kwa upande wangu mimi week iliyopita nimeagana na samsung nafikiri sitakaa ninunue simu za aina hiyo tena sababu ni hizi hapa mwaka jana nilinunua samsung galaxy Note 3kwenye duka moja maarufu hapo posta mpya walinipa na warrant ya mwaka mmoja bei ilikuwa ni laki 9 wakanipunguzia ka 20 baada ya mwaka mmoja kamili kupita ghafla simu ilikuwa inanionyesha kuwa haiko registered kama vile hakuna sim card ndani nilienda nayo samsung j mall nikiwa kwenye foleni ya kumuona muhudumu kati ya watu watano waliokuwepo mbele yangu watatu walieleza shida zao nikiwa nasikia shida inayofanana na yangu mmoja alisema yeye alitokanayo nje na ilipofika hapa alitumia kwa siku mbili ikaanza hiyo shida kwa ujumla wote tuliambiwa kama hatuna warrant basi simu hizo zitakuwa zimekufa japo kila kitu kinafanya kazi vizuri kwa maana kama ukiipa wifi toka simu nyingine unaweza kusoma mambo yako kwenye whatsapp email nk shida ni sim card tu hatosoma tena niliingia kwa mafundi wa mtaani kwa mapokezi walijitapa wao ndio pekee wanaweza samsung hawawezi hilo niliambiwa nirudi baada ya masaa matatu tu lakini niliambiwa bado bado mpaka ikafika masaa 48 kwa wakati nikisubiri nilianza kutafuta solution kwenye youtube kuna page niliingia nikakuta watu 327,000 wanatafuta solution ya tatizo hilo na waliojaribu kutoa maelekezo ya kulitatua majibu ya coments ya waliojaribu kufuatilia msaada wa maelekezo nikuwa walishindwa kutatua tatizo kulingana na maelezo yaliyotolewa mmoja wa fund wa mtaani aliniambia anasimu 3 zinatatizo hilo ameweza kutengeneza moja lakini pia hajadhubutu kumrudishia mteja kwakuwa inaweza kuwa hewani masaa mawili then ikarudia kuonyesha haiko registered binafsi najiuliza kwanini wanatengeneza simu ambazo ukitoka nayo nchi moja kwenda nchi nyingine inaanza kukuletea matatizo zamani ilikuwa haiko hivyo naogopa kuingia kwenye mtego wakati nanunua hiyo simu kuna mwenzangu mmoja alinunua sony experia z haina shida na wala sijasikia au kusoma matatizo yasimu za sony au labda kwakuwa haziko nyingi hivyo kaka kabla hujanunua soma mitandao kupata choice ya uhakika kama unataka kununua simu ya hela nyingi