Kwa Wataalam wa magari

Charger umejibu vizuri sasa sijui ubishi upo wapi hapo nadhani kaka jambazi umemuelewa vema
 
zingatia jibu la mwalimu. jibu lipo hapo kwa asilimia 70
 

TURBO ni kitu kinachoongezewa kwenye gari na mara nyingi huandikwa ubavuni. si kila gari lina turbo ndugu yangu

kuna TURBO (kuongeza uwezo kwenye inlet and outlet valves) na INTERCOOLER (kupooza oil) ambavyo vinaongezeka ili kuipa gari nguvu za ziada angalia kwenye Pajero nyingi na malori

speed ni ile ile lakini ukumbuke kuna spedometer nyingine zinachakachuliwa hasa za mabasi
 
Kifizikia vipimo vya mwendokasi haviwezi kutofautiana, kama ni km 80 kwa saa inabaki vilevile kwa kitu chochote kinacokwenda kwa kasi hiyo. Tofauti tunayoweza kuikuta kwenye magari ni amabayo speedometer zake zinaonyesha kasi sawa wakati kasi halisi inatofautiana inawez kutokana na sababu kama vile kutofanya kazi vizuri kwa speedometer au kubadilika kwa baadhi ya vigezo vilivyotumika kupimia mwanzoni.
Kuna kitu wataalamu wanaita standard calibration, ambayo inategemea mzunguko wa ingine, msuguano (friction/resistance) ya mahali chombo kinapotembelea (surface) na ukubwa wa tairi. Ikitokea kwamba mtu amebadili tairi, mfano standard zilikuwa inchi 15 akaweka za inchi 17 bila kufanya upya calibration, speedometer inaweza kusoma 80km/h wakati in reality gari inaenda 100km/h.
 
Ujue speedmeter inachukua vipimo from the end part of gearbox, maanake ule mzunguko baada ya kutoka kwenye engine, kupitia kwenye gear itakayokua inatumiwa kwa wakati huo, from gearbox propeller shaft ineconnect kwenye diff na kugeuzwa dirrection kwa 90 degrees kwenda kwenye matairi, sasa hii part kutoka kwenye gearbox mpaka tairi linapogusa surface ndizo zinazotofautiana kati ya starlet na mabasi, obvious gear wheels diameter katika diff za starlet ni ndogo kuliko za basi hivyo tayari kunakupishana kwa mzunguko na pia diameter za matairi zinapishana na hivyo tena kutofautisha mzunguko ndio maana speedmeter zinaweza kuwa zinasoma sawasawa ila mwendo halisi ukapishana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…