Jaribu kutafakari:
Wale wote wanaokihama Chama Cha Mapinduzi wakati huu wa uchaguzi na kujifanya wana uchungu zaidi na nchi yao ni kweli wanamaanisha?
Mimi nahoji kuwa ina maana misingi ya CCM imeachwa wakati huu tu wa uchaguzi?
Kama ni kweli kwani ni lazima kuita waandishi wa habari wakati wa kukihama na je wakati wanajiunga na chama hiki waliitisha hata gazeti?
Hebu hawa wachumia tumbo waache kuwahadaa wananchi kuna wengine pia shulw za kata zimetusaidia kupata elimu ya uchambuzi yakinifu.
Pili kila anayehama sasa hivi, anasema CCM ni mbaya mbona alipokuwa kwenye zile land cruiser V8, nyumba za Serikali na alipokuwa kwenye nafasi kadha wa kadha alizoteuliwa hakuona mabaya ya CCM, ubaya huu wa CCM uje tu kipindi hiki na kwanini hakuhama zamani.
Watanzania ifike mahali njaa ya matumbo na ubinafsi na roho ya kutaka vyeo vya fadhila iishe,watanzania wakiona upepo upepo huu hauwezi kuwasababisha waishi maisha yao ya anasa wanaanza kukisema vibaya chama na kuhama tena kwa mbwembwe nyiingi, hivi sasa wanaoihama CCM wanaondoka kwa mbwembwe lakini si kwa nia ile ya dhati kabisa na nina mashaka kuwa kuna nguvu kubwa sana inawavuta na itakapowatosa watabaki vinywa wazi, lakini niseme tu endapo CCM itarudi madarakani sidhani kama hawa wanaosema CCM ni mbaya kwa sasa nitawasikia tena, lakini kama ndio wale wa mabadiliko watashinda basi hawa waondokao kwa tarumbeta basi ndio mtawasikia wakiteuliwa nafasi mbalimbali(sina hakika).
Wengine hawa wanaohama wanatumia vyombo vya habari kujitangaza kwani wengine nadhani kabisa hata wananchi wa kawaida walikuwa hawawafahamu.
USHAURI WANGU KWA WANAOHAMA NA WATAKAOHAMA CCM:
Usitukane Mamba kabla hujavuka mto.Kinachoendelea kwa sasa kwa baadhi ya wanasiasa wanamtukana na.kumsema mamba kabla hawajavuka mto,sasa sijui mamba wanayemtukana wakimkuta kaachama pembezoni mwa mto sijui watavukaje jamani.
Nahisi kabisa wanaokihama CCM wameahidiwa mambo makubwa sana lakini wahenga wanasema pesa iliyopo mfukoni mwa mwenzio usiipangie matumizi ni mpaka pale itakapokuwa mkononi mwako.
Ila kwa mtazamo wangu huwezi kunishawishi kabisa kuwa umekuwa madarakani miaka zaidi 30+ na umekula mema ya CCM leo tu unasema eti kimepoteza dira au misingi je huko wanakokwenda wanapajua zaidi ya Prof. Lipumba na Slaa wanavyopajua? Ndio maana naona hapa ni maslahi binafsi na si kingine.
Haya ni mawazo yangu
20.10.2015