Hongera sana Mh. Godbless Jonathan Lema Mbunge wangu, nakumbuka wakati tuko katika harakati za ukombozi wa jimbo letu kutoka mikononi mwa CCM, uliwahi kutuambia kwamba wewe utakuwa mbele yetu, na sisi tuwe nyuma yako tusikuanguashe. kwa hili tumeshuhudia kweli uko mbele yetu na sisi tuko nyuma yako.
katika nchi hii sijawahi kuona kiongozi anapigwa na polisi kwa ajili ya kutetea maslahi ya wananchi wake, wewe umekuwa kioo, ulipigwa na polisi, ukawekwa ndani, ukadhihakiwa sana, lakini hukukata tamaa.
Mh. Lema wewe ni mzalendo wa kweli wa nchi hii, tunakutakia mema siku zote, tunakuombea mungu aendelee kukupa ujasiri ututetea watanzania wote tunakuhitaji.
Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Chadema
Mungu mbariki Godbless Lema.