Kwa wanaopenda mabadliko hususan katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wanaopenda mabadliko hususan katiba mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Jatropha, Sep 23, 2010.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  RAIA MWEMA

  Septemba 15, 2010Nchi, demokrasia inayumba kwa Katiba iliyopitwa wakati [1]

  [​IMG]
  Joseph Mihangwa​

  [​IMG]
  NIANZE kwa hitimisho kwamba Tanzania, tangu uhuru hadi sasa, haijawahi kamwe, kuwa na Katiba inayotokana na ridhaa ya wananchi; kwa maana, Katiba zote nne zilizowahi kutumika, ikiwamo ya sasa, zilitokana ama na shinikizo la watawala madarakani, au la vikundi vya kitabaka visivyowasilisha matakwa na hisia za wananchi, lakini vyenye kuhodhi mamlaka ya kuamua mustakabali wa Taifa.

  Na kwa kuwa Katiba zote zimewakilisha daima matakwa na maslahi ya kitabaka, kwa sababu hiyo zimeshindwa kudumu kama zilivyo kwa muda mrefu kwa sababu ya kuzua mitafaruku ya ndani na kuashiria mabadiliko yasiyoepukika. Marekebisho ya Katiba hizi kwa njia ya viraka lukuki, yameshindwa kuziokoa kwa sababu ya “wakati ukuta”.

  Tanzania imepitia Katiba nne tangu uhuru, ambazo, licha ya viraka zilizofanyiwa kujaribu kuokoa hali, ni nyingi mno kwa idadi kwa viwango vya mabadiliko ya Katiba barani Afrika kuashiria “hamkani si shwari tena”. Kila badiliko (lisiloepukika) liliashiria kupitwa wakati kwa Katiba hiyo na kwa aina fulani ya mfumo wa utawala na mustakabali wa Taifa kwa ujumla.

  Katiba hizo ni kuanzia na Katiba ya Uhuru [1961], Katiba ya Jamhuri [1962], Katiba ya Tanganyika na Zanzibar [1964], Katiba ya Muda ya Tanganyika na Zanzibar [1964], na Katiba ya Kudumu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, ambayo nayo, kwa shinikizo la mazingira ya sasa kisiasa na kiuchumi, haina budi kupisha Katiba mpya, tena haraka sana.

  Katika makala haya, nitaelezea chimbuko la kila Katiba na sababu za kufutwa ili kupisha Katiba mpya; na kwa nini Katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haiwezi kusimama kwa miguu miwili.

  Tujiulize: Kwa nini tabaka la sasa la watawala na wanasiasa uchwara wanatetea kuendelea kwa Katiba hii, wakati wakielewa na kuamini fika, kwa roho na mwili, kwamba haikidhi matakwa ya sasa ya wananchi, lakini wanaropoka juu ya paa kutetea wasichokiamini? Na kabla hatujaendelea tujiulize pia: “Katiba ni nini”?

  Kwa mtazamo na fikra za Kileberali, Katiba ni vitu viwili: Kwanza, ni ramani ya mamlaka inayotoa na kufafanua jinsi mamlaka ya nchi yanavyopaswa kuwa na kugawanywa ndani ya vyombo vya nchi.

  Pili, Katiba ni mandhari (terrain) ya mkataba wenye kuhalalisha uhalali wa kutawala na utawala; ndiyo pia inayotoa itikadi na misingi ya Kikatiba na Kanuni (doctrines) – kama vile mgawanyo wa madaraka, uwajibikaji wa serikali, utawala wa sheria na kadhalika.  Kuzingatiwa kwa mambo haya yote kunajulikana kama constitutionalism, kwa maana ya imani kwamba serikali (kwa kupenda au bila kupenda) inazingatia misingi na matakwa ya Katiba kwa manufaa ya wananchi wote.
  Kanuni za Katiba na constitutionalism zinaungana ndani ya Katiba, na hivyo kufanya Katiba kuwa si tu sheria mama (sheria ya msingi) ya sheria zote, bali pia msingi mkuu wa uhalali wa kutawala.

  Watawala hupata mamlaka na uhalali wa kutawala kutokana na Katiba; na kwa sababu hiyo Katiba hufanya utawala ukubalike na kuheshimiwa.
  Tanganyika (sasa Tanzania) ilipata Uhuru kutoka kwa Waingereza Desemba 9, 1961 chini ya Jumuiya ya Madola na kuridhia aina ya mfumo wa utawala wa Uingereza ujulikanao kama “Mfumo wa Westminster”.

  Kwa mazingira hayo, Katiba mwafaka wakati huo ilizingatia na kujikita kwenye hali ya kumalizika kwa kipindi cha ukoloni mkongwe na kuhamishia madaraka kwa uongozi wa kizalendo chini ya Chama cha Tanganyika African National Union (TANU), kikiongozwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

  Kama ilivyokuwa kwa nchi zote zilizotawaliwa na Uingereza enzi hizo, Katiba ya Tanganyika au kwa jina sahihi “Katiba ya Uhuru” – (The Tanganyika [Constitution] Order in Council, 1961) ilitolewa kwenye Ofisi ya Makoloni ya Uingereza na kutiwa sahihi (to assent) na Malkia wa Uingereza Novemba 27, 1961 kabla ya kukabidhiwa kwa Serikali ya Tanganyika na kuanza kutumika.
  Chini ya Katiba hiyo, Tanganyika ilitangazwa kuwa nchi ya Kidemokrasia yenye Vyama vingi vya siasa chini ya Waziri Mkuu [Nyerere], huku madaraka ya Malkia yakiendelea kubakia akiwakilishwa na Gavana nchini.

  Chini ya mfumo huo wa Westminster, ukuu wa Bunge (Parliamentary Supremacy) uliendelea kutambuliwa na kuheshimiwa kwa kuzingatia haki na demokrasia.
  Utangulizi wa Katiba hiyo ulisomeka hivi:
  “…… Na kwa kuwa haki hizo zitatekelezwa na kulindwa katika jamii ya kidemokrasia ambayo Serikali yake inawajibika kwa Bunge huru lenye kuwakilisha wananchi, ambalo Wajumbe wake ni wa kuchaguliwa na ambayo Mahakama zake ni huru na zenye kutoa haki bila woga wala upendeleo......”
  Kwa heshima zote, niharakishe kutamka mapema hapa kwamba, matakwa haya ya aina ya Serikali na Bunge bado yanasomeka vivyo hivyo kwenye utangulizi wa Katiba yetu ya sasa (ya 1977), lakini utekelezaji wake ni kinyume, wa dhihaka na kwa njia ya ukiukaji mkubwa wa Katiba yenyewe.

  Kwa mfano, kuna ukweli gani kwamba Bunge letu ni lenye wajumbe wa kuchaguliwa (kuwakilisha majimbo na wananchi), wakati limesheheni wabunge wa kuteuliwa [na Rais] na Wabunge wa Viti Maalumu?
  Kuna ukweli gani kwamba Mahakama zetu ni huru, wakati majaji wote ni wateule wa mhimili wa utawala (Rais), kiasi kwamba “amlipaye mpiga zumari ndiye huchagua wimbo”?

  Iko wapi demokrasia ya kweli, ya kila mtu kushiriki katika uongozi wa nchi, wakati demokrasia imefungwa kwenye jela ya vyama vya siasa, ili mradi kwamba mtu hawezi kugombea nafasi ya uongozi wowote nchini (urais, ubunge, udiwani) isipokuwa kupitia vyama vya siasa, kana kwamba wananchi hawana uwezo wa kufikiri na kutenda nje ya vyama vya siasa?

  Katiba ya Uhuru ya Tanganyika ya 1961, ilikuwa na upungufu mmoja mkubwa, tofauti na Katiba za nchi huru nyingine za Kiafrika enzi hizo: haikuwa na ibara kuhusu “Haki za Binadamu”, inadhaniwa hiyo ilitokana na kupitiwa tu kwa Watunga Katiba wa Uingereza!.

  Chini ya Katiba hiyo ya Uhuru, nchi ilikamatwa na kuongozwa na viongozi wa tabaka dogo la vibwenyenye wadogo wadogo [petty bourgeoisies], likiundwa na waliojiita wanaharakati wa mapambano ya uhuru; wakiwamo viongozi wa vyama vya wafanyakazi, wafanyabiashara wa ngazi za kati, wanaharakati wa vyama vya ushirika, waalimu na watumishi wa serikali wa ngazi za chini.
  Kama ambavyo ilivyo sasa, ambapo makundi haya yamecharuka kuvamia nafasi ya uongozi wa siasa (ubunge na udiwani), ndivyo ilivyokuwa enzi za uhuru, na kusema kweli historia inajirudia, kwa wananchi wa kawaida (wasio na ubavu kifedha na kujuana) kugeuzwa watazamaji tu kwa yanayotokea nchini.
  Matokeo yalikuwa ni nchi kushikwa na kuongozwa na tabaka la vibwenyenye lenye sera zisizo na mashiko, wala mkakati endelevu katika nyanja za kiuchumi na kisiasa. Kwa kifupi, tabaka hili lilishika na kuridhia tu mfumo kandamizi wa zamani wa kikoloni kutumikia matakwa ya kikoloni, kwa jina lingine “ukoloni mamboleo”.

  Kwa mfano, chini ya Katiba hiyo, vibwenyenye hao walishindwa kuvunja/kufuta mfumo wa uzalishaji wa kinyonyaji ndani ya nchi na uhusiano wake na ubepari wa kimataifa. Kwa sababu hii, uhuru [wa bendera] kwa mwananchi wa kawaida haukuwa na maana kwake.  Kutokidhi kwa Katiba hiyo na matarajio ya wananchi kunathibitishwa na migomo mingi na mikubwa enzi hizo katika mashamba makubwa ya makabaila, iliyoongozwa na Shirikisho la Wafanyakazi nchini (TFL), kiasi kwamba mmoja wa viongozi wakuu wa shirikisho hilo, Victor Mkelo, alipelekwa uhamishoni (mafichoni) katika maeneo duni ya mmoja wa Mikoa ya Magharibi kwa miezi mitatu.  Hapo Serikali ikaweza kuzima migomo kwa nguvu za dola; TFL ikafutwa, badala yake ikaundwa Jumuiya ya Wafanyakazi (National Union of Tanganyika Workers) – NUTA, kama chama cha propaganda kwa wafanyakazi wenye njaa ndani ya nchi yenye utajiri wenye kunufaisha vitabaka.

  Haikuishia hapo, mwaka 1962, Serikali ikafuta vyama vikuu 34 vya Ushirika na Vyama vya Ushirika vya Msingi 850 vilivyokuwa vinazalisha karibu asilimia 25 ya mazao ya ndani kwa soko la nje; badala yake likaundwa Shirikisho la Vyama vya Ushirika nchini (Cooperative Union of Tanganyika CUT) kuwalewesha wakulima kwa propaganda ndani ya uchumi uliokuwa unaendeshwa kunufaisha vitabaka vya kibwenyenye vya kuibukia.

  Ndani ya TANU namo mambo hayakuwa shwari. Januari 16, 1962, kwa shinikizo la wanachama wa Bara, Mwalimu Nyerere alikabiliwa na changamoto halali, kali na zenye nguvu, zikimtaka kutoa madaraka zaidi kwa Waafrika serikalini (Africanisation) na kuwaondoa wabunge wachache wawakilishi wa mataifa mengine (minority races) ili Bunge liwe la Waafrika tupu.

  Wanachama hao walimtaka pia achukue hatua za makusudi kuhakikisha kasi nzuri ya maendeleo nchini; wakataka pia Tanganyika ipate madaraka ya ndani na kuitwa Jamhuri (kwa kumwondoa mwakilishi wa Malkia – Gavana) haraka iwezekanavyo.

  Na pale Nyerere alipoonekana kusitasita, hasa kuhusu suala la “Africanisation”, hali ya kisiasa nchini na kwa TANU ilianza kuwa tete, tena kwa kasi ya kutisha.
  Na alipoona kwamba “hamkani si shwari tena”, na kwamba nchi ingeingia katika mtafaruku mkubwa, hatari na wenye madhara makubwa, Nyerere alilazimika kujiuzulu nafasi ya Waziri Mkuu akimwachia Rashidi Kawawa kuongoza harakati, na yeye akabakia kama Mjumbe wa kawaida wa Baraza la Kutunga Sheria – LEGCO.

  Kufikia hapo, Katiba ya Uhuru ya 1961, iliyotambua ukuu wa Bunge na uhuru wa Mahakama bila mgawanyo wa madaraka wa aina ya mfumo wa Kimarekani, ilishinikizwa tu kurithi mfumo katili wa Kikoloni na kubakia kama ulivyokuwa kabla ya Uhuru. Na kwa sababu hayo hayakuwa matarajio ya umma wa Tanganyika kuhusu uhuru waliopigania, Katiba hiyo haikusalimika, ikatupwa nje.
  Katiba gani ilichukua nafasi ya Katiba ya uhuru? Kwa nini nayo haikudumu? Je, kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushindwa kwenda na wakati, itaweza kusalimika?
  ……..Itaendelea wiki ijayo.
  [​IMG]

  Simu:
  0713-526972

  Barua-pepe:
  jmihangwa@yahoo.com
   
 2. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  RAIA MWEMANchi inayumba kwa Katiba iliyopitwa na wakati (2)

  [​IMG]
  Joseph Mihangwa
  Septemba 22, 2010 [​IMG]
  KATIKA sehemu ya kwanza ya makala hii, tuliona jinsi Katiba ya kwanza ya Tanganyika, maarufu kama "Katiba ya Uhuru", ilivyototolewa nchini Uingereza na kupandikizwa kwetu kuendeleza udikteta na matakwa ya ukoloni mamboleo, kinyume na matarajio ya Tanganyika huru.

  Nilieleza pia jinsi Katiba hiyo ilivyokinzana na mazingira ya wakati huo, na kuibua migogoro na mitafaruku kwa njia ya migomo mikubwa ya wafanyakazi nchini na hata ndani ya Chama tawala [TANU] chenyewe kiasi cha kusababisha Waziri Mkuu wa Kwanza, Dk. Julius Kambarage Nyerere, kulazimika kujiuzulu wadhifa huo ili kuepusha shari, Januari 16, 1962.

  Ingawa inaelezwa mara nyingi kwamba Mwalimu alijiuzulu kwa lengo la kurudi kwa wananchi kuimarisha Chama, ukweli ni kwamba alilazimika bila kupenda kuachia ngazi kwa sababu ya mgogoro wa Kikatiba uliotishia kuvuruga kabisa mustakabali wa Taifa, amani, umoja na usalama.

  Kujiuzulu kwa Mwalimu kulifungua mlango kuweza kupitishwa kwa Katiba mpya, maarufu kwa jina la "Katiba ya Jamhuri", ili kwenda na wakati kuthibitisha ule usemi wa wahenga kwamba, "Wakati Ukuta".
  Sasa tuendelee na sehemu ya pili ili kujibu swali nililouliza: "Je, Katiba yetu ya sasa itaweza kuhimili shinikizo la wakati?"

  Muswada wa kufanya Tanganyika kuwa Jamhuri uliwasilishwa bungeni wakati Nyerere akiwa mjumbe wa kawaida wa LEGCO [baada ya kujiuzulu Januari 16, 1962] ambapo madhumuni ya muswada huo yalitajwa kuwa ni "Kumaliza urithi [legacy] wa kikoloni kwa kuhamisha uhuru wa kuamua mambo [Sovereignty] kutoka kwa Malkia wa Uingereza kwenda kwenye Jamhuri chini ya mkuu wa nchi wa kuchaguliwa".  Kwa mujibu wa Hati ya Serikali ya Mapendekezo hayo, Namba 1 ya 1962, lengo lilikuwa ni pamoja na kuwa na Mtendaji [Rais] mwenye nguvu [za ki-imla] na uwezo wa kutenda; na pia kuiwezesha Serikali kuingilia kikamilifu katika nyanja za maisha ya kijamii na ya kiuchumi ya wananchi".
  Mlengwa mkuu wa muswada huo, kusema kweli, ulikuwa ni ule mfumo [wa kidemokrasia] wa Westminster [ukuu wa Bunge] uweze kuangamizwa, na nafasi yake ichukuliwe na Rais Mtendaji, mwenye maguvu maarufu kama "Rais wa Kibeberu" [Imperial Presidency] na asiyehojika.

  Hivyo, mjadala wa muswada huo ulikutana na kupigiwa debe na wakereketwa wa "madaraka hodhi" kama kina Mwalimu Julius Nyerere [baada ya kuonja kadhia ya Januari 16, 1962] na vibwenyenye wengine, wakitamba ndani ya LEGCO kwamba mfumo wa Westminster ulikuwa haufai kwa mazingira ya Tanganyika; na kwamba, ilitakiwa "Serikali imara chini ya mtendaji dikteta kuweza kusukuma maendeleo ya nchi hii'.
  Utaratibu uliotumika kupitisha Katiba ya Jamhuri 1962 nao ulikuwa na walakini, na unahojika pia. Ikumbukwe kwamba, wakati huo Tanganyika bado ilikuwa inazingatia [mfumo] utamaduni wa utawala wa Kiingereza ambao ulitaka wananchi kushirikishwa kujadili Katiba mpya kwa njia ya kura ya maoni.

  Lakini kinyume na utaratibu huo, Bunge, [LEGCO] la wakati huo lilijigeuza kuwa Bunge la Katiba na kupitisha Katiba hiyo kwa kuwaweka kando wananchi na hivyo kuwapokonya haki yao ya kutunga Katiba.

  Ni msimamo wa kisheria kwamba Bunge, hata liwe wakilishi kiasi gani, kwa maana ya demokrasia ya uwakilishi [representative democracy], kamwe halina mamlaka kiukweli, kisheria na kisiasa, kupitisha Katiba mpya. Lina mamlaka na uwezo tu wa kutunga sheria [legislative capacity].

  Lina uwezo pia kurekebisha Katiba, lakini chini ya utaratibu maalumu unaotajwa kwenye Katiba husika; lakini hata hivyo, limewekewa mipaka kwa kuzuiwa kufikia kiwango cha kugusa au kurekebisha muundo [structure] wa Katiba yenyewe.

  Ukiukaji huu wa misingi ya Katiba umetumika mara nyingi hapa nchini, na kufanya Katiba zilizofuata na iliyopo sasa, zihojike juu ya uhalali wa jinsi zilivyozaliwa na kuwapo kwake, kama tutakavyoona baadaye katika makala haya.

  Chini ya Katiba ya Jamhuri ya 1962, Rais [kiongozi mwakilishi wa tabaka la vibwenyenye] alivikwa madaraka lukuki, mengi ya kidikteta ili kuzima hoja, changamoto na demokrasia kwa ujumla; tofauti na enzi za Katiba ya Uhuru ya 1961 ambapo ukuu wa Bunge katika kusimamia Serikali ulitambuliwa; nayo Mahakama ilisimamia na kutoa haki bila woga kutoka kwa Gavana wala Bunge.

  Chini ya katiba hiyo mpya, Rais [ambaye sasa alichukua nafasi ya Gavana/Malkia] alibeba mamlaka ya mkuu wa nchi sambamba na ya kuwa kiongozi wa Serikali. Ndiye pia aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu na sehemu ya Bunge, kwa maana muswada wa Bunge hauwezi kuwa sheria hadi [yeye] ametia sahihi.

  Rais pia aliteua Baraza la Mawaziri na alikuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo. Mbaya zaidi, Rais alihodhi madaraka ya kuongoza nchi apendavyo. Ibara ya 3 (3) ya Katiba iliyompa uwezo huo, ilisomeka ifuatavyo:
  "……In the exercise of his functions the President shall act in his own discretion and shall not be obliged to follow advice tendered by any other person".

  Katiba hii, kwa kweli, ndiyo iliyosimika "Rais beberu" ambaye tunaweza kumwita pia "Rais asiyeambilika", na Katiba zingine zote zilizofuata, na hata ya sasa, ziliendeleza na kuendeleza matakwa ya ibara hii.
  Hicho ndicho alichotaka Mwalimu Nyerere baada ya kuonja "joto ya jiwe" Januari 16, 1962 alipolazimika kuachia ngazi ya uwaziri mkuu akarejea "vijijini" kwenye Chama [TANU] kujipanga upya, na kisha kurejea kwa nguvu mpya kwa mtindo huo, Desemba 9, 1962 kufuatia Uchaguzi Mkuu wa Novemba 1962.

  Udikteta huu wa kikatiba wa tabaka la vibwenyenye uchwara [Petty bourgeoise], kama ulivyokuwa chini ya Katiba ya Uhuru, 1961, haukupita hivi hivi; kwani ulizua upinzani, shutuma na changamoto kwa nguvu mpya kutoka vyama vya wafanyakazi, vyama vya ushirika na sekta nyingine za kijamii.  Bunge nalo kwa upande wake, likitekeleza wajibu wake bila woga kama taasisi inayowakilisha matakwa ya [walio wengi] wananchi.
  Kwa kutumia kisingizio cha vurugu na changamoto hizi chini ya Katiba hiyo ya kidikteta, Jeshi la Tanganyika [Tanganyika Rifles], bila ya kutarajia, liliasi na kushikilia Serikali kwa muda wa siku mbili mfululizo likitaka nyongeza za mishahara [kutoka Shs. 105/= kwa mwezi hadi 260/=], hali bora ya maisha na kuondolewa kwa maafisa wa kijeshi Waingereza ili vyeo vyao vichukuliwe na Waafrika.

  Katika kadhia hiyo, Nyerere, ambaye kwa siku zote mbili alijificha mahali kusikojulikana, sio tu aliita majeshi ya wakoloni wetu wa zamani – Waingereza, kuja kuzima maasi na kuwanyang'anya silaha askari wake mwenyewe, bali pia alitumia nafasi hiyo kulivunja Jeshi na Shirikisho la Vyama vha Wafanyakazi nchini [TFL], ili kuzima changamoto za kidemokrasia chini ya Katiba kandamizi yenye kusimamiwa na "Rais asiyeambilika".

  Pamoja na kufutwa kwa TFL, viongozi wake walitiwa kizuizini na wengine kuachiwa baada ya siku au wiki kadhaa, lakini baadhi waliendelea kushikiliwa. Wawili wa mwisho kuachiwa mwaka 1966, ni Kasanga Tumbo [aliyekuwa kiongozi wa Wafanyakazi wa Reli kabla ya kuteuliwa Balozi nchini Uingereza na kujiuzulu; kisha kurejea nyumbani kuendeleza harakati] na Victor Mkelo, Rais wa TFL.

  Kama tutakavyoona baadaye kwa urefu, ili kuzima kabisa "choko choko" na changamoto hizi za kidemokrasia, Serikali ililifuta Jeshi [TR] la wakati huo, na kuanzisha jipya kwa jina la "Jeshi la Wananchi wa Tanzania [JWT]; TFL nalo likafutwa, badala yake kikaanzishwa Chama cha Wafanyakazi nchini – NUTA.

  Ili kuhakikisha kwamba asasi zote muhimu za kiraia zinadhibitiwa na kunyamazishwa, kwa kutumia marekebisho ya Katiba ya 1965 [kama tutakavyoona], taasisi zifuatazo za kiharakati zilifanywa kuwa ama Jumuiya za Chama/na au kuwa na wawakilishi bungeni: NUTA, CUT, Chama cha Wafanyabiashara nchini [TACC] na Umoja wa Vijana wa TANU [TYL].
  Zingine ni Umoja wa Wanawake Tanzania [UWT], Umoja wa Wazazi Tanzania [TAPA], na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambacho kwa miaka yote ya 1970 kilikuwa kipima joto cha jamii ya Kitanzania na kitovu cha fikra na harakati za kimapinduzi nchini.

  Nadiriki kutamka kwamba, kama tishio la mgomo la Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini [TUCTA] la hivi karibuni lingefanyika enzi au wakati Katiba ya Jamhuri [1962 – 1965] ikiwa na makali yake, bila shaka yoyote, kina Nicholaus Mgaya [wa TUCTA] na wenzake, yangewafika leo yale yaliyowapata kina Kasanga Tumbo, Victor Mkelo na wenzao, na pengine Chama chao kufutiliwa mbali.

  Hii inathibitishwa na kauli ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, wakati akielezea kulaani kwake dhana ya kusudio la mgomo huo, alipowatahadharisha wafanyakazi nchini ‘wanaosikiliza ya Mgaya' kwamba wasishangae ikiwa kwamba [Mgaya wao] hawatamwona tena [kwa kuwekwa kizuizini? Kufutwa kazi?]; na kwamba hatapenda kuona watu [watumishi] wakilazimika kuja kwenye meza ya mazungumzo [maridhiano] na ngeu kichwani kwa kuumizwa na vyombo vya dola.

  Kwa kauli hiyo, ni dhahiri kwamba, kama angeweza, Rais Kikwete angependa kutoa "kipigo" hicho; lakini Katiba ya sasa [angalau kwa eneo hilo] inamkaba mkono na kumpokonya kisu.  Lakini pamoja na hayo, haya ya TUCTA ni ishara tosha ya historia kujirudia chini ya Katiba isiyokidhi matakwa ya wengi kwenye mazingira ya sasa yanayobadilika haraka.

  Kadhia hii [kama ile ya 1961] ilimfanya Mwalimu Nyerere asome haraka maandiko ukutani na kuchukua hatua za dharura.

  Januari 28, 1968, chini ya wiki moja tangu tukio la jeshi kuasi, Mwalimu aliunda Tume chini ya Uenyekiti wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Tanganyika, Rashid Mfaume Kawawa, "kufikiria ni mabadiliko yapi yalikuwa muhimu kwa Katiba ya Tanganyika na Katiba ya TANU, juu ya na namna ya kuendesha Serikali kwa kuingiza nchini mfumo wa demokrasia ya Chama kimoja" [Angalia Tangazo la Serikali Na. 300, Gazeti la Serikali la Februari 7, 1964].

  Hapa tena, mabadiliko ya Katiba yaliyokusudiwa hayakushirikisha wananchi kwani, licha ya Rais kuunda tume, tayari uamuzi ulikuwa umetolewa, kama Mwalimu alivyonukuliwa akisema:
  "Sio jukumu la Tume kufikiria [na kupendekeza] kama Tanganyika iwe nchi ya chama kimoja au hapana; uamuzi tayari umekwishafikiwa. Kazi ya Tume ni kusema tu aina gani ya nchi ya chama kimoja inayotakiwa kwa kuzingatia maadili ya Taifa letu kwa misingi ambayo nimekwishaiagiza Tume kuzingatia".

  Hapa tena kuna kasoro: Kwamba, kama Bunge lenyewe halina mamlaka makubwa kama haya ya kurekebisha Katiba kiwango cha kutikisa muundo [structure] wa Katiba; ilikuaje Rais wa kuchaguliwa kujivika madaraka makubwa kama haya yaliyo nje ya mamlaka yake?

  Hapo ndipo athari za mfumo wa Rais `wa Kibeberu [Imperial Presidency], Rais asiyeambilika, zilipoanza kujionyesha kwa gharama ya demokrasia ya uwakilishi [Bunge] na wananchi na kwa kipindi chote kilichofuata hadi kupitishwa kwa Katiba ya 1977, ambayo nayo vivyo hivyo, katika na kwa mazingira ya kutatanisha.

  Kwa nini tunasema kadhia ya TUCTA na changamoto zingine za sasa nchini ni ishara ya historia kujirudia? Kama ilivyokuwa chini ya Katiba ya Uhuru [1961] na Katiba ya Jamhuri [1962], ambapo hoja kuu ilikuwa kuhusu mfumo wa uzalishaji mali, namna inavyozalishwa, nani anazalisha, mgawo wake, nani anafaidika na uchumi wa nchi na kama sauti ya mwananchi inasikika, inavumilika na kusikilizwa; ndivyo vivyo hivyo mkondo wa kero za sasa unavyoelekea kugusa msingi wa Katiba kushinikiza Katiba mpya.

  Kwa nini Katiba ya Jamhuri ilibadilika miaka miwili tu baadaye; na kwa nini Katiba iliyofuatia nayo haikudumu zaidi ya mwaka mmoja? Je, Katiba ya sasa itaweza kuhimili kishindo cha "wakati ukuta"?
  ……..Itaendelea wiki ijayo.
  [​IMG]

  Simu:
  0713-526972

  Barua-pepe:
  jmihangwa@yahoo.com
   
 3. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  RAIA MWEMANchi inayumba kwa Katiba iliyopitwa na wakati (2)

  [​IMG]
  Joseph Mihangwa
  Septemba 22, 2010 [​IMG]
  KATIKA sehemu ya kwanza ya makala hii, tuliona jinsi Katiba ya kwanza ya Tanganyika, maarufu kama “Katiba ya Uhuru”, ilivyototolewa nchini Uingereza na kupandikizwa kwetu kuendeleza udikteta na matakwa ya ukoloni mamboleo, kinyume na matarajio ya Tanganyika huru.

  Nilieleza pia jinsi Katiba hiyo ilivyokinzana na mazingira ya wakati huo, na kuibua migogoro na mitafaruku kwa njia ya migomo mikubwa ya wafanyakazi nchini na hata ndani ya Chama tawala [TANU] chenyewe kiasi cha kusababisha Waziri Mkuu wa Kwanza, Dk. Julius Kambarage Nyerere, kulazimika kujiuzulu wadhifa huo ili kuepusha shari, Januari 16, 1962.

  Ingawa inaelezwa mara nyingi kwamba Mwalimu alijiuzulu kwa lengo la kurudi kwa wananchi kuimarisha Chama, ukweli ni kwamba alilazimika bila kupenda kuachia ngazi kwa sababu ya mgogoro wa Kikatiba uliotishia kuvuruga kabisa mustakabali wa Taifa, amani, umoja na usalama.

  Kujiuzulu kwa Mwalimu kulifungua mlango kuweza kupitishwa kwa Katiba mpya, maarufu kwa jina la “Katiba ya Jamhuri”, ili kwenda na wakati kuthibitisha ule usemi wa wahenga kwamba, “Wakati Ukuta”.
  Sasa tuendelee na sehemu ya pili ili kujibu swali nililouliza: “Je, Katiba yetu ya sasa itaweza kuhimili shinikizo la wakati?”

  Muswada wa kufanya Tanganyika kuwa Jamhuri uliwasilishwa bungeni wakati Nyerere akiwa mjumbe wa kawaida wa LEGCO [baada ya kujiuzulu Januari 16, 1962] ambapo madhumuni ya muswada huo yalitajwa kuwa ni “Kumaliza urithi [legacy] wa kikoloni kwa kuhamisha uhuru wa kuamua mambo [Sovereignty] kutoka kwa Malkia wa Uingereza kwenda kwenye Jamhuri chini ya mkuu wa nchi wa kuchaguliwa”.  Kwa mujibu wa Hati ya Serikali ya Mapendekezo hayo, Namba 1 ya 1962, lengo lilikuwa ni pamoja na kuwa na Mtendaji [Rais] mwenye nguvu [za ki-imla] na uwezo wa kutenda; na pia kuiwezesha Serikali kuingilia kikamilifu katika nyanja za maisha ya kijamii na ya kiuchumi ya wananchi”.
  Mlengwa mkuu wa muswada huo, kusema kweli, ulikuwa ni ule mfumo [wa kidemokrasia] wa Westminster [ukuu wa Bunge] uweze kuangamizwa, na nafasi yake ichukuliwe na Rais Mtendaji, mwenye maguvu maarufu kama “Rais wa Kibeberu” [Imperial Presidency] na asiyehojika.

  Hivyo, mjadala wa muswada huo ulikutana na kupigiwa debe na wakereketwa wa “madaraka hodhi” kama kina Mwalimu Julius Nyerere [baada ya kuonja kadhia ya Januari 16, 1962] na vibwenyenye wengine, wakitamba ndani ya LEGCO kwamba mfumo wa Westminster ulikuwa haufai kwa mazingira ya Tanganyika; na kwamba, ilitakiwa “Serikali imara chini ya mtendaji dikteta kuweza kusukuma maendeleo ya nchi hii’.
  Utaratibu uliotumika kupitisha Katiba ya Jamhuri 1962 nao ulikuwa na walakini, na unahojika pia. Ikumbukwe kwamba, wakati huo Tanganyika bado ilikuwa inazingatia [mfumo] utamaduni wa utawala wa Kiingereza ambao ulitaka wananchi kushirikishwa kujadili Katiba mpya kwa njia ya kura ya maoni.

  Lakini kinyume na utaratibu huo, Bunge, [LEGCO] la wakati huo lilijigeuza kuwa Bunge la Katiba na kupitisha Katiba hiyo kwa kuwaweka kando wananchi na hivyo kuwapokonya haki yao ya kutunga Katiba.

  Ni msimamo wa kisheria kwamba Bunge, hata liwe wakilishi kiasi gani, kwa maana ya demokrasia ya uwakilishi [representative democracy], kamwe halina mamlaka kiukweli, kisheria na kisiasa, kupitisha Katiba mpya. Lina mamlaka na uwezo tu wa kutunga sheria [legislative capacity].

  Lina uwezo pia kurekebisha Katiba, lakini chini ya utaratibu maalumu unaotajwa kwenye Katiba husika; lakini hata hivyo, limewekewa mipaka kwa kuzuiwa kufikia kiwango cha kugusa au kurekebisha muundo [structure] wa Katiba yenyewe.

  Ukiukaji huu wa misingi ya Katiba umetumika mara nyingi hapa nchini, na kufanya Katiba zilizofuata na iliyopo sasa, zihojike juu ya uhalali wa jinsi zilivyozaliwa na kuwapo kwake, kama tutakavyoona baadaye katika makala haya.

  Chini ya Katiba ya Jamhuri ya 1962, Rais [kiongozi mwakilishi wa tabaka la vibwenyenye] alivikwa madaraka lukuki, mengi ya kidikteta ili kuzima hoja, changamoto na demokrasia kwa ujumla; tofauti na enzi za Katiba ya Uhuru ya 1961 ambapo ukuu wa Bunge katika kusimamia Serikali ulitambuliwa; nayo Mahakama ilisimamia na kutoa haki bila woga kutoka kwa Gavana wala Bunge.

  Chini ya katiba hiyo mpya, Rais [ambaye sasa alichukua nafasi ya Gavana/Malkia] alibeba mamlaka ya mkuu wa nchi sambamba na ya kuwa kiongozi wa Serikali. Ndiye pia aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu na sehemu ya Bunge, kwa maana muswada wa Bunge hauwezi kuwa sheria hadi [yeye] ametia sahihi.

  Rais pia aliteua Baraza la Mawaziri na alikuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo. Mbaya zaidi, Rais alihodhi madaraka ya kuongoza nchi apendavyo. Ibara ya 3 (3) ya Katiba iliyompa uwezo huo, ilisomeka ifuatavyo:
  “……In the exercise of his functions the President shall act in his own discretion and shall not be obliged to follow advice tendered by any other person”.

  Katiba hii, kwa kweli, ndiyo iliyosimika “Rais beberu” ambaye tunaweza kumwita pia “Rais asiyeambilika”, na Katiba zingine zote zilizofuata, na hata ya sasa, ziliendeleza na kuendeleza matakwa ya ibara hii.
  Hicho ndicho alichotaka Mwalimu Nyerere baada ya kuonja “joto ya jiwe” Januari 16, 1962 alipolazimika kuachia ngazi ya uwaziri mkuu akarejea “vijijini” kwenye Chama [TANU] kujipanga upya, na kisha kurejea kwa nguvu mpya kwa mtindo huo, Desemba 9, 1962 kufuatia Uchaguzi Mkuu wa Novemba 1962.

  Udikteta huu wa kikatiba wa tabaka la vibwenyenye uchwara [Petty bourgeoise], kama ulivyokuwa chini ya Katiba ya Uhuru, 1961, haukupita hivi hivi; kwani ulizua upinzani, shutuma na changamoto kwa nguvu mpya kutoka vyama vya wafanyakazi, vyama vya ushirika na sekta nyingine za kijamii.  Bunge nalo kwa upande wake, likitekeleza wajibu wake bila woga kama taasisi inayowakilisha matakwa ya [walio wengi] wananchi.
  Kwa kutumia kisingizio cha vurugu na changamoto hizi chini ya Katiba hiyo ya kidikteta, Jeshi la Tanganyika [Tanganyika Rifles], bila ya kutarajia, liliasi na kushikilia Serikali kwa muda wa siku mbili mfululizo likitaka nyongeza za mishahara [kutoka Shs. 105/= kwa mwezi hadi 260/=], hali bora ya maisha na kuondolewa kwa maafisa wa kijeshi Waingereza ili vyeo vyao vichukuliwe na Waafrika.

  Katika kadhia hiyo, Nyerere, ambaye kwa siku zote mbili alijificha mahali kusikojulikana, sio tu aliita majeshi ya wakoloni wetu wa zamani – Waingereza, kuja kuzima maasi na kuwanyang’anya silaha askari wake mwenyewe, bali pia alitumia nafasi hiyo kulivunja Jeshi na Shirikisho la Vyama vha Wafanyakazi nchini [TFL], ili kuzima changamoto za kidemokrasia chini ya Katiba kandamizi yenye kusimamiwa na “Rais asiyeambilika”.

  Pamoja na kufutwa kwa TFL, viongozi wake walitiwa kizuizini na wengine kuachiwa baada ya siku au wiki kadhaa, lakini baadhi waliendelea kushikiliwa. Wawili wa mwisho kuachiwa mwaka 1966, ni Kasanga Tumbo [aliyekuwa kiongozi wa Wafanyakazi wa Reli kabla ya kuteuliwa Balozi nchini Uingereza na kujiuzulu; kisha kurejea nyumbani kuendeleza harakati] na Victor Mkelo, Rais wa TFL.

  Kama tutakavyoona baadaye kwa urefu, ili kuzima kabisa “choko choko” na changamoto hizi za kidemokrasia, Serikali ililifuta Jeshi [TR] la wakati huo, na kuanzisha jipya kwa jina la “Jeshi la Wananchi wa Tanzania [JWT]; TFL nalo likafutwa, badala yake kikaanzishwa Chama cha Wafanyakazi nchini – NUTA.

  Ili kuhakikisha kwamba asasi zote muhimu za kiraia zinadhibitiwa na kunyamazishwa, kwa kutumia marekebisho ya Katiba ya 1965 [kama tutakavyoona], taasisi zifuatazo za kiharakati zilifanywa kuwa ama Jumuiya za Chama/na au kuwa na wawakilishi bungeni: NUTA, CUT, Chama cha Wafanyabiashara nchini [TACC] na Umoja wa Vijana wa TANU [TYL].
  Zingine ni Umoja wa Wanawake Tanzania [UWT], Umoja wa Wazazi Tanzania [TAPA], na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambacho kwa miaka yote ya 1970 kilikuwa kipima joto cha jamii ya Kitanzania na kitovu cha fikra na harakati za kimapinduzi nchini.

  Nadiriki kutamka kwamba, kama tishio la mgomo la Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini [TUCTA] la hivi karibuni lingefanyika enzi au wakati Katiba ya Jamhuri [1962 – 1965] ikiwa na makali yake, bila shaka yoyote, kina Nicholaus Mgaya [wa TUCTA] na wenzake, yangewafika leo yale yaliyowapata kina Kasanga Tumbo, Victor Mkelo na wenzao, na pengine Chama chao kufutiliwa mbali.

  Hii inathibitishwa na kauli ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, wakati akielezea kulaani kwake dhana ya kusudio la mgomo huo, alipowatahadharisha wafanyakazi nchini ‘wanaosikiliza ya Mgaya’ kwamba wasishangae ikiwa kwamba [Mgaya wao] hawatamwona tena [kwa kuwekwa kizuizini? Kufutwa kazi?]; na kwamba hatapenda kuona watu [watumishi] wakilazimika kuja kwenye meza ya mazungumzo [maridhiano] na ngeu kichwani kwa kuumizwa na vyombo vya dola.

  Kwa kauli hiyo, ni dhahiri kwamba, kama angeweza, Rais Kikwete angependa kutoa “kipigo” hicho; lakini Katiba ya sasa [angalau kwa eneo hilo] inamkaba mkono na kumpokonya kisu.  Lakini pamoja na hayo, haya ya TUCTA ni ishara tosha ya historia kujirudia chini ya Katiba isiyokidhi matakwa ya wengi kwenye mazingira ya sasa yanayobadilika haraka.

  Kadhia hii [kama ile ya 1961] ilimfanya Mwalimu Nyerere asome haraka maandiko ukutani na kuchukua hatua za dharura.

  Januari 28, 1968, chini ya wiki moja tangu tukio la jeshi kuasi, Mwalimu aliunda Tume chini ya Uenyekiti wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Tanganyika, Rashid Mfaume Kawawa, “kufikiria ni mabadiliko yapi yalikuwa muhimu kwa Katiba ya Tanganyika na Katiba ya TANU, juu ya na namna ya kuendesha Serikali kwa kuingiza nchini mfumo wa demokrasia ya Chama kimoja” [Angalia Tangazo la Serikali Na. 300, Gazeti la Serikali la Februari 7, 1964].

  Hapa tena, mabadiliko ya Katiba yaliyokusudiwa hayakushirikisha wananchi kwani, licha ya Rais kuunda tume, tayari uamuzi ulikuwa umetolewa, kama Mwalimu alivyonukuliwa akisema:
  “Sio jukumu la Tume kufikiria [na kupendekeza] kama Tanganyika iwe nchi ya chama kimoja au hapana; uamuzi tayari umekwishafikiwa. Kazi ya Tume ni kusema tu aina gani ya nchi ya chama kimoja inayotakiwa kwa kuzingatia maadili ya Taifa letu kwa misingi ambayo nimekwishaiagiza Tume kuzingatia”.

  Hapa tena kuna kasoro: Kwamba, kama Bunge lenyewe halina mamlaka makubwa kama haya ya kurekebisha Katiba kiwango cha kutikisa muundo [structure] wa Katiba; ilikuaje Rais wa kuchaguliwa kujivika madaraka makubwa kama haya yaliyo nje ya mamlaka yake?

  Hapo ndipo athari za mfumo wa Rais `wa Kibeberu [Imperial Presidency], Rais asiyeambilika, zilipoanza kujionyesha kwa gharama ya demokrasia ya uwakilishi [Bunge] na wananchi na kwa kipindi chote kilichofuata hadi kupitishwa kwa Katiba ya 1977, ambayo nayo vivyo hivyo, katika na kwa mazingira ya kutatanisha.

  Kwa nini tunasema kadhia ya TUCTA na changamoto zingine za sasa nchini ni ishara ya historia kujirudia? Kama ilivyokuwa chini ya Katiba ya Uhuru [1961] na Katiba ya Jamhuri [1962], ambapo hoja kuu ilikuwa kuhusu mfumo wa uzalishaji mali, namna inavyozalishwa, nani anazalisha, mgawo wake, nani anafaidika na uchumi wa nchi na kama sauti ya mwananchi inasikika, inavumilika na kusikilizwa; ndivyo vivyo hivyo mkondo wa kero za sasa unavyoelekea kugusa msingi wa Katiba kushinikiza Katiba mpya.

  Kwa nini Katiba ya Jamhuri ilibadilika miaka miwili tu baadaye; na kwa nini Katiba iliyofuatia nayo haikudumu zaidi ya mwaka mmoja? Je, Katiba ya sasa itaweza kuhimili kishindo cha “wakati ukuta”?
  ……..Itaendelea wiki ijayo.
  [​IMG]

  Simu:
  0713-526972

  Barua-pepe:
  jmihangwa@yahoo.com
   
Loading...