Kwako Waziri Wa Mali Asili Na Utalii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwako Waziri Wa Mali Asili Na Utalii

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ndallo, Mar 15, 2011.

 1. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Muheshimiwa waziri wa mali asili na utalii ndugu Ezekiel Maige huu ni ushauri wangu na maoni yangu toka moyoni mwangu, Kutokana na kupewa sekta hii nyeti nchini kwetu nachukua nafasi hii kukushauri kupitia safu hii hapa JF kuhusiana na sekta ya utalii nchini mwetu.

  Kwanza nakupa pongezi kwakupewa sekta hii nyeti na kipindi hiki cha pili kumalizia nngwe ya mwisho ya muheshimiwa Jk katika kukaa kwake madarakani. Mada yenyewe ni kuhusiana na kukuza sekta hii kubwa ya utalii nchini mwetu tuna vivutio vingi sana hapa kwetu lakini bado ni ndoto kwa mwananchi wa tanzania kuyaona maisha bora kupitia sekta hii.

  Lakini sasa hivi naona huu ndio muda muafaka wa kukuza sekta hii kupitia Loliondo hususani kuchanganya na mbuga zilizo jirani kupita njiia kuu iendayo kwa Babu, ni matumaini yangu kua kama kweli muheshimiwa katika kutangaza sekta hii kubwa ya utalii nchini tukaitangaza Loliondo kupitia tiba anayotoa Babu hususani kwenye kutibu gonjwa kubwa kama la ukimwi.

  Muheshimiwa waziri kama ilivyoada kwa watalii wanapouziwa ratiba kwaajili ya kutembelea mbuga zetu ingependeza kama watalii hawa wakauziwa mtiririko huu hapa endapo mgeni ana kama holiday ya wiki moja au mbili chukulia mfano huu:

  1. Arrival Kilimanjaro Airport to Arusha
  2. Arusha - Tarangire N. Park
  3. Lake Manyara N. Park
  4. Loliondo kwa Babu
  5. Loliondo kwa Babu kupata dawa
  6. Loliondo Lake Natroni
  7. Lake Natroni Serengeti
  8. Serengeti
  9. Serengeti - Ngorongoro
  10. Ngorongoro Crater - Arusha mwisho wa safari.
  Muheshimiwa waziri huu ni mtiririko wa safari endapo kama wewe na serikali yako mtaamua kuutangaza utalii wetu bila kusahau kutilia mkazo eneo la Loliondo ni moja ya maajabu duniani kwa sasa hivi na watu wameshatoa ushuhuda kua wamepona kweli nakuhakikishia sekta ya utalii itakua kubwa zaidi na zaidi na hakuna zawadi kubwa tuliyopewa kutoka kwa Mungu kama hii! Tafadhali muheshimiwa kama upo hapa JF au kama kuna ndugu yako ambaye ni mwanachama wa JF peleka huu ujumbe haraka sana kabla siasa haijaingia Loliondo. Nawasilisha.
   
 2. seniorgeek

  seniorgeek JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2011
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 500
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tour company ndio wanaopanga itinerary na inauzwa kama package na siyo ministry.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,947
  Trophy Points: 280
  infrastructure zinaruhusu?
   
 4. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Pamoja na tour company wao kupanga hii package lakini lengo kubwa hapa ni msisitizo kuuza eneo la Loliondo kua ni eneo la kitalii mkulu!
   
 5. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Mkulu Ivuga wakati ndio huu hatuna muda mwingine miundombinu kuanzia sasa hivi ianze kufanyiwa kazi!
   
Loading...