Kwa wanaume tu: kama ni wewe unakutana na kisirani hiki utafanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wanaume tu: kama ni wewe unakutana na kisirani hiki utafanyaje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by vukani, Jan 3, 2012.

 1. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kuna jamaa mmoja alikuwa na rafiki yake anayeishi maeneo ya Ukonga naomba nimtambulishe kwa jina Ulimbo , sasa siku moja wakapanga na rafikiye anayeishi maeneo ya Tabata, (naomba huyu tumuite Kizito) wakutane kwenye Baa moja maneo ya Mwenge wajumuike pamoja na kupata moja moto moja baridi. Kizito alifika pale na usafiri wake na akamkuta Bwana Ulimbo ameshafika zamani.

  Wakati wanendelea kupata kilaji a.k.a ugimbi, Bwana Kizito akapata mgeni, hakuwa mwingine bali mfanyakazi mwenzie ambaye alifika mahali pale kama nasibu tu (Coincidence), Bwana Kizito akamtambulisha yule Binti kwa Bwana Ulimbo ambaye hakuwa ameoa, na kisha wakajumuika pamoja na kuendelea kupata vinywaji.
  Muda wote wakati wanakunywa, Ulimbo alionekana kuvutiwa na yule Binti, hivyo muda wote alikuwa bize akimdadisi kutaka kumjua zaidi. Walizoeana ghafla na hatimaye walibadilishana namba za simu. Ilipofila usiku, yule Binti aliomba kuondoka, lakini Ulimbo akaomba kumsindikiza, walipofika nje ya Baa, yule Binti akamuaga Ulimbo kuwa anawahi kupanda Daladala kwani ilikuwa ni usiku majira ya saa nne hivi.

  Ulimbo alimuuliza kama anaishi wapi, yule Binti alimjulisha kuwa anaishi Mwananyamala, Kizito alimuomba amsubiri pale nje, akamuage Bwana Kizito ili aje amsindikize. Ulimbo alikwenda kumuomba Kizito Gari lake kwa kuwa yeye hakuwa na usafiri ili amsindikize kimwana maeneo ya Mwananyamala. Kizito alimpa gari lakini alimtahadharisha kuwa aendeshe kwa makini ili kuepuka ajali. Ulimbo alimhakikishia Kizito kuwa atarudi salama. Alichukua gari na kuondoka na yule binti kuelekea Mwananymala, walipofika njiani Ulimbo alisimamisha gari kwenye duka la dawa na kumuomba binti amsubiri ili akanunue dawa, kwani mdogo wake anasumbuliwa na Malaria na kuna dawa aliandikiwa angependa kumnunulia.

  Baada ya muda alirejea ndani ya gari, na kuondoka, walipofika maeneo ya Mwananyamala, Ulimbo alisimamisha gari tena na kudai kuwa anajisikia kwenda haja ndogo, yule binti alimshauri waendelee na safari kwani nyumbani kwake anapoishi sio mbali hivyo wakifika atajisaidia hapo kwake kuliko kujisaidia njiani. Ulimbo alikaidi ushauri wa yule binti akidai kuwa amebanwa. Alishuka na kuzunguka nyuma ya gari aliporudi akazima gari na hadithi ikageuka, ilikuwa ni kama Swala ndani ya himaya ya Chui, Ulimbo hakukubali kumrejesha binti yule bila kumuonja, na kweli baada ya kutumia maneno matamu kama asali hatimaye binti akajikuta akikubali kumpa ulimbo utamu lakini kwa masharti ya kutumia Kifanyio a.k.a Condoms.


  Kumbe Ulimbo aliposimama kwenye duka la Dawa hakuwa akitaka kununua dawa bali alitaka kununua Condoms kwa kuwa alishayapima maji na kuyaona kuwa hayakuwa na kina kirefu hivyo isingemuwia vigumu kuvuka hata bila mtumbwi (Yaani isingemgharimu kutafuta Guest House ya chapchap).
  Sharti la kutumia Kifanyio lililotumiwa na Binti halikuwa kikwazo, Ulimbo alishakuwa nazo zamaani, (Wanaume waasherati huwa wana akili za ziada) Zoezi likafanyika mle mle ndani ya gari kisha akampeleka Binti nyumbani na kumshusha na kuagana kwa Mabusu kemkem.

  Alirudi pale Baa na kumkuta Kizito akiwa na ameungana na jamaa wengine wawili, hivyo wakaendelea kupata vinywaji hadi usiku wa saa sita hivi. Kwa kuwa Kizito ni mtu na familia yake akawaaga wenzie na kuondoka zake kurudi nyumbani.
  Asubuhi mkewe Kizito alimuamsha mumewe na kumuomba funguo za gari ili waende Kanisani, kwani Kizito alidai kuchoka hivyo alimuomba mkewe aende na watoto, yeye wamwache apumzike.

  Mkewe alipofika kwenye Gari aliamua kulifanyia usafi kwa kutoa Kapeti za gari na kuzikung'uta na kisha kuzirejesha ndani ya gari, alianza na kapeti za mbele na alipotoa kapeti za nyuma……….. Lahaullah……….. akakutana na Kifanyio kilichotumika kikiwa bado kina ubichi………….
  Mwanamke yule alikurupuka na kwenda ndani kumuita Mumewe na kumtoa nje….walipofika kwenye Gari alifungua mlango wa gari wa nyuma na kumuonesha mumewe kile Kifanyio kilichotumika…… Mumewe alishikwa na Butwaa na kujikuta akitamka…………….. "Aaaaaaakh Ulimbo umeiponza masikini"……………

  Je mume atawezaje kumuelewesha mkewe mpaka amuelewe?
   
 2. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Najua mko bize, nitafuatilia maoni yenu bidae...........................
   
 3. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hiki ni kisa cha kweli na sio fiction, naomba muelewe!
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Wanaume wako bar wanakunywa saa hizi, wengine wanapiga story na wake zao, wengine wanacheza na watoto, wengine ndo wanamalizia malizia kazi wape muda.
   
 5. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Aaa kwani kazi kumfahamisha mwanamke mwenye akili, si yale majinga tu ndo yana kuwa hayataki kusikiliza, na yana anzisha vita.

  Ndo siku zote ukitaka kutest mwanamke mwenye akili, ndo utamjua hapo.
   
 6. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #6
  Jan 3, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kabla hata sijatoa maoni, tukubaliane tu kuwa wewe ndiye huyo binti unayemzingumzia kwenye hii stori, maana sitarajii ungeweza kuwa na details zote hizi kwa kuhadisiwa...
   
 7. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #7
  Jan 3, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Wengine wapo kwa saml housez
   
 8. MwafrikaHalisi

  MwafrikaHalisi JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 1,746
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Huo msala ni mzito sana, hata sijui unaanzaje kujitetea duh!
   
 9. MwafrikaHalisi

  MwafrikaHalisi JF-Expert Member

  #9
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 1,746
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Huyu ndo ulimbo mwenyewe!
   
 10. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #10
  Jan 3, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Aisay kuna badhi ya wanawake wanawasoma wa ume/boi friend zao chap chap...Yani wakisema uwongo tu wanajua pale pale.
   
 11. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,147
  Likes Received: 3,335
  Trophy Points: 280
  Inabidi aongee na huyo jamaa aliye fanya zinaa kwenye gari aje ajibu kesi.
   
 12. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  what if ulimbo naye ana ndoa na ni family friends? Utamwambia mkeo kwamba Ulimbo ndo kafanya hii maneno?
   
 13. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #13
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  story tamu sana hii..ila mbona naoana dogo kwenye kusuruhisha tu..unamweleza hari halisi nadhani kama mwanamke kamili ataelewa ila mihimu kupiga konde moyo kwa mwanamke kwa kumtafuta ulimbo na kuomba msamaha kwa kufanya kinyume na matarajio..kuchafua gari ya family kwa ufuksa!
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  nahisi mimi mtu mgumu saana kuishi na watu......
  yaani mtu nimuazime gari ili limsaidie kupata cheap sex?
  kwanza sikai bar na mwanamke ambae sie wangu na halafu nim introduce mtu mwingine
  tena mwanamke mwenyewe kicheche kama huyo...
   
 15. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #15
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,559
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  wewe huyoo
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  ulitaka vipi labda?
   
 17. sister

  sister JF-Expert Member

  #17
  Jan 4, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,028
  Likes Received: 3,940
  Trophy Points: 280
  kwanza ntaangalia kama mume wangu ana hii tabia au ndo mara ya kwanza? kama ni mara ya kwanza ntahitaji maelezo ya kina na kidhibitisho kutoka kwa rafiki yake huyo ulimbo kama yeye kama hvyo au ikishindikana ulimbo kutoa statement basi maelazo mazuri ya mume wangu yatanifanya nimuamini na kumsamehe baada ya kunipa maelezo yaliyojitosheleza kwamba c yeye aliyefanya hvyo.
   
 18. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #18
  Jan 4, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Yani hapo kuna ugumu gani....Yule mke wa Bwana Kizito si anajua mme wake ni mlevi? Au hajui? Kama anajua mme wake mlevi siaseme nilipokuwa bar nilijisahau nikawacha mlango wa gari wazi, sikupiga lock nashakaka sana kuna walevi wameingia nakufanya hayo.
   
 19. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #19
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kwa mwanamke muelewa si kesi kubwa hii..
   
 20. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #20
  Jan 4, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180


  YES! I know sio mwanaume.... From a womans perspective.... Hapo hata haitakiwi umuulize, hicho alicho kikuta ni ishara tu ya nini kinafanyika.... Ni kama yatoa mwongozo anza kumfuatilia huyu mtu nyendo zake ni mbovu. Amini usiamini hakuna mwanaume hapo atajicommit na kusema kua ni kweli (labda kama kakuchoka na alikua akutafutia sababu za wewe kuwaka na kusepa!)

  Hapo unaanza na applying Woman intelligence to the matter.... Taratiiibu, wajifanya hata hamna kitu umegundua; Infact waziacha humo humo wala asishtuke kua umeona. Then ndo utamkamata vizuri ipasavo!
   
Loading...