donniebrasco
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 887
- 775
MUNGU atakusaidia utapona,
Juhudi zako wote tuliziona,
Tumehuzunika sana kila kona,
Wabaya sasa aibu tu wanaona.
Ilikuwa tarehe saba septemba,
Wakapandisha risasi chemba,
Kwa ustadi kabisa wakalenga,
MUNGU akazipigisha chenga.
Mh umepigwa nyingi risasi,
Hatuna haja ya kulipa kisasi,
Tunaamini MUNGU yu nasi,
Ukirejea ongeza sana kasi.
Nikifikiria ulivyoumia sana nalia,
Wanajaribu amani kutuchafulia,
Ili baadae wapate kutusingizia,
Hongera wananchi kwa kutulia.
Wachache bado wanatughasi,
Mara wana gari mara farasi,
Wanatuchunguza kwa kasi,
Wanataka eti za juu nafasi.
Hakuna watu wasiojulikana,
Siku ifikapo tutatambuana,
Wenyewe tu wataumbuana,
Haitowaacha kabisa hii laana.
Naamini kwenye pipoz pawa,
Uchaguzi ukifika watapagawa,
Sala na subira kwetu ni dawa,
Wameshachoka kabisa hawa.
Umejaa busara na ukweli,
Kwao hivyo kabisa vimefeli,
Wamejaa dharau na kejeli,
Wanaahidi ahidi tu hata meli.
Matatizo ya kweli wanayaogopa,
Hawataki JEMBE wala KOPA,
Kwa siri nje wanaenda kukopa,
Bora waanze kuimba kama Kopa.
Madiwani wameanza wanunua,
MUNGU haachi tu kuwaumbua,
Inaonesha jinsi mnavyosumbua,
Wanatamani chama chetu kukiua,
Tunaombea iimarike yako hali,
Na ukirudi usife moyo tafadhali,
Tuko pamoja nawe na tunasali,
Wao waendelee tu kudhulumu mali.
Wabaya walitamani tukuzike,
MUNGU anakuandaa ili uimarike,
Tukiomba wanatumana watushike,
Ukishapona wao wanung'unike.
Aliyekuchaguwa ni MUWEZA,
Binaadamu katu hatokuweza,
Hawajui kiakili unavyocheza,
Kama kompyuta kwenye meza.
Tunakusubiri sana kwa hamu,
Tunaombea uje ushike hatamu,
Wewe ni ndugu yetu wa damu,
Wote, si wakristo si waislamu.
Juhudi zako wote tuliziona,
Tumehuzunika sana kila kona,
Wabaya sasa aibu tu wanaona.
Ilikuwa tarehe saba septemba,
Wakapandisha risasi chemba,
Kwa ustadi kabisa wakalenga,
MUNGU akazipigisha chenga.
Mh umepigwa nyingi risasi,
Hatuna haja ya kulipa kisasi,
Tunaamini MUNGU yu nasi,
Ukirejea ongeza sana kasi.
Nikifikiria ulivyoumia sana nalia,
Wanajaribu amani kutuchafulia,
Ili baadae wapate kutusingizia,
Hongera wananchi kwa kutulia.
Wachache bado wanatughasi,
Mara wana gari mara farasi,
Wanatuchunguza kwa kasi,
Wanataka eti za juu nafasi.
Hakuna watu wasiojulikana,
Siku ifikapo tutatambuana,
Wenyewe tu wataumbuana,
Haitowaacha kabisa hii laana.
Naamini kwenye pipoz pawa,
Uchaguzi ukifika watapagawa,
Sala na subira kwetu ni dawa,
Wameshachoka kabisa hawa.
Umejaa busara na ukweli,
Kwao hivyo kabisa vimefeli,
Wamejaa dharau na kejeli,
Wanaahidi ahidi tu hata meli.
Matatizo ya kweli wanayaogopa,
Hawataki JEMBE wala KOPA,
Kwa siri nje wanaenda kukopa,
Bora waanze kuimba kama Kopa.
Madiwani wameanza wanunua,
MUNGU haachi tu kuwaumbua,
Inaonesha jinsi mnavyosumbua,
Wanatamani chama chetu kukiua,
Tunaombea iimarike yako hali,
Na ukirudi usife moyo tafadhali,
Tuko pamoja nawe na tunasali,
Wao waendelee tu kudhulumu mali.
Wabaya walitamani tukuzike,
MUNGU anakuandaa ili uimarike,
Tukiomba wanatumana watushike,
Ukishapona wao wanung'unike.
Aliyekuchaguwa ni MUWEZA,
Binaadamu katu hatokuweza,
Hawajui kiakili unavyocheza,
Kama kompyuta kwenye meza.
Tunakusubiri sana kwa hamu,
Tunaombea uje ushike hatamu,
Wewe ni ndugu yetu wa damu,
Wote, si wakristo si waislamu.