Kwa Wapenda maendeleo Kutoka Jimbo la Busega (CHADEMA)

Bukutonaga

JF-Expert Member
Jan 18, 2011
246
46
Habari ndugu wana JF!

Napenda kuanzisha uzi huu kwa ajili ya kutengeneza system yetu mapema ni vizuri tukijuana ili kuweza kutengeneza system iliyoiva kama mnavyojua Jimbo letu lina challenge nyingi,Hivyo nimeona tuanze kutafutana ili kujua tuna vijana/wana Busega wangapi wenye mapenzi na chama.

Ni vizuri tukija na kitu kwa ajili ya kwenda sasa kwa wazee/wazazi na ndugu zetu ili jimbo letu tuliendeleze kama tunavyojua ukitaja maendeleo ktk nchi lazima uangalie pia kama CDM ipo maeneo unayotoka hapo tunaweza kutoka,Mimi napatikana Mwanza mjini na ni Eng. ktk mambo ya IT so as the time goes on tutakuwa na email ya wana-busega kila mtu atakuwa ana Post views zake kule.

Nawakilisha!
 
Umefanya vizuri lakini kwa sababu hii ni cyber space si ajabu watu wasikuamini sana labda ungeenda busega na kufanya inventory ya wapenzi wa maendeleo ya busega kwa chama kipi
 
Umefanya vizuri lakini kwa sababu hii ni cyber space si ajabu watu wasikuamini sana labda ungeenda busega na kufanya inventory ya wapenzi wa maendeleo ya busega kwa chama kipi

Aksante kwa hilo ila kutokana na shughuli zangu huwa nafika jimboni kila mwezi mara 2 nimejaribu vijijini na hata Centre kubwa kama Ramadi,Nyashimo,Badugu,Nyaluhande na Nyangili kote watu wanaitaka CDM so na sisi ambao hatupo busega ni vizuri tukiwa na Mikutano yetu kupitia mtandao kama JF na kwingineko tuakawakilisha mawazo yetu juu ya hili.

Mwamko jimboni ni mkubwa sana!
 
Mkuu panua wigo hadi Bariadi tuwe wengi.
 
Hivi watu wa RULAYU,JISESA,SANGA,RUKALANGWA,IGEGU,MWAMONDI,NGUNGA A+B,MWAMAGIGISI,MKULA,MWAMWENGE,MALILI,MALANGALE,SHIGALA,NG'WANIGA,RWANGWE,GININIGA,MIZWALE,MWAMAGULU,NYASHIMO NA NYAMIKOMA wote wameshapata kweli hii elimu ya uraia?.
 
Anzeni harakati mapema, fungueni matawi katika kila eneo la jimbo la busega.
Yupo mpuuzi moja alipigwa chini kwenye kura ya maoni 2010 Masunga Chegeni, tukadhani angepeperusha bendera, kumbe alikuwa mnafiki. Kuweni makini naye.
 
Jimbo haliwakilishwi kwa kibofya(keyboard)nenda field acha hizo

Kila siku mambo mazuri huanzia jikoni hapa ni mahali pazuri sana pa kupika mambo na ndiyo maana watu mnachangia,ktk huu uzi mimi nataka wana-Busega ili tutengeneze kijiji.
 
Anzeni harakati mapema, fungueni matawi katika kila eneo la jimbo la busega.
Yupo mpuuzi moja alipigwa chini kwenye kura ya maoni 2010 Masunga Chegeni, tukadhani angepeperusha bendera, kumbe alikuwa mnafiki. Kuweni makini naye.

Aksante Mungi kwa tahadhali ni kweli tunatakiwa kuwa makini sana na watu hasa wanaofata upepo na jua jimbo linataka mtu mwenye hoja na uchungu kwa wananchi wale kweli kunatia hasira sana ukifika kule.So tuamke ili jimbo tulipatie mtu makini.
 
Hivi watu wa RULAYU,JISESA,SANGA,RUKALANGWA,IGEGU,MWAMONDI,NGUNGA A+B,MWAMAGIGISI,MKULA,MWAMWENGE,MALILI,MALANGALE,SHIGALA,NG'WANIGA,RWANGWE,GININIGA,MIZWALE,MWAMAGULU,NYASHIMO NA NYAMIKOMA wote wameshapata kweli hii elimu ya uraia?.

Kwa maeneo uliyo yataja mkuu baadhi hatujayafikia maeneo haya najua ni potential sana kama sanga,Rukalangwa,Mwamagigisi,Gininiga ni kama kiasi tu ila mwamagulu siyo pagumu mm natokea Nyaluhande so mwamagulu ni pazuri sana.Mpango wangu ni kupeleka viongozi wa ki-mkoa na kitaifa ktk baadhi ya maeneo na wabunge ili tukafungue matawi kule so tushirikiane mapema tu kupeana details za maeneo yetu.
 
Tujipangeni mapema maana naona Magu yetu hatuna maendeleo tangu kipindi cha Erenest Nyanda until now tunajivuta tu majimbo yenye wasomi wengi wakila ina lakini maendeleo ni chini kabisa naomba tujipange maana hata mimi kweli ninauchungu na wilaya yangu japo niko mbali kimasomo lakini kwa msaada wowote utakao hitajika tutasaidiana il tu cdm iweze kuyatwaa hayo majimbo Magu mjini,busega, bariadi magharibi na mashariki tutakuwa tumeunganika na meatu. tuko pamoja mkuu nawatakieni kila la kheri.
 
Mwanaweja nakushukuru sana kikubwa mimi nta create email yetu afu ntawapatia members ambao tupo serious na hili password ili wote tuimiliki zinatakiwa fikra pevu b4 mda hauja enda sana.
 
ndugu mbona nampango wa kwenda pambana na bwana mapesa .mwezi wa 9 tutakuwa tunafanya uzinduzi wa nguvu ya umma.

Mkuu kama unampango huo ni vizuri. Najua bwana mapesa aliomba achaguliwe kwa mara ya mwisho sidhani kama atagombea tena. Lakini saa nyingine siasa ni tamu anaweza akataka tena.

Jiandae sana maana wanyantuzu wa kule wametekwa sana na huyu jamaa kwa kutumia mbina. Sijui strategy gani inabidi uitumie. Nadhani inabidi utumie vijana zaidi wa maeneo hayo Na hasa kuhamasisha wajiandikishe kwa wingi.

Mimi ninaona jimbo la chenge ndo rahisi kulichukua kama tutapata mgombea machachari maana wanyantunzu wanapenda mtu mwenye viijembe na mwenye uwezo jukwaani.

Chadema watafute mgombea mzuri bariadi watamvua chenge na hata mapesa kwa urahisi sana. Chenge ni rahisi sana kumng'oa ila mapesa kunakaugumu kwa sababu ni jamaa anaweza sana vijembe majukwaani na wanyantuzu wanapenda sana hivyo vitu.

kila la kheri mkuu!
 
Nimekupata, Maeneo ya Nyashimo na Nyanh'anga pale mwamko ni mkubwa sana, wanhitaji starter up.
 
My plan ni kwamba kabla mwaka huu haujaisha nitaweka kambi kwa miezi kadhaa jimboni Busega kwa lengo la kueneza elimu ya URAIA na M4C. Nilimwamini sana Dr Kamani lakini nimebaini kwamba hataweza kuwakomboa wanabusega kwasababu mazingira aliyonayo ndani ya ccm hayam-support kuleta ukombozi wa kweli.
 
Back
Top Bottom