Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 30,812
- 59,392
Inatokea wakati mwingine watu wawili wanakutana mmoja au wote wawili wakiwa kwenye mahusiano na watu wengine na bado kila mmoja anaishia kuvutiwa na mwenzie hata kufikia hatua ya "KUTAKA" kuwa pamoja.
Wanapofikia hatua hiyo yule mwenye mahusiano anaweza akatoa offer ya "Ntamwacha nilie nae/nataka nimwache nilie nae ili mimi na wewe tuwe katika mahusiano". Kwa namna moja huu naweza kuuita ustaarabu kwasababu mhusika atakua mkweli kwa yule mwenzi wake kua mahusiano yao yamefikia tamati ili asonge mbele, which means hamna anaecheat. Ila sasa. . . .
Wewe binafsi unaonaje swala la mtu kumuacha mtu wake alokua nae "KWAAJILI YAKO"?!
Sio kwakua hampendi tena, sio kwakua hamtaki ila kwa kiasi kikubwa ni kwasababu wewe umejitokeza.
Binafsi hiyo "KWAAJILI YAKO" hua inanipa utata sana. Naona kama ni namna ya kuanzisha mahusiano ambayo ni complicated tangu mwanzo, maana hata siku akikuchoka anaweza asichelewe kukutupia dongo la " we ndo ulinifanya nikamwacha mpenzi wangu. . .and for what? Huna maana!" . Hapo mshachokana au complication zishakua nyingi. Nimefikiria njia ambayo ni bora kudeal na mtu ambae yupo kwenye mahusiano anayodai hayataki tena bali anataka kuwa nawe , huku nawe ukipenda kuwa nae ni kumtaka ajitoe kwenye situation aliyomo (current mahusiano) bila ya kukuhusisha wewe. Kwamba bila ya kujua kama utampokea au la, avunje hayo mahusiano anayodai hayataki tena alafu ndio arudi kutaka kujua kama unamtaka na kama uko tayari kumpokea au la.
That way atakua ameonyesha kwamba kweli yale mahusiano hakua anayataka/furahia bali alikua anaendelea nayo tu labda kwa kukosa ujasiri/msukumo wa kuyasitisha. Pia utakwepa lawama ya kuwa 'ulihusika' kuvunja mahusiano ya mwenzio.
What you all think. . . . ?