Uchaguzi 2020 Nini mkakati wa CHADEMA na ACT-Wazalendo kulinda ushindi katika vituo vya kupigia kura?

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
CCM wako "so desperate" kuhakikisha kuwa mgombea Urais wao John Pombe Magufuli anatetea kiti chake.

CCM wanatambua fika kuwa, kupitia sanduku la kura (Ballot Box), Magufuli hawezi kushinda iwe mvua ama jua.

Wanataka ashinde kwa "njia zingine haramu" ambazo Mimi na wewe msomaji tunazijua na zimefungashwa kwenye maneno haya mawili tu "WIZI WA KURA" Huu ndiyo msingi wa hoja hii. Na wanadhani kuwa, mbinu hii ni ya uhakika kwao!

Ni KWELI na HAKIKA mkakati wa kulifanikisha hili upo. Ni mkakati kabambe, unaotumia FEDHA NYINGI SANA na unaendelea nchi nzima sasa kuhakikisha kuwa MEZA INAPINDULIWA ili mradi Magufuli apate ushindi wowote. Bado hawana uhakika wa asilimia, lakini kwao NI LAZIMA ASHINDE!

Kila mtu anajua na kutambua kuwa wengi wa maafisa wa serikali kama vile maDC, maRC, DEDs, WEOs ndiyo viongozi na makada wa kufa wa CCM.

DEDs and WEOs ndiyo wanaofanya kazi ya Tume ya uchaguzi (NEC) kama wasimamizi katika ngazi ya jimbo (Urais & Ubunge) na kata (udiwani).

NINI KINAFANYIKA KWA SASA?
Kama nilivyoanza kuandika hapo juu, upo mkakati kabambe unaendelea sasa kuihakikishia CCM ushindi kwa kuwatumia hawa maofisa wa serikali ambao wakati huohuo wengi wao wakiwa ni makada watiifu wa CCM.

Sambamba nao, wanapata "back up" ya nguvu na ya kutosha kutoka kwa baadhi ya maafisa wa Idara ya usalama wa taifa ( TISS) na Polisi kuandaa mikakati ya wizi wa kura kumshindisha Magufuli, wabunge na madiwani wake.

Wizi utafanyikia katika ngazi ya VITUO VYA KUPIGIA KURA. Zoezi linaloendelea nchi nzima kwa sasa ni kufanya "recruitment" ya wasimamizi wakuu na wasaidizi wao katika ngazi ya vituo vya kupigia kura.

Nina hakika kila mtu kwenye magrupu yenu ya FB, Instagram, WhatsApp nk mmeona matangazi ya kazi ya usimamizi wa uchaguzi toka ktk majimbo yote yanatembea huko.

Asiwadanganye mtu, matangazo hayo ni "bosheni" tu, ila ukweli ni kuwa tayari walishawateua wasimamizi tayari na kila DED ama CCD anao mezani kwake. Kama wewe hujaitwa "privately" aidha kwa kufuatwa ama kupigiwa simu, unajisumbua tu kuomba hizo kazi.

Kwa 95%, wanawatumia wafanyakazi wa umma i.e teachers, nurses, watendaji wa vijiji, madaktari, mabwana na mabibi shamba nk.

Kilichofanyika ni hiki:

1. Cha kwanza, huyu MAGUFULI POMBE "anafikiri" kuwa atashinda tu uchaguzi huu na ataendelea kuwa Rais.

2. Kwa kudhani kuwa ataendelea kuwa Rais tu (2020 - 2025), ametoa "ULTIMATUM" kuwa DED yeyote ambaye jimbo lake atashinda mpinzani, ATAFUKUZWA KAZI!

3. DEDs nao wanaweka wafanyakazi walio chini yao kuwa wasimamizi wa uchaguzi ktk vituo vyote. Na wao wametoa "ULTIMATUM" kwa maWEO kuwa, yeyote ambaye kata yake atashinda mpinzani ATAFUKUZWA KAZI!

4. WEOs wote wamekasimiwa madaraka ya kuteua WASIMAMIZI WA UCHAGUZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA kutoka miongoni mwa walimu, manesi nk walioko katika kata zao. Nao wamewapa ULTIMUTUM watumishi hawa kuwa, kwenye kituo chake atakachosimamia ikitokea mgombea wa upinzani ameongoza kura, msimamizi wa kituo husika, ATAFUKUZWA KAZI!

MAANA YAKE NINI?

å Hawa watumishi ndiyo wataipa ushindi tena CCM mwaka huu 2020 kwa "KUPINDUA MEZA".

å Kitisho cha KUFUKUZWA KAZI kimewatisha.

Mimi nimetoa taarifa. CHADEMA na ACT WAZALENDO kazi iko hapo. Kama mtaweza kudhibiti hili, CCM TUTAIZIKA CCM MWAKA HUU 2020!

MIMI NIKO KWENYE KAMATI HII. WANADHANI MIMI NI MWENZAO.

Nimetimiza UZALENDO WANGU.
 
Hali ni tete, ugumu upo hapa,, ila ya Mungu mengi bhnaa, upinzani tuna Jambo letu na lazima litimie hapo October 28. Tuwe na subira tu
 
Huwa Shida inakuja kwamba upinzani uliopo mjini haupo vijijini. Napengine huko vijijini hata kupata tu mawakala kwenye vituo vya kupigia Kura sio rahisi na hata wakiwepo mawakala sio competent.

Upinzani ujitahidi kwenda vijijini kutengeneza mazingira mazuri. Lakini pia hilo lamaelekezo kwa wasimamizi sidhani Kama lipo, Kama unamawakala wa Chaka wenye ubora kwenye kila kituo hakuna Shida ila Kama wakuokoteza tu Shida inaanzia hapo.
 
CCM wako "so desperate" kuhakikisha kuwa mgombea Urais wao John Pombe Magufuli anatetea kiti chake...
Duuh.. siku zote kuondoa mkoloni kazi yake pevu.

Pia, ccm walikuwaga na mfumo wa kuwa na vituo vya kura "hewa" ambavyo kazi yake ni kuwasilisha masanduku ya kura yaliyojazwa kura hewa za ccm pekee ili kuongeza idadi ya kura zao.. Kwa sasa hakuna hivyo vituo?
 
Huna lolote unalolijua, vituo vipo zaidi ya 80000 na vyote mawakala wa CCM wote watakuwa special force in civilian clothes waliokunywa maji ya bendera,wamechujwa zaidi ya miaka mitatu. Na wamelishwa kiapo maalum. Hao wakurugenzi kazi yao ni ya baadae sana kutangaza matokeo na kuya forward. Mwaka huu mawakala wa upinzani watapigwa ngwara za kutosha, na wengi wataondolewa vituoni kwa nguvu. Nyie mmejazana mitandaoni mnajipa moyo kumpamba Lissu.

Hata bila hivyo JPM anashinda tu Ila kutokana na kelele zenu CCM inajihakikishia ili zisipungue 85%(Mark my words), ni kama mtu anauefaulu hesabu anapataga 90% O level nzima Ila ukikaribia mtihani wa taifa anasaka feki kabla ili kujihakikishia 95%
Nyie badala ya kudili na vitu vya maana, mmejazana Jamii Forums kuanzisha threads za kupeana moyo.

Tukiwaambia Tundu Lissu hawezi kuwa Raisi wa nchi hii tunajua mengi. Narudia tena ni rahisi Steve Nyerere kuwa Waziri mkuu kuliko Tundu Lissu kuwa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, bado siku 36 tu mpate matokeo ya ninayosema.

Siku moja huko miaka ya baadae CCM itaondolewa madarakani, Ila ni mpaka utakapopatikana upinzani wenye kuishawishi system kwamba angalau ni 50-50 au 48-52 au hata 40-60(%) kimfumo wa vyama, Ila hizi za kuokoteza wagombea eti kisa alipigwa risasi, hajui aongee nini,lini na wapi?. Bado CCM ipo miaka mingi mbele.
 
Hawana kingine cha kufanya zaidi ya kuiba. Alivyojitengenezea maadui, akifikiria kuwa raia, tumbo la kuhara linaanza usiku mkubwa!
 
Kila kitu kimedhibitiwa , kulikuwa na mipango ya tume kuapisha mawakala feki wa Chadema ili wasaidie kusaini matokeo ya uongo , lakini watu wetu ndani ya tume wamefichua
 
Kila kitu kimedhibitiwa , kulikuwa na mipango ya tume kuapisha mawakala feki wa Chadema ili wasaidie kusaini matokeo ya uongo , lakini watu wetu ndani ya tume wamefichua
Wewe jamaa nadhani unaongoza kujipa matumaini Afrika mashariki, Kati na kusini mwa jangwa la Sahara. Serikali na nchi kwa ujumla unaichukuliaga poa kama mtaa wa ufipa ukiunganisha na maeneo ya manyanya Kinondoni.
 
Kwa mawakala wetu wanaotaka kuondoa utata wa kura fake kwenye vituo wanazo njia mbili zakufuata kabla yakusaini karatasi za matokeo.

1. Kuhesabu kura zote zilizopigwa kwenye kituo utapata idadi ya wapiga kura

2. Baada yakupata idadi ya kura za kituo kwa diwani, mbunge na Rais, waombe msimamizi kuwapa vitabu vyote vilivyotumika, vitabu hivi vinabaki na vishina vyene kakaratasi ambako kana namba za wapiga kura. Walinganishe idadi ya vishina na idadi ya karatasi zilizopp kwenye sanduku la kura. Zikitofautiana kuna kosa la kiufundi.
 
Back
Top Bottom