwa computer zote ambazo zilikuwa zinadata za malipo yote,pia walituibia nyaraka na baadh ya kopi ya risiti za malipo na hivyo kufanya mahesabu ya fedha za miaka iliyopita kuwa ngumu,lakin usiwe na was was,tuletee hizo risiti ili tufid upwa kwenye machine zetu.ok,nakutakia kazi njema
 
Tatizo wanatulipisha bili mara mbilimbili yaani kama risiti za miaka ya nyuma zimepotea ndio basi tena.
 
usiwe na wasi wasi kijana hapo newala kuna tatizo lilitokea kwenye ofisi yetu,tuliibiwa computer zote ambazo zilikuwa zinadata za malipo yote,pia walituibia nyaraka na baadh ya kopi ya risiti za malipo na hivyo kufanya mahesabu ya fedha za miaka iliyopita kuwa ngumu,lakin usiwe na was was,tuletee hizo risiti ili tufid upwa kwenye machine zetu.ok,nakutakia kazi njema
we naye acha kuongopea watu, ina maana data base ya newala iko humo humo kwenye hizo pc zilizoibiwa!?? kuibiwa pc na data base imefutika?? vitu serious vijibiwe kwa u serious, kuna jukwaa la jokes kule kashinde kule au nenda fb kabisa. mtu ana malalamiko ya msingi we unaleta utani!!
 
Back
Top Bottom