Shukrani A. Ngonyani
JF-Expert Member
- Feb 23, 2014
- 1,182
- 2,015
Wakati Kikwete akiondoka madarakani kuna jamaa flani amewahi kuniambia mtamkumbuka sana Kikwete kwa kuruhusu uhuru wa habari.
Nikamjibu kuwa uhuru wa habari sio hisani yake, ni zao la katiba yetu inayoruhusu uhuru wa habari. Pia nikampasha kuwa Kikwete hajawa rafiki wa uhuru wa habari wala vyombo vya kupashia habari.
Nikamkumbusha kitendo cha kuzuia kwa muda usiojulikana gazeti la Mwanahalisi, kuzuia kwa mikutano ya kisiasa mkoani Mtwara na sheria mbovu ya mtandao.
Awamu ya tano imekuja na moto wa makaa ya mawe unaolenga aidha kuzima vyombo vya habari au kuzima kabisa uhuru wa maoni na habari.
Wakati rais Magufuli anaingia madarakani tumeshuhudia namna vyombo vya habari vilivyomnadi huku yeye akionesha namna asivyovipa umakini. Wakati anajibu maswali ya wanahabari siku ya kutangaza baraza la mawaziri alikuwa anajibu "kifalme" zaidi huku akijibu majibu ambayo hayaleti ustawi kwa muuliza maswali(waliofuatilia wananielewa).
Ndani ya muda mfupi pia tumeshuhudia waziri wa habari akilifuta gazeti la mawio, tena mshtaki akiwa huyo huyo aliyefungia, mpelelezi huyo huyo na hakimu huyo huyo aliyefungia. Tena mshtakiwa na mhukumiwa hakujieleza hata neno.
Leo waziri yule yule aliyefuta majuzi gazeti la Mawio leo anakuja bungeni kuzuia TBC wanaoendesha shughuli zao wasirushe LIVE bunge.
Eti kupunguza gharama na kwa kuwa wengi ya watanzania huwa wanakuwa makazini na katika shughuli zingine wakati wa mchana.
Wakati TBC wanarusha harusi LIVE na mikutano ya CCM wakati wa kampeni je kulikuwa wanatumia majani na sio pesa? Walikuwa wanarusha mikutano ya CCM usiku?
Ni aibu sana kwa serikali inayoogopa wananchi wake kupata habari na kuogopa vyombo vya habari.
Ni aibu sana.
Shukrani A. Ngonyani
Januari 27, 2016,
Tanga,
0784379799
sirngonyani@gmail.com