gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,305
- 3,327
Kadiri siku zinavyosonga mbele tunaona upinzani ukizidi kupoteza mvuto na imani kwa watanzania.Hii ni dalili mbaya sana japo waliowengi wanaziba pamba na kujitia moyo kwamba mambo yanaenda vizuri jambo ambalo si kweli.
Teuzi na maamuzi ya hovyo yanayo tolewa na viongozi wachache ndani ya chama ndio kiini cha huu mvurugano ndani ya CDM.
Jana tuliaminishwa kwamba ujio wa Lowasa umekijenga chama,hili si kweli bali ni changa la macho ambalo wanufaika wa ujio huu wa Lowasa wanajaribu kuupindisha ukweli ili waendelee kuaminika machoni pa wanachama.
Ukweli ni kwamba muunganiko wa vyama vya upinzani(UKAWA) ndio umeinusuru CDM na hata Lowasa kufanikiwa ushindi wa 40% kwani kura za vyama vya upinzani zilimuelekea lowasa peke yake.
Watu wanasema Dr Slaa 2010 alipata kura kwa 27% ambazo wao wanaziona ndogo ukilinganisha na 40% alizopata lowasa lakini wanasahau 2010 kila chama kilisimamisha mgombea wake hivyo ulinganishi huu wa Dr Slaa dhidi ya Lowasa ni batili.
Jana tumeshuhudia muendelezo wa maamuzi ya hovyo ambayo yataendelea kukigharimu chama kama ambavyo mwenye kashafa ya ufisadi (Lowasa) anavyoendelea kukigharimu sasa.
Kumchagua katibu mkuu kwakutizama ushupavu wake kwenye kusimamia vema mgomo wa madaktari,mgomo ambao ulisababisha vifo na mateso makubwa kwa watanzania si sawa.
Kwakufanya hivi tunaendelea kudumaza Upinzani kwani watanzania bado hawajasahau vifo na mateso makubwa walioyapata ndugu zetu.
Sijui ugumu upo wapi na tena sijui kwa maslahi ya nani kwani CDM imejaa hazina kubwa ya wanachama safi wasio na chembe ya mashaka machoni pa watanzania.
Kwa jinsi mambo yanavyoendelea ndani ya vyama vya upinzani ni dhahiri magufuli hahitaji kufanya kampeni 2020