Kwa asilimia kubwa mambo hayo huambatana na imani za kishirikina. Tangu lini kucha na mavi ya tembo yakamponya mtoto?
Kwa asilimia kubwa mambo hayo huambatana na imani za kishirikina. Tangu lini kucha na mavi ya tembo yakamponya mtoto?
Eeeh! Kumbe zinakuwa ni kucha na mavi ya tembo? That's weird. Ahsante kwa kunijulisha.
ulivyotoka meno utotoni, ulirusha juu ya bati au uliweka chini ya mto??
Au ulipopata kwikwi walikuwekea uzi mweupe kwenye paji la uso??
here we go again lol
Ashukuriwe MUNGU mambo hayo sikupitia. Meno mengi niliyatupa sana sana ilikuwa ni chooni (cha shimo) na kwa habari ya Kwikwi mara nyingi tuliambiwa tunywe maji au kubana pumzi. Sina uhakika kitabibu kama ndivyo inavyotakiwa kufanyika but somehow it works for me! lol!
Ni zaidi ya hapo kuna mambo mengi ambayo mengine hayafai hata kutamkwa yanayofinyangwa ndani ya vile vihirizi vidogo na kamba nyeusi viunoni mwa watoto! Tahadhari tu, USIJARIBU!
Kama mambo yenyewe ndo hayo, siwezi kujaribu.
wee naye kiazi cha chipsi.
Kasema wanaweka vitu vingi vikorkoro, afu unajibu kama ni hivyo siwezi hata kujaribu.
Ingredients za vikokoro ni nini hadi umekonkludi huwezi?
enzi za zamani haikuwa rahisi mzazi kupima uzito wa mtoto wake klinik mara kwa mara.
Kamba ile nyeusi anayovalishwa mtoto kiunoni na au mkononi, ilikuwa ni katika kusaidia kupima ukuaji wa mtoto.
Kama ikiendelea kumbana mtoto, mzazi anajua mtoto anendelea vema, ila kama ikianza kupwaya, anajua kuna shida mahala.
Pia katika kamba hizo, kuna baadhi ya mila wanazitengenezea pamoja na kitovu cha mtoto, sijawahi kujua kwa nini.
Ila siamini kama kuna ushirikina hivyo, halafu kamba kuwa nyeusi nsdhani ni pamoja na kuficha uchafu ama rangi kubadilika ukilinganisha na rangi zingine.
Sasa hivi hata usipotumia kamba, klinik zipo kwa wingi.