Kwako Kaka yangu Jamal Emily Malinzi

Kwako Kaka yangu Jamal Emily Malinzi

Eddie

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2008
Posts
516
Reaction score
127
Salam kwako Kaka,

Niruhusu nikutumie ujumbe kupitia jukwaa kwani sina namna nyingine ya kuwasiliana na wewe.

Niende kwenye maudhui ya waraka huu. Shirikisho la soka la dunia FIFA limetoa maelekezo ya kuanza upya kwa mchakato wa uchaguzi wa TFF.

Tokea awali sikuwa na imani na President Tenga kwa namna alivyo hodhi na kuendesha mchakato ule kwa kutumia remote control huku yeye akiwa mbaali as if hahusiki. Hadithi ni ndefu na wewe waijua vizuri lakini kuifanya fupi ni kuwa Tenga kwa kushirikiana na FIFA wamekupiga bao la kisigino kwenye tamko lao, kwa nini nasema hivyo;

1. Kimsingi TFF kwa kushirikiana na FIFA wataka uchaguzi uanze upya kwa maana ya kuanzia ngazi ya mkoa, hii imefanywa kwa makusudi kwa kuwa wanajua viongozi wa mikoa mingi wa sasa wanakuunga mkono wewe na uliwekeza sana kwenye chaguzi za mikoa.

2. Tenga anataka sana kugombea tena lakini kwa kuwa hakujiandaa mikoanii alishanusu harufu ya kushindwa vibaya, hivyo basi tarajia kwenye mchakato mpya huu Tenga ataweka watu wake mikoani na kuna uwezekano mkubwa wa yeye kugombea tena.

3. Kama hatagombei atahakikisha kibaraka wake Athumani Nyamlani anajiimarisha kwenye chaguzi za mikoani ili kujipanga.

4. Kaka kuelekea mchakato mpya wa uchaguzi kaa chini na Michael Wambura na Ramdhani Nasseb mkubaliane juu ya makamu wa rais, msiruhusu kugawanyika.

Nina nina mengi lakini kwa leo naomba niishe hapo
 
Naamini muhusika ameshasoma na kukuelewa ila hawezi kuongea chochote hapa kutokana na miiko ya kiungozi japo hilo wanalijua wenye busara tu, binafsi natamani Malinzi au Wambura mmoja wao ashinde urais ili tuone ni kweli hawafai au fitina tu? Mara nyingi wapenda mabadiriko wa kweli huwa wanapigwa vita na watawala.
 
Eddie
Nakuomba uwe na amani.
TFF kupitia kamati ya rufaa ya uchaguzi iliongea tukaisikia.
Serikali kupitia tamko la wizara yenye dhamana ya michezo iliongea tukaisikia.
Jana kupitia ujumbe wa Bw. Tenga FIFA imeongea tumeisikia.
Alhamisi tar 09/05/2013 kamati ya utendaji ya TFF itakaa tutaisikia.
Inshallah tuombeane kheri,bora uzima.
 
Last edited by a moderator:

Sikuwahi kujua kama TFF kuzuri hivi!ni kweli kwa mapenzi ya soka na maendeleo yake au maslahi binafsi?mnatoka mapovu wewe Malinzi na Wambura!sidhani kama ni mapenzi ya soka!na hivi hakuna muingiliano wa kiutendaji kati ya Rais na TFF na BMT?...nahisi TFF ni daraja la ubunge labda!
 
Last edited by a moderator:
eddie
nakuomba uwe na amani.
Tff kupitia kamati ya rufaa ya uchaguzi iliongea tukaisikia.
Serikali kupitia tamko la wizara yenye dhamana ya michezo iliongea tukaisikia.
Jana kupitia ujumbe wa bw. Tenga fifa imeongea tumeisikia.
Alhamisi tar 09/05/2013 kamati ya utendaji ya tff itakaa tutaisikia.
Inshallah tuombeane kheri,bora uzima.
jamal unjibishana na kina nyamlan athman smahan nimechelewa nilitaka kukwambia usimjibu chochote wanahisi majibu yako yatawapa mwongozo nini cha kkufanya shame n them hii ni nidhamu ya uwoga tu waendelee kujiandaa kama walivyotaka kufanya mmchezo wao mchafu mungu akaingilia kati
 
Last edited by a moderator:
Malinzi akishinda uraisi TFF Yanga tumeumia

pole sana yuko Manji pale juu na kama unajua tff aitaongoza ligi tunaenda kuleeee mtaa wa mafia ndio tutaongoza ligi
 
Sikuwahi kujua kama TFF kuzuri hivi!ni kweli kwa mapenzi ya soka na maendeleo yake au maslahi binafsi?mnatoka mapovu wewe Malinzi na Wambura!sidhani kama ni mapenzi ya soka!na hivi hakuna muingiliano wa kiutendaji kati ya Rais na TFF na BMT?...nahisi TFF ni daraja la ubunge labda!

Hata mchakato ukianza upya nakuhakikishia Malinzi na Wambura hawatapita on technicalities ambazo wao na wapambe wao kwa vile ni mbumbumbu hawajazigundua!!
 
Simtetei mgombea yoyote wala sisemi Tenga hana kasoro yoyote au kilichosemwa si sahihi au la.Ila ukweli ni huu;Cheo kinachotafutwa kwa kununua waandishi na media houses zote,kuloby hadi Naibu Waziri,kutetewa na Kaka kwa kisingizio cha Uenyekiti wa BMT,kununua kwa hila viongozi wa Mikoa hakutatuletea RAIS MWADILIFU na ndio anguko letu litapoanza.Angalieni alikotoka huyo mnayemshabikia sana.
 
tatizo njaa na uroho wa madaraka na kikubwa zaidi kuzuia mtu mwengine asijue uchafu wako ndio maana kaka Jamal Malinzi na kina wambura wanatoswa kama mtu ni msafi kwanini ubague watu fikiri sana juu ya hili..
 
Last edited by a moderator:
Eddie
Nakuomba uwe na amani.
TFF kupitia kamati ya rufaa ya uchaguzi iliongea tukaisikia.
Serikali kupitia tamko la wizara yenye dhamana ya michezo iliongea tukaisikia.
Jana kupitia ujumbe wa Bw. Tenga FIFA imeongea tumeisikia.
Alhamisi tar 09/05/2013 kamati ya utendaji ya TFF itakaa tutaisikia.
Inshallah tuombeane kheri,bora uzima.

chonde chonde mkuu yaani kama utabahatika kupata urais ukileta mambo ya kisasi soka la bongo litakufa amini hilo..
 
Last edited by a moderator:
Sikuwahi kujua kama TFF kuzuri hivi!ni kweli kwa mapenzi ya soka na maendeleo yake au maslahi binafsi?mnatoka mapovu wewe Malinzi na Wambura!sidhani kama ni mapenzi ya soka!na hivi hakuna muingiliano wa kiutendaji kati ya Rais na TFF na BMT?...nahisi TFF ni daraja la ubunge labda!

Hatuwezi kujua kama wanatoka povu kwa maslahi yao au la. Tuwape nafasi kwa kuwatendea haki katika nchi yao Tanganyika.
 
Sikuwahi kujua kama TFF kuzuri hivi!ni kweli kwa mapenzi ya soka na maendeleo yake au maslahi binafsi?mnatoka mapovu wewe Malinzi na Wambura!sidhani kama ni mapenzi ya soka!na hivi hakuna muingiliano wa kiutendaji kati ya Rais na TFF na BMT?...nahisi TFF ni daraja la ubunge labda!

oversimplification at its best!
Hivi nchini mwetu kila jambo lazima tulihusishe na political ambition? Lambardi hivi ushawahi kusikia Jamal anagombea hata uongozi wa mtaa?
usiusemee moyo ( source: jide)
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom