Kwa wazazi wenza

Kwa wazazi wenza

gilldenu

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2015
Posts
2,909
Reaction score
3,026
Hasa wanawake ......

Unakuta umezaa na mwanamke kwa bahati nzuri au mbaya hamkufanikiwa kufikisha lengo la kuoana ...sasa shida inakuja pale mwanaume uliye zaa nae anataka kuoa mwanamke mwingine tofauti na wewe ulie zaa nae ....

Kwanini huwa mnawaletea fujo wale mabinti walio olewa na baby daddy wenu mnafika mbali zaidi adi kuwaendea kwa waganga kuwafunga vizazi....

Wengine kutwa kucha kuwalaani ma baby daddy wenu kwa kuwatosa kwenda kuoa kwingine shida hasa ni nini....
Maana kama angekupenda angekuoa sasa ndoa imeshindikana mwachie mwenzio alo bahatika na ndoa afurahie maisha ya ndoa.

Me nadhani kuzaa na mtu sio tiketi ya ndoa kama haijapangwa muoane haijapangwa tu....

Muwaache wenzenu waenjoy maisha na sio kuwaonea kinyongo na wivu...
 
Unadhani wanafanya kwa kupenda? Pole sana, usijitambe maana hata yeye hakupenda kuachwa ili wewe uolewe.
Kukubaliana na ukweli unaouma ni ngumu sana, jaribu kumuelewa kama ambavyo nawe unataka akuelewe.
La moyoni hilo jamanii!
Ni sawa na yeye aachwe hapo aolewe mwingine
 
Unadhani wanafanya kwa kupenda? Pole sana, usijitambe maana hata yeye hakupenda kuachwa ili wewe uolewe.
Kukubaliana na ukweli unaouma ni ngumu sana, jaribu kumuelewa kama ambavyo nawe unataka akuelewe.
Halafu hiyo mbona ipo wazi tu, atafatwa kwa mbwembwe atajiona pussy so good kumbe huwa ni swala la muda tu hata aliezaa alifatwa kwa gia hizo hizo
 
Tatizo ni ubinafsi wewe unaangalia upande mmoja tu. Sidhani kama kuna mwanamke anapenda mwanaume aliezaa nae amuache hlf akamuoe mwanamke mwingine labda kama hampendi.

Nawewe uliezalishwa na kuachwa usimfanyie fujo mwenzio maana kosa sio lake. Ukiona mtu amekukataa jua huyo sio wako usilazimishe.
 
Hicho kitu kinauma mnoo, tena sana tuu jamani! Hakuna kitu kizuri kama mtoto kulelewa na baba na mama tena kwa mapenzi yote!

Hiyo hutokea lakini kufanya fujo nayo sio poa!
Welcome back
 
Hv labda niseme mfano ulio hai je kama niliye zaa nae kaenda kwao namwambia arudi ataki na anamausiano na mtu mwingine ila siku akiwa na genye anakuja anapata dozi anaondoka ukimwambia rudi tulee mtoto wetu ataki ,na baadae mmekaa nae unaona anachati na hawara zake ,sasa ukaamua kutafuta mwanamke mwingine ukaamua kufunga nae ndoa hapo atalaumu kweli???
 
yani kaka umenigusa sana hata mimi ndo kinachojitokeza kwangu sasa mtu kam huyu nikiamua kuoa mwanamke mwingine si ataumia sana

Buimchizi mpka sasa mm niko njia panda ilo jambo linanipa shida sana ,alafu mbaya ukimuuliza mzazi mwenza anakwambia nakupenda sana mme wangu, af ataki kurudi home muendelee na maisha yenu af wakati huo ana kwake na anamahusiano na mtu mwingine, yani napata tabu nimeshampa muda nimemwambia nataka nifanye maamuzi magumu so fikiria unipe jibu
 
Back
Top Bottom