Kwa wapenda hekima za mapenzi tu

Ryan The King

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
2,788
2,690
Basi naiwe amani na furaha wana-JF wenzangu,

Andiko hili liwe hekima kwa wenye hekima, nuru kwa waliovipofu na liwe ukungu kwa wapumbavu, watu wasiojua umuhimu wao wenyewe.

Basi umshukuru Mungu maana ndio umezaliwa. Walioomba kuja huku walikuwa ni wengi lakini ukapewa wewe neema, basi ifurahie Neema hii ya kuishi.

Nawe uishi kwa akili utakapokuwa duniani, uusikilize moyo wako kwa uangalifu usije ukajikwaa. Jichunge na Maneno usiyoyajua, mafundisho yapotezayo ambayo hayana maana yoyote kwa nafsi yako zaidi ya kukuchafulia barabara.

Nawe utaona wengi kwa wengi, wapitao na wapitishwao. Basi uchunge moyo wako usije kujitwalia Mwanamke asiye na hekima moyoni mwake. Mwanamke ambaye kwa nje amejipamba kwa mavazi ya pamba na Sufi, amajiremba kwa mapambo ya gharama lakini moyo wake ni bei nafuu. Basi uangalie macho yako yasije kujikwaa katika yale uyaonayo.

Macho huona chochote bali wewe chagua vya kutazama. Usiupe Uhuru moyo wako kujiamulia vile utakavyo kwa maana moyo hujitafutia masumbufu ya kufisha.

Upitapo njiani usiangalie chini ukashindwa kuona mbele kwani hakika wewe ni mwanaume ni wajibu wako kuangalia Yale Mungu aliyoyaumba kwaajili yako ijapokuwa si yako.

Mpende sana Mwanamke akupendae, mlinde na mfanye ajisikie fahari ya kuwa Mwanamke. Naye atakutukuza na kukutii siku zote za maisha yake. Walakini usije muonea huruma Mwanamke Bali kuwa na busara ulizopewa na Mungu mwenyezi kwa maana huruma haimfai mwanaume nayo ni aibu kwake kuwa nayo.

Jichunge na maneno ya mdomo wako uwapo mbele ya mwanamke. Kwa maana ujaposema yeye husadiki, ujapokaa kimya yeye huhofu naye asijue uliwazalo. Usiwe mwepesi kutenda ukiwa na mke wako mbele za watu wengi kwani ni aheri usifanye lolote usisifiwe kuliko ufanye lolote ukaingia aibu.

Jitukuze uwapo kwa mkeo, usiwe kinyume kwa kujidunisha kwani Mwanamke hapendi mwanaume dhaifu hata kwenye maneno tuu.

Usimruhusu mkeo akaishi kwa Uhuru bila hofu katika nyumba yako. Kwani ni akheri aishi kwa woga kuliko kuishi akiwa na amani.

Wanawake husema maneno mengi kwa kujifariji lakini mioyoni mwao hujawa na huzuni na simanzi kuu.

Nawe utakapojitwalia mwanamke usijitie uchungu kwake bali jifurahishe kwa yale majaliwa yenu. Mpe utamu naye atakupa utamu, nawe angalia usije utia uchungu moyo wake naye akakutia ganzi ya maisha.

Maisha ni leo, naam kesho ni kwa wachukianao lakini wapendanao husameheana kabla ya jua kuzama.

Mme mjinga humdharau mke wake asijue yu ajivua tupu zake nje.
Mwanamke asiye na akili hujipatia Mme mpumbavu kwa kutoangalia chemchem za moyoni. Hutazama pesa ambazo huenda kuuza furaha yake. Naye huenda dukani kununia mambo ambayo husema mbona sikupata furaha katika hili asijue aliuza furaha yake kwa fedha za mwanaume mpumbavu.

Mwanaume mjinga huamini maneno ya mwanamke, naam hupumbazwa na sauti yake. Bali mwenye hekima hutunza kumbukumbu.

Ndege hupaa kutoka chini(mtini) kwenda angani. Naye huangalia tena chini alipotoaka. Mwanamke mwenye hekima hufananishwa na ndege huyo bali Mwanamke mpumbavu ni Kama ndege aliyepaa juu na kukataa kuangalia chini alipotoka akakosa pakutua.

Usije ukampa Mtu tupu yako kwa tamaa ya moyo kwani usijejiongezea uchungu katika siku zako za mwisho.

Heri mtu yule aitunzaye nyeti yake isipulizwe na kila upepo wa nje isipokuwa wa nyumbani kwake.

Basi nanipumzike kwa maana hainifai kuendelea ikiwa elimu ni nyingi duniani lakini watu wamechagua ujinga.

~MICHAELRAY.
TAIKON WA FASIHI.
 
Siku hizi wahubiri wengi. Ameeeenn baba mchungaji.

Ila punguza kumsema vibaya mwanamke,kwan kuwa mwanamke sio dhambi au laana.
 
Basi naiwe Amani na furaha wana-Jf wenzangu.

Hapo ulipo sema " Usimruhusu mkeo akaishi kwa Uhuru bila hofu katika nyumba yako. Kwani ni akheri aishi kwa woga kuliko kuishi akiwa na amani. " ndio umenipoteza aisee.

Kwa maana hiyo nikae nimemuwekea bastola au? Anyway my point is, mimi siwezi kumfanya mtu asiishi kwa amani, kwani nimekaa na mama muda mrefu na kanisomesha kwa shida shule za International. Siwezi kumfanya mke wangu aishi kwa hofu. Women are our best friends. That's the advice my mother gave me.

Nina imani kuwa akiwa mke mwema hutaijaji kumfanya aishi kwa hofu. Ukioa bomu, ni bomu tu. Aishi kwa hofu au la.

My two cents. Una ushauri mzuri, asante.

-callmeGhost
 
Nakazia, mwanamke asiwe huru kupita kiasi wala asiwe na hofu kupita kiasi.

Unapaswa uhakikishe unabalance hayo mambo
 
Back
Top Bottom