Ninajivunia kuwa na kiongozi kama wewe.
Lakini naogopa ninapoona umekaa kimya tena mara nyingine unahudhuria mialiko isiyofaa.
Nini kinakusibu hata uogope kulikemea pepo pale magogoni!
Hamkupewa nyinyi jina la Yesu kuyakemea mapepo?
FUNGUA KINYWA UWASEMEE MABUBU.
TAIFA LINAANGAMIA MKITIZAMA.
Senti moja moja zimechangwa kujenga madhabahu, zitumieni hizo madhabahu kumlilia MUNGU aliye hai kwa ajili ya wajoli wake wanaosetwa.
UJUMBE MFUPI TOKA KWA ALIE JUU.
Ewe kiumbe dhaifu, nimekisikia kilio chako pamoja na vilio vya mamilioni ya wenzio tokea niwape hii nchi (TZ) toka kwa wakoloni.
AWAMU YA 1.
- Niliwawekea Nyerere kama chaguo langu lakini mlimdharau kwa kumuita Mchonga, Haambiliki, na majina mengi ya kejeli. Nyerere nilimuwekea roho ya imani na ya kusamehe. Leo hii ninae hapa tunawaangalia tu.
AWAMU YA 2.
- Niliona labda ni vema mjaribu siasa za kinyang'anyiro. Hivyo nikawawekea kiongozi mstaarab toka visiwani ili awasaidie kusonga mbele na ulafi wenu. Wengi mlifurahia utawala ule na kumuita mteule wangu mzee Rukhsa. Kwa upole wake Ikulu takatifu mkaigeuza danguro la ulanguzi na ufuksa. Kiongozi huyu alipiga kelele weeee, lakini kwa upole wake mkamzidi nguvu. Sikutaka kuingilia kati kwa sababu mlikuwa mnajifunza.
AWAMU YA 3.
- Nikaona niwawekee mtu mkali kidogo lakini mwenye diplomasia na mwana habari. Nilitegemea mtamuelewa kutokana na kipaji chake cha kujieleza na diplomasia. Tatizo lilikuwa ni wapambe wake waliojikita na mizizi mirefu iliyokuwa inafyonza kila kitu toka serikalini. Hali ilikuwa mbaya mpaka kushutumiwa kuwa Ikulu imekuwa stock exchange ya kwanza nchini. Lakini nilifarijika kuona upinzani umeshamiri na wameanza kuyakemea maovu ya serikali.
AWAMU YA 4.
- Baada ya awamu ya 3 ilibaki kidogo tu niamue kuwapa wapinzani nafasi nao wajaribu. Lakini niliwaona bado kidogo, wapinzani walikuwa hawajakomaa vya kutosha. Basi ile awamu ya 4 nikaamua nimuweke kijana hodari niliemuandaa kwa muda mrefu sana. Ni mcheshi, ana diplomasia, ana uwezo mkubwa kiuongozi, yani kwa kifupi ni kama yule wa awamu ya 3 lakini ni kijana zaidi na mcheshi zaidi. Nilijua huyu ataiunganisha nchi. Kweli alikuwa mcheshi na alikua kiungo kizuri sana kati ya TZ na ulimwengu mzima.
Eti wapinzani walimuita dhaifu! Lakini kijana huyu hakuwa na hiyana, aliwakaribisha chai Ikulu hawa hawa waliokuwa wanamtusi na kumkejeli.
Kwa kuwa kiongozi huyu alikuwa ni mtu wa watu na alikuwa na marafiki wengi nchini, alishindwa kuwakemea maswahiba wake pale walipojihusisha na wizi uliokithiri. Mambo hayakuwa shwari katika uongozi wake hasa kufuatia kelele za wapinzani.
AWAMU YA 5.
- Ni katika kipindi hiki cha awamu ya 4 ndipo nilipoamua kuwa sasa CCM basi. Ifikapo awamu ya 5 itabidi niwapokonye uongozi hawa CCM ili kwanza, waote kijua cha kijiweni (upinzani), na pili niweke hodari mmoja toka upinzani aliekereketwa vya kutosha. Nilikuwa namfikiria Slaa. Ingawaje Slaa alinisaliti kwa kuacha kuchunga kondoo wangu (kanisa) na kuingia siasa lakini niliona labda anaweza kufanya hiki kitubio (atonement) cha kuuboresha uongozi wa nchi hii.
Wapinzani walinichosha walipoamua kumuweka mmoja wa vinara waliokuwa wanaharibu vitu kwenye awamu za huko nyuma. Hapa TZ walinikasirisha sana.
Niliwapa nafasi nyingi mjirekebishe lakini hamkujirekebisha. Nikaamua kuwa sasa itabidi nimshike mkono huyo mtawala wa awamu ya 5 na nimuelekeze cha kufanya na pa kupita kona hadi kona mpaka mwisho.
Magufuli ni mteule wangu na anatekeleza maagizo yangu ili kuiokoa hii nchi taajiri duniani lakini yenye watu ombaomba na masikini wa kutupa.
AGIZO LANGU KWENU LITATIMIA.
[Kifyatu ametumwa tu. Mjumbe hauawi]