Kwanza nikupe pole kwa majukumu ya kila siku, pili nikupongeze kwa yale uliyoweza kuyafanya katika utawala wako na kwa yale uliyoshindwa ujitathmini na kuchukua hatua. Binafsi sijawahi kuleta maoni yangu ya aina yoyote kwako hivyo kupitia mtandao huu najua utaletewa taarifa.
Mimi ni mdau mkubwa sana wa elimu. Nina furaha jinsi ambavyo nchi hii ilikuwa karibu ya mwisho kwa kuwa na idadi ndogo ya vyuo vikuu Afrika mashariki lakini leo hii Tanzania inaongoza kwa kuwa na idadi ya zaidi ya vyuo vikuu 28, zaidi ya vyuo vikuu vishiriki 19, na 'centers' za vyuo vikuu zaidi ya 14. Na pia vipo vyuo vingine vingi vinavyosimamiwa na nacte vinatoa elimu ya juu haya ni maendeleo.
Zipo nchi duniani zimwekeza katika huduma ya elimu. Kwa Tanzania pia tunaweza kuwekeza katika elimu na kujitangaza katika nchi za Afrika kupata wanafunzi kuja kusoma kwa kulipa ada kama ambavyo Uganda imekuwa na mafanikio kwa kupata wanafunzi wa nchi mbalimbali maana zimeanza kuonekana dalili kuwa baadhi ya vyuo vinakosa wanafunzi kwa sababu idadi ya wanafunzi wa ndani ni ndogo.
Kwa kuangalia mbele na idadi ya wanafunzi inavyoongezeka kutoka shule za kata bado tunahitaji idadi kubwa ya wasomi wa vyuo vikuu na vyuo vya kati/ufundi.
Napendekeza Muheshimiwa Raisi agiza wakuu wote wa mikoa kutenga maeneo kwa ajili ya vyuo vikuu vya serikali angalau kila mkoa uwe na chuo kikuu chake. Zitengenezwe kamati za wananchi kusimamia uchangiaji kwa kushirikiana na serikali na pia wapewe uwezo na mamlaka ya kushirikiana na vyuo vikuu vya nje kusimamia na kuendeleza taasisi.
Au la vialikwe vyuo vikubwa duniani wapewe maeneo kwa ajili ya kujenga vyuo hapa Tanzania. Baada ya miaka kumi hadi 20 Tanzania itakuwa ni education hub ya Afrika na wananchi tutakukumbuka kwa hili pia.