kwaherini malenga JF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kwaherini malenga JF

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Barubaru, Feb 21, 2012.

 1. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Buriani Barubaru.

  1. Anayeifanya njia, usipate angamizi.
  Anayekupa bamia, njaa inapokujia,
  Ndio wa kumwaminia, kwa asilimia mia,
  Buriani barubaru, Kwa herini JF.

  2 Hewa bila kubabia,Wavuta na yabakia,
  Tena bila kupapia, Taratibu yaingia,
  Ni bure uja lipia, wala si bili sikia,
  Buriani barubaru, Kwa herini JF.

  3 Unaye mwomba mia, maelfu akwachia,
  Dola na hata rupia,Riyali kwa kuwania,
  Ndie pekee jalia, wengi ninawaambia
  Buriani barubaru, Kwa herini JF.

  4 Uwapo na malaria, Pengine ni almonia,
  kwikwi vidonda kuvia, yeye ukimlilia,
  Huukomesha udhia, Mola akakushindia,
  Buriani barubaru, Kwa herini JF.

  5 Kesi za kusingiziwa, walizonibambikia,
  Wakanitia hatia, kusema kwa jumuiya,
  Hufai kwa umma huu, siku mbili mahuria.
  Buriani barubaru, Kwa herini JF.

  6 Nawapongeza kwa dhati, wote mliopigania,
  Mwanakijiji,Choveti, Maranya na fauzia,
  Ritz bado sijaketi, Rejeo zomba na Paw,
  Buriani barubaru, Kwa herini JF.

  .

  7 Wote Ninawashukuru , wanachama JF,
  Nisije fanya kufuru,Mods kuwaongezea.
  Mke wangu l'afuru, na watoto wangu pia
  Buriani barubaru, Kwa herini JF.


  8. Tamati ndio akhifu, jina langu maarufu.
  Hamza wa Yousuf, Naamaniy ni sharafu,
  Mkurugenzi sarafu, Qatar kwenye mafuta.
  Buriani barubaru, Kwa herini JF.


  Dr Hamza Yousuf Al Naamaniy (Barubaru)
  Director of Finance & Admin
  Qatar petrolium.
  +974 4457 4888.
  Doha. Qatar

  mapumzikoni ,
  Hesawa, mwanza.
  Local number 255 684 221 077 mpaka 24 feb 12

   
 2. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4,094
  Likes Received: 1,268
  Trophy Points: 280
  kwann waondoka..bila sababu kutupatia
  wengi tulipenda michango,uliyochangia
  hakika siwezi kukuzuia,kwaheri nakutakia
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Barubaru msalimie bujibuji
   
 4. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mkuu,.............. subiri kidogo usilog off, ....................naku PM now!....................
   
 5. Y

  Yakuonea JF-Expert Member

  #5
  Feb 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 601
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  FANYA URUDI KUNDINI

  Beti nina zianzia, kwa jina lake manani
  Mola wa hii dunia, na vyote vilivyo ndani
  Kaumba na Mbingu pia, hana yeye mshindani
  NI WAPI WAKIMBILIA, FANYA URUDI KUNDINI

  Dunia ni mitihani, Mola ametwambia
  kila siku tuvitani, si vyema ukakimbia
  Hebu rudi humu ndani, uanze na kuchangia
  NI WAPI WAKIMBILIA, FANYA URUDI KUNDINI

  Ni lipi limekughasi, mpaka waondokea
  Au umepigwa tusi, na kesi walokugea?
  Tueleze wacha wasi, kwa nini watokomea
  NI WAPI WAKIMBILIA, FANYA URUDI KUNDINI

  Kwa jamvi kuliachia, siafiki ninakana
  Hakuna kunyamazia, bora hata kupigana
  Yu wapi na fauzia, mngefanya kuungana
  NI WAPI WAKIMBILIA, FANYA URUDI KUNDINI

  Sindano Mwana wa Ganzi(SMG)
  Kijijini Tongoleani
   
 6. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #6
  Feb 21, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Rudi mapema Mkubwa!

  Michango yako ni muhimu sana humu!
  Mapumziko Mema Mkubwa!
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Baada ya kufikiri
  na nena umekiri
  wapajua Ikwiriri
  seuse kirikiri
  ukweli si mshari
  kutuacha twakariri
  Baada ya kufikiri
  na nena umekiri

  Barubaru Mzanzibari
  kwao atakabari
  si shari kukukariri
  kujifanya mshairi
  umepanda manuwari
  kuja kwetu kuhariri
  Baada ya kufikiri
  na nena umekiri

  Nimenuna nafikiri
  ni nini kilojiri
  wala sio mhariri
  ukweli wausitiri
  nakuomba we jabari
  uwache kutakabari
  Baada ya kufikiri
  na nena umekiri

  Usende kwa kiburi
  baki ulete habari
  si wengi walo jiri
  kufikia kuwa wari
  wao hawasitiri
  huanza kwa ushari
  Baada ya kufikiri
  na nena umekiri

  Usiwape tafakari
  yao ni masaburi
  ukienda kwa hiari
  wataacha kufikiri
  wala hilo sio siri
  wao wana jiajiri
  Baada ya kufikiri
  na nena umekiri

  Max amekiri
  kuwa yeye si mshari
  amerudi safari
  akakuta wavinjari
  wamejitia kabari
  FaizaFoxy kumtairi
  Baada ya kufikiri
  na nena umekiri

  MS kwa kabari
  Ritz kwa mahubiri
  Mike kasitiri
  Kwa kujifanya mshari
  tusianze kuhubiri
  kujitia uhodari
  Baada ya kufikiri
  na nena umekiri

  Barubaru sio siri
  wewe ni jabari
  ulishinda kule Suri
  na pia kule Qatari
  Barubaru tafakari
  watuachia hatari
  Baada ya kufikiri
  na nena umekiri


  Mimi sio nguri
  ujabari si u kiri
  nakuomba tafakari
  watuacha kwenye shari
  baki utusitiri
  kwa usomi ulojiri
  Baada ya kufikiri
  na nena umekiri

  Kidogo walo kariri
  uyajuayo dhahiri
  waachia kisirisiri
  tujuao twakariri
  wewe umahiri
  kwako ni bahari
  Baada ya kufikiri
  na nena umekiri

  Hawajibu zao shari
  hawana lilojiri
  ukweli ukidhihiri
  uongo huwa shari
  nakuomba jabari
  baki ukifikiri
  Baada ya kufikiri
  na nena umekiri
   
 8. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  duh!!...................... ngoja na mimi nkajipange, ................narudi na vina timamu soon ...................
   
 9. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Jamaa kaaga kweli au anabip?
   
 10. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #10
  Feb 22, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,130
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  ndo kaaga huyu.
   
 11. C

  Choveki JF-Expert Member

  #11
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Usiondoke jamvini


  Vuta subira wakwetu, ujumbe nimesikia
  Nakataa katu katu, jamvini kuondokea
  Usikimbie msitu, ni wapi wakimbilia?
  Usiondoke jamvini, ni wengi twakuambia

  Muungwana ni vitendo, na vyako vimeoneka
  Nasema siende kando, jamvini tunakutaka
  Tunautaka uhondo, wa kwako uso kauka
  Usiondoke Jamvini, ni wengi twakuambia

  Barubaru wenda wapi, nasema tutapooza
  Turudie mara ngapi, ujuwe unaongoza?
  Hoja zako si makapi, kwa mema zinaongoza
  Usiondoke Jamvini, ni wengi twakuambia!

  Mitihani ndiyo hiyo, nasema nawe ujuwe
  Na tena yataka moyo, kwa hao wenye viwewe
  Twajuwa siyo mchoyo, na tena huli mwenyewe
  Usiondoke Jamvini, ni wengi twakuambia

  Kaditama wa tamati, siende kaka siende
  Utujulishe umati, tusherehe tule tende
  Halua navyo visheti, tuvitafune vipande
  Usiondoke Jamvini, ni wengi twakuambia
   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Apr 12, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  JF wanaoondoka hawaagi, wanaoaga hawaondoki.
   
Loading...