Kwanza kabisa naomba pokea salamu zangu na za watu wangu wa karibu. Pili naomba niwapongeze kwa utekelezaji wa majukumu mazito wa ujenzi wa Tarifa letu pendwa Tanzania.
Mh. Katambi,takribani wiki ya pili sasa nipo Dodoma ndani ya wiilaya yako ya Dodoma mjini.
Katika pitapita zangu kwenye shughuli zangu za kujitafutia mkate wangu wa kila siku,nimebahatika kukutana na vijana kwa nyakati na sehemu tofauti tofauti. Kikubwa hasa kinachozungumzwa na vijana hawa waliojichokea na kujikatia tamaa juu ya hatma ya maisha yao ya kesho, hasa ni juu ya ile kauli ya Afisa maendeleo ya Manispaa ya Dodoma mjini, aliyoitoa usiku ule wa Jumamosi yaTamasha la Burudani la Fiesta pale uwanjan wa Jamuhuri Dodoma.
Ni kama vijana hawana imani na Maneno ya Afisa maendeleo huyo, inaonekana alikuwa anafanya siasa kuuhadaa uma/vijana lakini ukweli mambo ni tofauti kabisa.
Alizungumzia kuhusu mikopo inayotolewa na Halmashauri,nanukuu" Mwaka wa fedha uliosha(2018-2019) Halmashauri ilitenga na walitoa mikopo zaidi ya Billion 2, kwa ajili ya mikopo ya Vijana,Kina mama na Walemavu.
Na kwa mwaka huu wa fedha (2019-20) Halmashauri imetenga zaidi ya Bn 3.5 kwa ajili ya mikopo ya makundi hayo husika, Alisisitiza Vijana wachangamkie fursa waombe mikopo".
Hakuna nilichosingizia hapa uzuri hata na ww ulikuwepo na ulimsikia.
Mh. DC ukweli wa mambo hauko kama ulizungumzwa kwa mbembwe kwenye lile jukwaa la Burudani,Baada ya kusikia ile kuli ya Afisa maendeleo nilionelea nijichanganye mtaani kwa wahuni niujue ukwel. Nilitembelea vijiwe tofauti vya kina mama ntilie,mafundi cherehani,bodaboda na vibarua wa mafundi huko maeneo ya Changombe,Nkuhungu,Kikuyu,Miuji,Makole, Skuya,kisasa, Area D, Msalato,Ombolo na sehemu nyigine nyingi tu.
Baada ya utafiti wangu niligundua kitu tofauti kabisa, Kwelli vijana walipata mwamko huhusu hiyo mikopo,walifuata taratibu za kuomba hyo mikopo ya Halmashauri yako. Lakini Mh. Kuna Vikundi vina miezi 4,5,6,7-8 havijapata hiyo mkopo na hadi sasa hakuna mikopo iliyotolewa wala dalili ya kupata hyo mkopo.
Vijana wamebakia na mamakabrasha yao ya usajili wa vikundi (katiba, cheti cha usahili na bank account kwenye mkoba yao) .
Nimebaki na mwaswali ambayo nayelekeza kwako Mh.DC ,kama ni kweli kwa mwaka wa fedha uliishia June 30, zilitengwa Bn 2, sasa kwa nini Vikunda vya Tangu Mwezi wa (4) April 2019 havijaingiziwa chochote hadi leo hii takribani miezi 8 sasa, na tayari tupo kwenye budget ya mwaka mpya wa fedha.
Na kwa mwaka huu wa fedha ulioanzia July 1,inadaiwa zimetengwa more than Bn 3.5 , mbona vile vikundi vya yangu mwaka wa fedha uliopita na hata vya mwaka huu hakuna kilichonufaika hadi leo hii?
. Nilitafakari zile kauli zilizokuwa na mbembwe toka kwa Afisa Maendeleo wa Manispaa kwamba vijana wajitokeze kwa wingi fedha zipo wakati anajua ni miezi 8 sasa imepita hawajawahi to a mkopo kwa kikundi chochote kile.
Je! alipata wapi ujasiri wa kuongea ile kauli tena mbele yako, mbele ya waziri na mbele ya mkuu wa nkoa kuwaona vijana ni wajinga kiasi kile ili hali anaujua ukweli ni miezi 8 imeshapita hakuna kikundi kilichonufaika na mikopo ya Halmashauri iliyipo ndani ya Wilaya yako ya Dodoma mjini?
Mh. DC, nakuomba usisubiri Rais aanze ziara kanda ya kati,vijana wateme nyongo zao kwa Mh. ( Vijana wameshachoka na wamejikatia tamaa na hyo mikopo ya Halmashauri yako wanaona ni siasa na ulagai za watendaji wa Halmashauri yako,walichokifanya wanetunza documents zao wanasubiria Mh rais ili wamueleze yanayoendelea
Mh. DC kama ulikuwa hulijui hili basi nimekupenyezea na ukitaka kujua ukweli itisha kikao na uwaite (Viongozi wote wa vikundi vuliyoomba mkopo kwenye halmashairi yako tena waambie waje na Documents zao.
Utastaajabu, utayaona ya Musa kuna Vikindi tangu mwezi wa 4 hadi leo vinasubiri kuwekewa pesa bila matumaini.
Nilitamani japo nikuone huenda tungeongea mengi,lkn mda wangu wa kuwpo Dodoma ulinitupa mkono.
Natambua ww n member hapa Jf,ujumbe wangu utakufikia,utausoma na hekima ya uongozi uliyojaliwa na Mungu utaufanyia kazi kwa manufaa ya Vijana,mama na ndugu zetu walemavu ndani wilaya yako kwa manufaa mapana ya Taifa letu.
Naomba nikutakie majukumu mema ya ujenzi wa Taifa.
Maendeleo hayana chama.