Kwako Mheshimiwa Hussein Ammar kassu Mbuge wa Jimbo la Nyang'hwale Geita

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Feb 26, 2024
479
665
Wasalam Mheshimiwa Mbuge wetu.


Kwanza nichukue fursa hii kukupongeza bila kinyongo Wala kijicho Cha aina yoyote.

Mheshimiwa Mbuge Ndg Hussein Ammar kassu Kwa miaka karibia 20 sasa tulikupa Jimbo letu la Nyang'hwale liwe mikononi mwako. Ukituwakilisha nakutatua changamoto zetu hakika unastahili pongeza sana mh!


Siwezi kutaja hapa mambo yote mazuri yote uliyofanya maana ni mengi (Nina jarada lako mambo makubwa ulivyo fanya) nakiri wazi kabisa yakuwa Mimi nimiongoni wa vijana wako watiifu sana.


Mh Mbuge Kwa miaka ya mwanzo ulifanya vyema sana sana Wana Nyang'hwale tulijuvunia sana kupata Mbuge unaesikiliza nakutatua changamoto zetu Kwa Wakati.


Lakini Kwa miaka ya Hivi karibu utendaji wako wa kazi umepunguza Kwa kiasi kikubwa sana.

Mh Mbuge umeshindwa kabisa kutatua changamoto ya barabara ya kutoka karumwa (msalala) kwenda kakola Ili Hali ukijua wazi kabisa kuwa barabara hii Ina mchango mkubwa kabisa kiuchumi na kimaendeleo.

Barabara hii haipitiki hata Kwa pikipiki inapitika Kwa watembea miguu pekee Yao hasa pale mvua inaponyesha!!
Mh Hilo hulioni kweli?

Mwaka Jana hapo nyang'omago njia panda ya kwenda nyamikonze,kafita msalala karumwa na kakola watu 4 wamesombwa na maji nasio kwamba hili limesababishwa na mvua kubwa la hasha mana hili Kila mwaka hutokea maji hupita juu ya barabara kupita kiasi lakini Cha ajabu hujawahi fanya matengenezo yoyote.

Tangu barabara hii iachwe kutengezwa na watu wa mgodi ushaitelekeza kabisa.

Mh Mbuge kumbuka gari (madampa )yako ndo zinaharibu Kwa kiasi kikubwa hii barabara. Maana hayo maloli yanayobeba michanga Yako ya dhahabu yanakuwa na Tani nyingi kuliko uimara wa barabara hii

Cha ajabu hutaki kutengeneza ikinyesha mvua kidogo tu basi safari ya kwenda msalala au kakola Imeisha Hadi usubiri mwanga wa jua!

Je haya maisha tutayaishi Hadi lini Mheshimiwa Mbuge? Huoni wananchi wako tunateseka na kusumbuka Kila Leo?

Nikweli hujui wakazi wa lushimba,kafita,Kanegele , Bumanda na karumwa wanategemea kupeleka mpunga wao kakola?

Unajuwa wazi kabisa kuwa wakulima ni wengi soko la mpunga wao karumwa pekee halitoshelezi hivyo huwalazimu kupeleka kakola kwanini barabara iliyo na umuhimu kiasi hiki umeitegea mgongo?

Muheshimu itakuwa ajabu kubwa sana barabara hii usipoitengeneza halafu bila aibu uje utuombe kura!!

Mh nakuomba sana fanya jitihada zozote Wala usisubiri kiangazi ndo uitengeneza ni Bora mara mia ukaleta hata changalawe kwanza kabla hujaja kufanya matengenezo mengine.


Jingine mh Mbuge hapo darajani nyang'homago wananchi wa hapo Huwa wanaichimba barabara wakitafuta mawe ya dhahabu kutoka mgodini yaani Yale yaliyosombwa na kuletwa kipindi Cha nyuma na wazungu kipindi wakiitengeneza wao.

Naomba iwekwe Sheria na katazo Kali Kwa wananchi wa pale maana hao wanasababisha barabara kumomonyoka Kwa Kasi sana.

Kama Kuna yaliyo sahaulika naombeni Wana msalala(Nyang'hwale) myaandike hapo chini.

Mbuge au wasidizi wake wampe taarifa Najua

Mheshimiwa Mbuge wa Jimbo la Msalala Idd kassumu Iddi utampa habari hizi Mbuge jirani Yako kabisa maana mnapakana pale No9 karibu na mgodi wa Bulyanhulu.

Yangu ni hayo Ni Mimi MwanaNchi mzarendo. Ahsantee.

Zifaatazo ni picha za barabara ninalo litolekero hapa.
Nilipiga nikiwa na kwenye boda boda

Ni sehemu tofauti tofauti za barabara ila ni hiyohiyo barabara.Na hapo mvua haijanyesha ilikuwa na siku3 bila mvua



Moderator naomba kero yangu hii ipelekwe na kwenye kurasa Zenu za mitandao ya kijamii kama Facebook,X na Instagram.






IMG_20240307_175350_6.jpg
IMG_20240307_175355_7.jpg
IMG_20240307_175341_4.jpg
IMG_20240307_175246_7.jpg
IMG_20240307_175208_433.jpg
IMG_20240307_175246_0.jpg
 
Back
Top Bottom