Kajolijo
JF-Expert Member
- May 30, 2016
- 3,364
- 4,612
Zitto kwa hili nasema toka moyoni sasa naamini we si mpinzani wa kweli, haiwezekani wewe kama kiongozi mkuu wa chama ukakubaliana na hili, kama kweli una nia ya dhati kwanini unamuweka Mgombea alieshindwa ubunge huko Kibondo mhambwe kuja kugombea udiwani huko mbagala kijichi, leo katika pita pita zangu nmekutana na watu wanasema kua lengo lako ni kufelisha chama, eti mgombea Ediger mkosamali aligombea ubunge tena alikuwa hakubariki, ana uroho wa madaraka, kwnz aligombea ubunge 2015 kwenye kura za maoni akashndwa akakimbilia ACT ambapo napo aliboronga akapigwa chini sasa inakuaje umpe nafasi agombee udiwani huko kijichi? Kuna kitu gani kimejificha, kama alishndwa kibondo ataweza hapa, kwanini anatafuta madaraka kwa nguvu, mbona unaleta ukabila, kwani hamna wengine ambao ni 'cream' yaani hawana makando kando wa hapohapo kijichi? Unadhani watakuwa tayari kumchagua mtu alieshindwa sehem nyingine wakati ungewawekea wa kwao wangempa. Kiukweli nilivosikia haya maneno nikasema ngoja nilete wanajamvi muuchambue muone kama kweli hapa kuna upinzani wa kweli.
