Kwa waomba ushauri wote JF zingatieni haya..

Kwa waomba ushauri wote JF zingatieni haya..

Namge

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2016
Posts
1,446
Reaction score
2,002
Wasalaam wana janvi..

Bila kupoteza mda naomba kutoa maoni yangu juu Ya watu tunaotaka ushauri JF hasa wale ambao hakika wanakuwa kwenye uhtaji wa Mawazo na ushaur toka humu..
Wanasaikolojia na watu wa guidance na councelling ntaomba Msaidie zaidi
Kuna vitu muhimu vya kufahamu hasa pale unapokuwa unataka ushaur ama kutoa ushaur navyo ni
1.Jinsia ya mtu,Hii ni muhimu Sana kwa washaur kujua jinsia.. Inasaidia Sana Maana makuzi na ukuaji wa jinsia hizi mbili hutofautiana na hata mchakato wa uchakataji wa taarifa na maamuz hutofautiana.. Ko ni muhimu kujua jinsia yako

2.Umri wa mtu.. Ni muhimu Sana katika kutoa ushaur kwa mtu.. Umri husema vitu vingi kwa mtu.. Kwa maana kila umri Una mambo yake.. Na tabia zake
Kwahivyo kufahamu umri wa mtu kabla ya kumshaur ni muhimu. Kwa mfano Kuna tabia ambazo mtu kuwa nazo katika fulani ni sawa.. Na katika umri mwingine inakuwa si sawa..

3.Asili Ya mtu(ukanda anaotoka) .. Ambayo hudokeza Utamuduni na vitu vingine ambayo huathir sehem kubwa ya Maisha ya mtu


Kwa hiyo waomba ushauri wote Naomba Tuwe tunadokeza mambo hayo
Muhimu Ili kupata ushaur murua

Wajuzi zaid mtaongezea hapo karbuni
 
5.aina ya familia aliyo toka mfano kalelewa na mama pekee au baba, au na bibi hii uonyesha aina ya makuzi aliyo yapata kwa asilimia kubwa malezi ya namna hii watoto wengi uwa na mapungufu kadhaa.
 
6.ambatanisha Picha na kadi la clinic ili tuweze kukushaur sometimes haya mafeki I'd na avatar unakuta unamshaur shemale agrrrrrrrrr
 
Na watu waache kuleta story za uongo humu, mnatuchosha jamani.
 
  • Thanks
Reactions: THT
7. Uanishi na mtiririko mzuri wa tukio lako.
Kuna wengine wanaandika tu weeee bila hata kuweka aya kwenye stori zao mpaka unapata ugumu kuusoma.

8. Matumizi mazuri ya lugha pia husadia watu kukuelewa vema na ushauri mzuri pia utapatiwa.
 
10. Muomba ushauri lazima pia ajue kuwa katika hao anaowaomba huo ushauri kati yao kuna mwendawazimu mmoja kati ya wanne.
 
11: kuwa tayari kupokea ushauri wowote

12: usisahau, za kuambiwa changanya na zako
 
13. Usisahau kuleta mrejesho.

Hii itatusaidia wana JF kuona manufaa ya michango yetu.
 
14. Usifunge PM yako ili wanao taka kukupa ushauri zaidi wapate kukutumia ushauri wao huko.
*hii ina wahusu sana jinsia ya KE
ahahaha nimecheka kwa sauti adi walio lala wameamka.
 
15. Kujifunza kuwa wawazi kwa mnayoandika ili mtu ueleweke vizuri na kuvutia mtu kutaka kukujibu. Bila kusahau kuacha zile dharau za kukosoa wanaochangia maana hata ambaye hayupo hivyo, ataamua kuacha kuandika jambo muhimu kwako.
 
Back
Top Bottom