Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 284,456
- 738,857
Kuna baadhi ya familia zina migogoro mikubwa,ndugu hawapatani hawapendani wana chuki wivu na kijicho kati yao.Wengine wanafanyiana mambo ya ajabu hata kufikia hatua ya kuendeana kwa waganga,chuki imepitiliza.
Lakini chanzo na asili ya tatizo ni wazazi na walezi, kutokuwa fair kwa watoto wote familia nyingi zina watoto mchanganyiko! Yatima, wa kufikia na wa kambo, hapa wazazi wakuu wa nyumba wanapaswa kuwa na hekima kuu akili na busara ya malezi.
Kamwe epuka haya;
- Kumpenda mtoto mmoja zaidi ya wengine
- Kumthamini mtoto mmoja zaidi ya wengine
- Kumpa upendeleo maalum mtoto mmoja zaidi ya wengine
- Kumnyanyasa na kumnyanyapaa mtoto mmoja zaidi ya wengine
- Mateso visirani chuki na mateso kwa watoto unaoishi nao ni vitu vya kuepuka kabisa
Ni kwanini nimesema hivyo?
Kuna familia hazipendani,watoto hawapendani, wana visasi na chuki na hufikia kuendeana kwa waganga ili kuharibiana kukwamishana na kuzibiana riziki hili ni jambo baya mno.
Watoto wanaumizana na kuwafaidisha waganga wa kienyeji kwasababu ya wazazi na walezi, tunaharibu na kufisha ndoto nyingi kwa ajili ya malezi yenye mapungufu makubwa kama wewe ni mzazi au mlezi jitafakari tena kwa makini na familia unayoishi nayo.