Kwako mheshimiwa Sumaye.

Kwako mheshimiwa Sumaye.

ndayilagije

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Posts
7,490
Reaction score
8,305
Mimi sina tatizo binafsi na wewe maana hujanikosea lolote lile.
Imenijia kukuandikia ujumbe huu kwa sababu nimesikia yaliyokupata,kwanza nikupe pole sana kiubinadamu inaumiza unaponyang'anywa au kupoteza kitu chako bila kujali kwamba ulimpa mkeo au mwanao.
Pili nakushauri ujaribu kuvaa kiatu cha wale wakazi wa Mvomero ambao hawakubahatika kufikia nafasi uliyofikia na ujisaili kama baba mwenye watoto nane halafu anamiliki ekari moja tu,ungejisikiaje kuona mtu mmoja amehodhi ekari zaidi ya 300 na wala hazilimi hata robo? Hesabu mimi zilinipita kando ila nasikia ekari moja ni sawa na kiwanja cha mpira..
Kumbuka haya ni maisha tu hakuna anayependa umasikini hasa wa ardhi,angalau basi umiliki hata ekari 50!
Wengi wanaokuonea huruma wanasema kuwa eti ni kisasi cha kisiasa,maana hata former boss wako anamiliki maeneo kuliko yako. Huenda ni kweli. Lakini hiyo haihalalishi wewe wala yeye kuhodhi ardhi yote hiyo. Naamini kama siyo kesho basi hata keshokutwa nayeye zamu yake itafika tu. Maana mkigawana hivyo Tanzania itajaa watu elfu tano tu. Sasa hawa mamilioni waende wapi?wasipokuibia watakunyang'anya tu!!
Lakini kwa kweli pole sana. Mungu akutie nguvu katika harakati zako za kila siku huku ukikumbuka kuwa kama umeonewa basi atakulipia muumba wako,la kama umeonea atawalipa pia.
Ni hayo tu kiongozi wangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nchi yetu hii hoja yako ni zaifu sana tuna mapoli mangapi mnaleta unafiki eti watu awana mashamba huo ni upuuzi atujafika uko kwa mapori yetu
 
Walizoea kujimilikisha bila kuhitaji. Hayo ni Mashamba ya Ndoto ,hawayahitaji ila Ndoto zao. Poor human being!!!
 
Mishamba yote ya nini kwani we utaishi milele?watoto wenyewe unakuta watatu sijui wanne alaf unamiliki ekari kama mia 300,sasa kajamba nani waende wapi?
 
Mimi sina tatizo binafsi na wewe maana hujanikosea lolote lile.
Imenijia kukuandikia ujumbe huu kwa sababu nimesikia yaliyokupata,kwanza nikupe pole sana kiubinadamu inaumiza unaponyang'anywa au kupoteza kitu chako bila kujali kwamba ulimpa mkeo au mwanao.
Pili nakushauri ujaribu kuvaa kiatu cha wale wakazi wa Mvomero ambao hawakubahatika kufikia nafasi uliyofikia na ujisaili kama baba mwenye watoto nane halafu anamiliki ekari moja tu,ungejisikiaje kuona mtu mmoja amehodhi ekari zaidi ya 300 na wala hazilimi hata robo? Hesabu mimi zilinipita kando ila nasikia ekari moja ni sawa na kiwanja cha mpira..
Kumbuka haya ni maisha tu hakuna anayependa umasikini hasa wa ardhi,angalau basi umiliki hata ekari 50!
Wengi wanaokuonea huruma wanasema kuwa eti ni kisasi cha kisiasa,maana hata former boss wako anamiliki maeneo kuliko yako. Huenda ni kweli. Lakini hiyo haihalalishi wewe wala yeye kuhodhi ardhi yote hiyo. Naamini kama siyo kesho basi hata keshokutwa nayeye zamu yake itafika tu. Maana mkigawana hivyo Tanzania itajaa watu elfu tano tu. Sasa hawa mamilioni waende wapi?wasipokuibia watakunyang'anya tu!!
Lakini kwa kweli pole sana. Mungu akutie nguvu katika harakati zako za kila siku huku ukikumbuka kuwa kama umeonewa basi atakulipia muumba wako,la kama umeonea atawalipa pia.
Ni hayo tu kiongozi wangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sumaye alipata lile eneo kwa mgongo wa mkewe na kwa kutumia madaraka ya uwaziri mkuu. Sumaye anasema lilikuwa la ushirika na likauzwa kwa kuwa walikuwa wanadaiwa. Waziri mkuu kununua mali ya wanachi ambao wametapeliwa na wahuni wenzie haoni kuwa ilikuwa ni unyang'anyi? Kasahau kama ile ni conflict ya wazi wazi? Hivi ni nani hapa atapanga kununua kitu cha serikali au kinachohusiana na serikali leo hii apambane na Majaliwa nae akipate? Sumaye kakosea step kama wenzie wanavyokksea na matokeo yake ni kuanguka tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muulize kwanini aliuza na kunyang'anya mashamba ya ushirika ya katesh? Tena akahamishia mashine na mitambo ya kule shambani kwake. Mbaya zaidi mashamba na.miundombinu yake yote akawauzia waburushi kina sethi wa Rugemalila huku akiwanyang'anya ndugu zake.

Laana ya huko kwao haitomwacha salama.

Hiyo ndiyo huitwa KARMA

Ana mengi ya kutueleza,asiishie tu kujificha nyuma ya chadema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nchi yetu hii hoja yako ni zaifu sana tuna mapoli mangapi mnaleta unafiki eti watu awana mashamba huo ni upuuzi atujafika uko kwa mapori yetu

Kweli mali ya mjinga ni akili yake. Kweli kabisa unaongea haya wewe. Kwa sisi wananchi ambao Hawa viongozi walichukua kutokana na hadhi zao. Embu Kanye kwanza Afu Rudi hapa toa point.
 
Watu wanashindw a Pa kulima. Kisa ardhi we unaongea toka wapi unapozungumzia mapori mengi. Mtz wa mvonero aende wapi. Mbali na home kwake. Pumba sana wewe
 
Kweli mali ya mjinga ni akili yake. Kweli kabisa unaongea haya wewe. Kwa sisi wananchi ambao Hawa viongozi walichukua kutokana na hadhi zao. Embu Kanye kwanza Afu Rudi hapa toa point.
Mlaumu baba ako kwanini akuwa na hadhi na yeye achukue sio unilete mimi shida zako kula kwa urefu wa kamba yako unataka usawa dunia hii uku umelala nyumbani,siri ya kupata ni kutaka sio kuzawadiwa mnaleta uvivu wa kufikiri eeh
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom